Nimesikitishwa na kifo cha faru Sudan, dunia ijufunze

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
Tamaa za mwanadamu zinaaharibu Nature nzuri ya dunia.
Ujangili, Ujangili,Ewe Jangili ona sasa umesababisha vizazi vyako kutoweza kumuona Faru Mweupe tena katika Uso wa Dunia.
Kwakweli nimesikitika mnoo.

Sudan: Faru dume wa kipekee aliyekuwa amesalia duniani afa
Screenshot_2018-03-21-10-18-00.jpg
Screenshot_2018-03-21-10-17-30.jpg
 
Mimi hua sielewi hili linakuaje,,,hivi inawezekana vp mpaka faru mweupe abaki huyo tu ? Serikali hazikuona kua faru wanapungua zifanye kuwafuga sehemu salama ?
Hata mimi naona wahusika walishindwa kuchukua hatua mapema. Sasa hivi wanajipanga jinsi ya kufanya in vitro fertilization. Seriously? mpaka dume pekee aliyebaki anakufa!
 
MAJANGILI WATU WABAYA SANA

kwanini
mbona umri ulifika miaka 45
Mwenyezi naye hupanga
acheni akapumzike mlitaka alete faida gani ingine zaidi ya kumshangaa tuu
Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake.
Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.
Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
"Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana," Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.
 
Afe tu, mbona hata sisi majangiri wa selikali wanatuua kwa risasi mapanga na marungu vizazi vyetu vinatoweka kwa hila za watawala wenye uchu wa Madaraka.
 
Huyu faru pamoja na off springs wake wawili mtoto na mjukuu walikuwa wanatunzwa na private conservancy ol pajeta iko Laikipia Kenya. Aliporudishwa Kenya pamoja na jike mmoja walijaribu sana kuwafanya wa mate ikashindikana. Huyo jike alikufa nadhani around 2009 sina uhakika sana lakini. Hawa majike wawili waliobaki wana matatizo mengi kiafya na wanajua kabisa kuwapandikiza mimba haitawezekana. Story ya hawa faru iliisha kitambooo juhudi zilitakiwa kufanyika kabla ya jike yule kufa.
Serikali zetu ni wazembe sana aisee,,
 
Dunia na mazingira yake ya sasa sio rafiki tena kwa FARU. Watu watalaumiana sana lakini ukweli ni kwamba uzao wa faru unakaribia kuwa historia kama ilivyokuwa wale mijusi wakubwa walioishi miaka mingi liyopita na wakapotea.
Hiyo ni NATURE hatuwezi kushindana nayo.
 
Mimi hua sielewi hili linakuaje,,,hivi inawezekana vp mpaka faru mweupe abaki huyo tu ? Serikali hazikuona kua faru wanapungua zifanye kuwafuga sehemu salama ?
Sure kiongozi huyo faru alitakiwa atolewe mbugani awekwe sehemu salama tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom