Nimesikitishwa na video aliyopost Mwanamitindo/Msanii Wolper inayomuhusu Msanii Harmonize

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,581
Habari wana JF,

Mimi kama raia mwema na mzalendo wa nchi yangu Tanzania, nimesikitishwa na VIDEO iliopostiwa na msanii WOLPER katika page yake ya Instagram ikimuonesha msanii mkubwa (Kioo cha Jamii sio Tanzania pekee bali Africa kwa ujumla) HARMONIZE akicheza mziki na mpenzi wake huku akivuta kitu kinacho ashiria kama BANGI/HASHISH au pengine ni sigara (akiificha isionekane mkononi).

Mpaka sasa sijaona vyombo husika, JESHI LA POLISI wala TCRA kikitoa taarifa ya kumwita na kumhoji, sambamba na kumpima damu/mkojo na kumkagua makazi yake ili kujiridhisha kama anatumia madawa ya kulevya (Iwe ni BANGI/HASHISH au vinginevyo) au ni sigara ama hatumii chochote.

Tumeshuhudia wasanii kadhaa wakiitwa kwaajili ya kusadikika wanatumia madawa ya kulevya, walikaa Central Police kwa siku kadhaa, walipelekwa kupimwa mkojo, walipekuliwa majumbani kwao, na kisha kufikishwa mbele ya mahakama kujibu tuhuma za kutumia madawa ya kulevya. Na baadhi yao (Wema Sepetu & Hayati Masogange) tulishuhudia wakikutwa na hatia mbele ya mahakama. Baadhi ya raia tulifurahishwa sana na utendaji wa police kwenye kufanya hivyo (Police waliweza na walitoa fundisho kwa hilo).

Tulishuhudia Mh Tundu A Lissu alipokamatwa, kwa kusadikiwa kutoa maneno ya Uchochezi & Kumtusi Mh Rais, alipopelekwa Central Police, alihojiwa na kuchukuliwa maelezo kisha walitaka kumpima mkojo kujiridhisha kama anatumia madawa ya kulevya (Japo kwa maneno yake mwenyewe alisema ALIGOMA kwenda kupima kwasababu hajakamatwa kwa kosa la kutumia madawa ya kukevya).

Ni hatua nzuri Jeshi la Police linazochukua kudhibiti madawa ya kulevya (Kwa matumizi na biashara). Hongereni,

Wito wangu hatua stahiki zichukuliwe ili kujiridhisha, sambamba na kutushawishi raia kua jeshi letu la Police linafanya kazi kwa "IMPARTIALITY AND UTMOST-GOOD FAITH" na weredi.

NB Tuna wadogo zetu, ndugu zetu, jamaa zetu, jirani zetu, marafiki zetu, na wengine wana watoto zao AMBAO NI VIJANA WADOGO SANA, wanaoweza kuingia katika janga la madawa ya kulevya either kujidunga au kuvuta bangi kutokana na ushawishi sehem tofauti tofauti, (hasa ushawishi wa wasanii ambao wameisha waharibu vijana wengi wadogo wa KIUME kuvaa HERENI/VIKUKU na KUNYOA VIDUKU/KUSUKA).

Wana haribu MILA NA DESTURI zetu kama Watanzania. Na tuwalinde vijana wetu sote kwa pamoja.

Link ya video hio;

#Kuna baadhi hamtaridhishwa na nlichoandika (mtakua ni wapuuzi msiojua nini maana ya uzalendo).

#Povu ruksa,#Kunitukana ruksa.

Ila nimetimiza wajibu wangu kufikisha taarifa hii, ili kulinda vijana wenzangu kwa ushawishi na mifano mibaya wanayopata.
 
Siyo bangi hiyo umekurupuka ni cirock!
Mkuu ulimnunulia wewe hio CIROCK? Au ushahidi upi unaashiria hio ni CIROCK? Mpaka unasema nimekurupuka???

Binafsi hujui navyochukizwa na matumizi ya madawa yakulevya, nimeshapoteza RAFIKI KIPENZI na NDUGU kwaajili ya hio kitu. Ni jambo la kumwomba mungu lisikufike na kukuepusha nalo.
 
Pole sana mkuu subili kusikia mchakato wa kuruhusu bangi ukizungumziwa bungeni na ludia Tena pole sana
 
Mkuu ulimnunulia wewe hio CIROCK? Au ushahidi upi unaashiria hio ni CIROCK? Mpaka unasema nimekurupuka???

Binafsi hujui navyochukizwa na matumizi ya madawa yakulevya, nimeshapoteza RAFIKI KIPENZI na NDUGU kwaajili ya hio kitu. Ni jambo la kumwomba mungu lisikufike na kukuepusha nalo.

Huyo uliempoteza ilithibitishwa ni matumizi ya kitu (blanton/weed )kama anachoonekana anavuta Harmonize?
 
Habari wana JF,

Mimi kama raia mwema na mzalendo wa nchi yangu Tanzania, nimesikitishwa na VIDEO iliopostiwa na msanii WOLPER katika page yake ya Instagram ikimuonesha msanii mkubwa (Kioo cha Jamii sio Tanzania pekee bali Africa kwa ujumla) HARMONIZE akicheza mziki na mpenzi wake huku akivuta kitu kinacho ashiria kama BANGI/HASHISH au pengine ni sigara (akiificha isionekane mkononi).

Mpaka sasa sijaona vyombo husika, JESHI LA POLISI wala TCRA kikitoa taarifa ya kumwita na kumhoji, sambamba na kumpima damu/mkojo na kumkagua makazi yake ili kujiridhisha kama anatumia madawa ya kulevya (Iwe ni BANGI/HASHISH au vinginevyo) au ni sigara ama hatumii chochote.

Tumeshuhudia wasanii kadhaa wakiitwa kwaajili ya kusadikika wanatumia madawa ya kulevya, walikaa Central Police kwa siku kadhaa, walipelekwa kupimwa mkojo, walipekuliwa majumbani kwao, na kisha kufikishwa mbele ya mahakama kujibu tuhuma za kutumia madawa ya kulevya. Na baadhi yao (Wema Sepetu & Hayati Masogange) tulishuhudia wakikutwa na hatia mbele ya mahakama. Baadhi ya raia tulifurahishwa sana na utendaji wa police kwenye kufanya hivyo (Police waliweza na walitoa fundisho kwa hilo).

Tulishuhudia Mh Tundu A Lissu alipokamatwa, kwa kusadikiwa kutoa maneno ya Uchochezi & Kumtusi Mh Rais, alipopelekwa Central Police, alihojiwa na kuchukuliwa maelezo kisha walitaka kumpima mkojo kujiridhisha kama anatumia madawa ya kulevya (Japo kwa maneno yake mwenyewe alisema ALIGOMA kwenda kupima kwasababu hajakamatwa kwa kosa la kutumia madawa ya kukevya).

Ni hatua nzuri Jeshi la Police linazochukua kudhibiti madawa ya kulevya (Kwa matumizi na biashara). Hongereni,

Wito wangu hatua stahiki zichukuliwe ili kujiridhisha, sambamba na kutushawishi raia kua jeshi letu la Police linafanya kazi kwa "IMPARTIALITY AND UTMOST-GOOD FAITH" na weredi.

NB Tuna wadogo zetu, ndugu zetu, jamaa zetu, jirani zetu, marafiki zetu, na wengine wana watoto zao AMBAO NI VIJANA WADOGO SANA, wanaoweza kuingia katika janga la madawa ya kulevya either kujidunga au kuvuta bangi kutokana na ushawishi sehem tofauti tofauti, (hasa ushawishi wa wasanii ambao wameisha waharibu vijana wengi wadogo wa KIUME kuvaa HERENI/VIKUKU na KUNYOA VIDUKU/KUSUKA).

Wana haribu MILA NA DESTURI zetu kama Watanzania. Na tuwalinde vijana wetu sote kwa pamoja.

Link ya video hio;

#Kuna baadhi hamtaridhishwa na nlichoandika (mtakua ni wapuuzi msiojua nini maana ya uzalendo).

#Povu ruksa,#Kunitukana ruksa.

Ila nimetimiza wajibu wangu kufikisha taarifa hii, ili kulinda vijana wenzangu kwa ushawishi na mifano mibaya wanayopata.
afu pia ukaitwa justify ni bangi au sigara au vape pen sababu amevuta lakini hamna anaejua kwakweli sababu video yenyewe iko na reasonable doubt

afu una wivu wakijinga sana unasema mitandaoni nakati kumejaaa vitu vya kila aina ukiondoa tu kwamba havijafanywa na watz ila mtoto,mtu mzima,mzee akiwa na access na internet anakutana navyo fundisha mwanao maadili mema uache kulia uzalendo nakati wewe unayakwako regardless hatuyajui ila nobody is right 100%
 
Kazi wanayoifanya tena mfululizo bila kupumzika lazima matumizi ya bangi etc yahusike
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom