Nimesikitishwa sana na mwendendo wa demokrasia Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,721
9,026
Tanzania ni nchi kati ya nchi za Africa ambayo inauwezo wa kwenda mbali sana kiuongozi kwenye kila eneo. Tuna rasilimali karibu zote na kwasasa tunaanza kuona jidihata za uwekezaji na uzuiaji wa rushwa.

Kitu kimoja ambacho kinaturudisha nyuma na tumerudi nyuma sana ni demokrasia. Nchi yetu inajichanganya sana. Serikali imekuwa na double personality haijui kama inataka demokrasia au demokrasia ni kikwazo. Serikali wamekuwa wanajali vitu vidogo vidogo , vijimaneno na hii hali imeanza kutuletea shida sana. Lakini kibaya zaidi viongozi wengi wa serikali wamekuwa wanajali siasa zaidi ya kujali nchi kama njia ya kujionyesha.

Inawezekana kabisa hii wiki tukaikumbuka kitendo cha Mbowe na utaratibu wake na uvumilivu wake kususia uchaguzi sio kitendo kidogo kama wengine wanavyopiga madongo hapa. Hakuna mtu mtu anajua upinzani unawatu wangapi lakini Lowassa alipata karibu 40% ya wapiga kura na kuna wengine wengi hawana vyama lakini wanapenda demokrasia na haki. Tujiulize swala dogo tu Je Watanzania 35% tu wakisusia shughuli za kimaendeleo, wakagoma, wasitoe ushirikiano na viongozi, wakawaona kama maadui itasaidia vipi nchi.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba nchi yetu itakuwa kama inapata shida na kutokuelewana kusiko na sababu. CCM tayari ina super majority kwenye bunge, Raisi anateua karibu kila kiongozi sasa kuna sababu gani ya kuingiza nchi kwenye hali hii wakati hatujui tunanufaika kwa lipi. Lissu akifa, Mbowe asigombee au Lema je itasaidia vipi nchi.

Kwa wale washabiki na mnaofikiri mambo hayatabadilika mnajidanganya maana hii siyo nzuri kwa nchi bila kuweka siasa. Na ndiyo maana nasema nchi hizi tungekuwa na mfumo ambao hakuna chama chochote cha siasa watu wanachaguliwa kama raia na kufuata katiba nchi ingekuwa mbali zaidi.
 
Umeongea maneno mazito sana kiongozi. Wengi tunao shabikia humu Ndugu zetu wako vijijini wana nyanyaswa vilivyo na hawa watu.

Watu wanaangalie leo, mtu haangaliu je leo nikifa je hawa watoto wangu nitawaacha kwenye mikono salama ya hawa watawala?
 
Kuna Waziri mmoja anaitwa "JAFO", bila aibu wala kupepesa macho leo anasema eti kususia uchaguzi ni kuwanyima raia haki yao.

Hivi inaingia akilini kweli "CCM" wamejipitisha nchi nzima bila kupingwa, wamewakata wagombea wa upinzani wote, na kama mgombea akipitishwa bila kupingwa maana yake hakutakua na uchaguzi wowote wa mitaa.

Swali kwa Jafo,

Hao wapinzani wanawanyima haki gani raia??? Au ni serikali kwa mabavu ndio wamewanyima haki raia ya kuchagua wagombea wanaowafaa na kuwachagulia viongozi kwa nguvu???

Dunia hii hakuna nchi inayo tawaliwa kwa mabavu, wajifunze kwa Saddam Hussein, Muamar Gaddafi, na Jacob Zuma.

Wasifanye watanzania wapumbavu. Ama kweli tanzania hatuna mawaziri wala serikali. Aibu hii dunia nzima.

#CCM subirini wananchi wenye hasira kali #2020, njia wanayopita ndio njia iliosambaratisha vyama tawala vyote Afrika.

#Haya yanayofanyika nchini hata raia waliokua hawana mipango na siasa/kupiga kura yatawafanya waichukie zaidi, pamoja na kujituma kuitoa madarakani. Chuki ikizidi kwa raia watajificha wapi.
 
Hiyo Ndio demokrasia Kama hujajipanga

unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani Sasa
 
Ikiwa tayari viongozi wapitishwa bila wapinzani wao kuna sababu gani ya kipiga kura? Huo diyo uhujumu uchumi? Au tuiteje jamani mnisaidie
 
Kuna watu wenye upeo mdogo wanadhani faida za upinzani ni kwa wapinzani, hawajui kuwa faida za upinzani ni kwa nchi nzima wao included.

Chama tawala kisicho na watu wa kukiamsha usingizini madhara yake si kwa Mbowe, Lema, Zitto, Seif Shariff Hamad etc, maana hawa nao watapita bali ni hasara hata kwa hawa leo ambao ni waimba mapambio na vizazi vyao.

Na hawa watendaji masikini wanaotumika kubomoa fabric ya Taifa kwa shibe, siwezi kuwalaumu sana masikini lakini laiti wangejua wanasimika mfumo wa aina gani nchini basi wangejuta na kulilia hii kazi waliyoifanya kwa mikono yao. Wanajichimbia kaburi lao wenyewe.

Katiba inasema, Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia, Magufuli aliapa kulinda katiba lakini hajali kiapo chake hiki alichoapa kwa kushika Biblia na kusema maneno "Ee Mwenyezi Mungu nisaidie" Laiti angejua uzito wa kiapo chake hicho mbele ya wanadamu na Mungu!.

CCM wanashangilia mambo haya wakidhani wanawakomoa wapinzani, Kumbe wanaikomoa nchi.
lakini hata wao wajue, Wakinyamazishwa wapinzani, Upinzani ukishavurugwa basi hata wao watabaki na option moja tu, Kukubali kuwa vikaragosi vya bwana mkubwa la sivyo watapata cha mtemakuni

Huu ni ukurasa wa huzuni sana kwenye historia ya nchi yetu, Demokrasia yetu haokuwa perfect lakini tulikuwa tumepiga hatua kubwa mbele. Magufuli katurudisha nyuma sana kwenye jambo hili
 
Fujo zote hizi kwa serikali za mitaa tu je hiyo 2020 hali itakuwaje?
Huenda tutashuhudia kituko kikubwa zaidi ya hiki
Wapinzani mtulie tu hadi 2025 tuangalie upepo huko
 
Demokrasia ni maendeleo ya watu. Maendeleo ya vitu hayana maana bila maendeleo ya watu. Tumerudi nyuma miaka 40 na kupoteza yote tuliyoyajenga kwa gharama kubwa katika kipindi cha miaka 4.
 
Kitendo cha kuwaita watendaji wa kata nchi nzima na kuwajaza ikulu kama mbuzi na kuwapa maelekezo ya kipumbavu, ilikuwa ishara tosha kuwa hili lizee ni pumbavu kabisa.

Haya ndio matokeo ya upumbavu wake, anadhani watendaji wote nchi nzima wakiwa sana ccm, itaongeza tija gani kiuchumi? ushamba na ulimbukeni utaligharimu taifa.
 
Back
Top Bottom