Nimesikitishwa sana na kibonde na clouds fm kuhusu mbunge nasari

Unaandika kwa kufikiria au ili mradi na wewe umepost.
Hivi Jamani hata hivyo, kuna tatizo gani mtu kutoa kauli ya kujitenga. Nahisi Kama Mbowe ndio alikurupuka kumuambia Nasari ametoa kauli ya kitoto.

Kama wazinzibar wanazungumzia kujitenga, kwa nini sehemu nyingine za Tanzania zisizungumzie kujitenga? Huyu Kijana anahoja ya msingi na watanzania tunapaswa kuitafakari inaweza ikawa ni the best option for us, especially kama Matakwa ya Wananchi kwenye mchakato wa Katiba na Uchaguzi wa 2015 hayataheshimiwa.

Utawala wa nchi hii chini ya Uongozi wa CCM umeshindwa kuwaletea watanzania tija katika umoja wao, Hata wazanzibar wanapopiga kelele za kutaka kujitenga ni kwa sababu wanaona kwamba Muundo wa Serikali ya Muungani hauwaletei tija,
Hivyo kama sehemu yoyote ile ya Tanzania inaona inaweza ikasimama yenyewe nje ya Ushenzi unaofanyika ndani ya Jamuhuri nawashauri waendelee kufikiria kujitenga.
 
Ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala CCM.

Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu baadhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndiyo msimamo wangu ijapokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.

Joshua Nassari (MB)


Source: wavuti - wavuti
 
mi nimeipenda hii ya kujitenga

kama watu wa kaskaz i.e Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shy, Mara,,,, wanataka kujitenga bora wafanye hivyo coz wana bandari ya tanga ambapo wataingizia bidhaa zao toka nje na watatozwa ushuru mdogo nchini kwao kama ilivyo zanzibar tofauti na utumbo unaoendelea hapa bandari ya dsm
ambapo wanaiba tu pesa za wananchi.

watu wa kaskaz pia wana viwanja vya ndege vya kimataifa, madini ya kutosha, mbuga na milima kwa ajili ya utalii na watatunza twiga wao sio kuwauza

Sijui kama umepata wasaa wa kusoma ulichokiandika.
 
salam put this idiot in his place kwenye kipindi cha mkasi,alimuuliza wewe ni ccm?mijicho ikamtoka kwa kigugumizi akajibu hapana
Mkuu Nyabingi umefanya nicheke kwani Kibonde anakataa vipi kuwa sio CCM wakati wenzake wanachomolewa kwenye media na kupewa ukuu wa wilaya???? Ana malengo yake huyo lakini asidhani CCM yake itatawala milele maana mwisho wake umekalibia!!!!

 
nimeona niwawekee kelele mnazopiga na kibine sawa na kupiga na mwenzake wa ""IV Fluconazole 200mg 8Hrly x 5/7. Inaweza saidia kwa stage 4 HIV/AIDS pt
Chenga chenga zungusha antena, funga busta, au weka king'amuzi cha startimes.................... husomeki, Hiyo picha umejiwekea mwenyewe.
 
Tumsamehe bure KIBONDE, huenda yuko kwenye last point vidudu vimeingia kichwani ndio maana anaropoka

Iweje utake kutoa kibanzi kwny jicho la mwenzio wkt kibanzi kweny mboni za jicho lako hujaweza kutoa.Kumbuka wakati ukuta na leo kwako kesho kwangu kama kufa wote tutakufa na kila nafsi itaonja mauti na usimtukane mamba kabla hujavuka mto je wewe umepima una usafi gani baradhuli wee kutwa kucha kushinda kwny vijiwe vya umbea dume zima utavalishwa kanga siku 1!
 
Kibonde ndiyo kawaida yake kushabikia na kuongezea chumvi kwa visivyo hitaji kuongezewa,ni kweli Nassari alikosea ila mbona wengi hadi rais wanakosea na hawawashupalii kama vile?
 
huyo ni mtangazaji tu, watu wa namna yake lazima wawepo ili hoja ziwe hai, kauli yake si ya jaji...huo ni mtazamo wake, kila mtu na kichaa chake.
 
Iwe kweli au la. Lakini kuzungumzia afya ya mtu hadharani ni kumnyanyapaa. Siisapot hii.
 
Back
Top Bottom