Nimestushwa na Bunge La Tanzania

Yaani servers zilivyojaa nyingi kiasi hata JF wameweza kununua servers zao lakini bunge wanakodisha servers space marekani?
 
Hata uyatunze mwezini, mradi yako kwenye mtandao unaomilikiwa na US basi yakitakikana yanapatikana, usijidanganye wala usidanganye wengine kwa kuwa yanatunzawa Tanzania au US ndio yanawezekana yasipatikane. Kama unataka usalama wa data zako basi uwe na mtandao tofauti na huu wa internet, data zote ambazo zina link ya aina yoyote ya kwenye internet basi zipo "vulnerable" hakuna njia yoyote ya kuzuia.

Sidhani kama data za bunge au hizo za Serikali zina siri ambayo haijulikani kwa anaetaka kuzijuwa.
Mtandao upi unaomilikiwa na US?
 
Nimeshangazwa na kusikitiswa kuona kuwa tovuti ya bunge la Tanzania ambayo inatumia ip adress 66.187.104.94linatunza mafaili yake Marekani. Kwakweli nimeshtuka kwasababu bunge ni nguzo muhimu katika nchi yetu, huwezi kutunza mafaili yake nje ya nchi.

View attachment 48362

Inakuwaje taarifa muhimu na hata zile za siri kuhifadhiwa ughaibuni? Hivi nchi husika (US) ikiamua kufunga hiyo akaunti kama walivyofanya Megaupoad, Bunge la Tanzania litafanya nini?

Mwisho natoa pongezi kwa Tovuti ya Taifa kutunza mafaili yake nchini.

View attachment 48364
Duh...!, kumbe!.
P
 
Back
Top Bottom