Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Balozi Saleh Tambwe

Ngoja nikupe pole wewe mwenyewe kabla ya familia zao hao marehemu watatu,kwani naona mafungamano yako nao,Mungu baba awape pumziko jema.
 
Hakuna Youtuber au Podcaster humu ndani akafanya interview na mzee wetu huyu. Hii ni hazina.

Nina ombi langu Mzee Mohamed Said naomba unitajie siku ambayo upo na muda wa kutosha nikufanyie interview hapa hapa JF pamoja na member wengine wa JF
 
Ina Lillah Waina Illah Rajioun
Pole kwa wote Sheikh
Naijua familia hii vizuri na Baba yake Marehemu Rajabu Tambwe na ndugu yake Omari Tambwe (late) Mungu awahifadhi pema
Nilipoona jina nikajua ni jamaa wa nyumbani
 
Hakuna Youtuber au Podcaster humu ndani akafanya interview na mzee wetu huyu. Hii ni hazina.

Nina ombi langu Mzee Mohamed Said naomba unitajie siku ambayo upo na muda wa kutosha nikufanyie interview hapa hapa JF pamoja na member wengine wa JF
Cvez,
Mimi napatikana muda wowote kaka.
Karibu sana.
 
SALEH RAJAB TAMBWE, JOB LUSINDE NA SAMWEL SITTA

Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Balozi Saleh Tambwe ambae tukifahamiana kwa miaka mingi na yeye akimjua babu yangu katika kundi la wazee wa Kimanyema waliopigania uhuru wa Tanganyka kutokea Tabora, Western Province.

Katika kundi hili alikuwapo Rajab Tambwe, Abdallah na Maulidi Kivuruga, Bilali Rehani Wiakela, Issa Kibira kwa kuwataja wachache.

Kiasi cha kama miaka mitatu hivi nilikutana na Balozi Tambwe Makaburi ya Kisutu akiwa ameongozana na Balozi Job Lusinde na Spika Samwel Sitta.

Balozi Tambwe akanitambulisha kwao na tukawa na mazungumzo ya hapa na pale.

Nakumbuka nilimwambia Mh. Samwel Sitta kuwa mimi namfahamu toka utoto wangu Tabora nilipokuwa nikienda likizo kwa babu yangu Baba Popo.

Jina hili ni maarufu tukawa tumefahamiana.

Lakini nikamtajia kitu ambacho naamini hakukitegemea kutoka kwangu nilipomwambia kuwa akiwa mwanafunzi alipata kushinda mashindano ya kuandika insha ya Kiingereza na zawadi yake ilikuwa safari ya Marekani.

Alifurahi sana kwa mimi kumtambua hivyo.

Balozi Job Lusinde nilimwambia kuwa nimemtaja katika kitabu cha Abdul Sykes wakati akiwa mwalimu Alliance Secondary School, Dodoma, Central Province.

Kulikuwa na mgogoro wa kuunda tawi la TANU pale mjini na viongozi wa harakati hizi alikua Omari Suleiman aliyekuwa fundi cherahani na Haruna Taratibu Fundi Mwashi, Public Works Department (PWD).

Job Lusinde na wasomi wengine wa Makerere waliokuwa walimu pale Alliance walijiweka mbali na harakati hizi kwa kuhofia kupoteza kazi zao.

Lakini mimi sikumpeleka huko nilitosheka na kumfahamisha kuwa nimemtaja katika kitabu changu.

Job Lusinde alinijia kama mtu mkimya na mpole jinsi alivyokuwa anazungumza na mimi.

Nilikuwa na nakala ya kitabu hicho katika mkoba wangu nikaufungua nikamkabidhi.

Alinishukuru na nikawaomba niwapige picha ya pamoja wakanikubalia nikawapiga na tukaagana.

Job Lusinde alinijia kama mtu mkimya na mpole jinsi alivyokuwa anazungumza na mimi.

Haukupita muda mrefu Spika Samuel Sitta akafariki, kisha Balozi Job Lusinde na leo Balozi Saleh Rajab Tambwe ametangulia kwa Mola wake.

Tunamuomba Allah amfanyie wepesi Balozi Tambwe katika safari yake hii.

Amin.​

View attachment 1686043

Angalia picha: SALEH RAJAB TAMBWE, JOB LUSINDE NA SAMWEL SITTA

View attachment 1686046
Habari mzee,huyu Saleh tambwe ndio yule balozi aliye kosa nafasi kwenye ndege iliyokua inatoka dar es salaam kwenda Rwanda mwaka 1994 ambayo ilipata ajali na kuua Marais wawili wa Rwanda na Burundi?

Kuna sehemu nilikua nasoma historian nimekutana na hili jina la Saleh tambwe.
 
Yanga,
Ndiye yeye.
 
Back
Top Bottom