Nimesikitishwa sana na Walimu hawa. Hawakutumia busara kwenye hili

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
423
451
Habari wakuu,

Siku chache zilizopita imesambaa video ya Wanafunzi ambao kwa muonekano wanaonekana ni wa Shule ya Msingi (Sifahamu jina la shule). Video hii inasikitisha mno kwa kuona ambacho wanafunzi wanakiri walichofanya.

Ipo hivi, hawa wanafunzi wakiume wanakiri kuwa na na tabia ya kuingiliana wao kwa wao na wanakiri kufanya hivyo si mara moja, tabia hii si njema na inasikitisha sana hata kwa kuwasikiliza unaweza angua kilio. Sifahamu nini kilitokea ila jambo hili likawafikia Walimu na ndipo watoto hao wakaanza kujielewa kwa Walimu

Nilisikitishwa na kukerwa zaidi na akili za Walimu hao walipokuwa wakiwahoji Watoto tena kwa kuonesha sura zao na huku wakitumia maneno yasiyo ya na tafsida walipokuwa wanazungumzia kitendo kile. Walimu ni walezi wa watoto na walitakiwa kujua namna ya kuongea na watoto wale ili kuweza kuwapatia msaada/kuwakanya kwa mambo mabaya waliyofanya na sio kuwaaibisha.

Sijui kesi hii imeendaje hadi muda huu ila najiulisha maswali mengi sana:

  • Je, baada ya watoto hawa kusemwa mbele ya wanafunzi wengine/kwa mtindo ule Walimu waliofanya wanaweza kuendelea kuewa darasani?
  • Je, watoto wale mtaani wanaishi vipi ikiwa video za makosa yao zimesambaa mtandaoni?

Naumizwa sana na watoto hawa na natamani wapatiwe msaada wanaohitaji ili waendelee kuwa watoto wanaofanya mambo ya watoto na si ya watu wazima na naamini hili linawezekana.

Nahimiza watu wazima wenzangu tunaposhughulikia kesi/makosa ya watoto tuwe makini sana kwani maamuzi yetu mabaya yanaweza kuharibu zaidi ya kosa alilofanya mtoto.
 
Kila kazi na wito ila siunajua muda mwingine kukosa pesa ndo kunawafanya watu kudandia fani za watu.
 
Kimsingi kila mwenye mtoto ampe malezi mema na amfanye mtoto awe huru kumueleza maswaibu anayokumbana nayo...
Hili ni jambo la msingi sana. Na hata ikitokea wamekosea ni wajibu wetu kama wazazi kuwaonya/kuwakanya kwa namna ambayo itawabadilisha na kuwafanya wema si kuharibu zaidi
 
Oooh! Sikuwa nafahamu hili ila still wale watoto hawakufanyiwa vizuri
Yeah nilimaanisha huenda mamlaka zilishalishughulikia maana ilisambaa kama miaka minne ago na ililalamikiwa sana na wadau mbalimbali
 
Back
Top Bottom