Nimesikitika sana kuona CHADEMA wanalishambulia Bunge kwa kuisimamia Serikali

Nilipowaona CHADEMA hawana maana baadabya Mbowe kukamatwa na swala la Katiba mpya likaishia pale pale.

Kumbe walitakiwa waji organise wafanye matukio kila Mkoa kila siku Ku support alichokuwa anapigania Mbowe kama chama,ungeona hiyo SAMIA kama angeshindwa kumwachia Mbowe.

Hivyo hivyo katika hili swala la Ndugai walitakiwa watumie mwanya huu kutengeneza moto,yenyewe yamekaa kama Pipa stupid Chadema.
Yani hiki chama hawajielewi hata, kimejaa ushabiki kuanzia wanachama mpaka viongozi. Hakuna lolote la maana wamewahi kulisimamia mpaka mwisho.

Hivi unawapaje nchi hawa watu wasiojielewa.
 
Chadema wakisubiri njia za kisitaarabu kwa kufanya siasa za kistaarabu eti ndio washike dola watasubiri miaka 1000.

Ni kweli Wananchi wamelala na ni waoga lakini nani wa kuwatoa katika usingizi huo??? ,wanatakiwa wa force vitu litakalo tokea litokeee uone kama kesho tu hawataingia Ikulu.

Sasa wamebaki Kumuomba mtesi wao SAMIA amwachie Mbowe,weka mikakakti ingia mtaani Fanya matukio mpaka SAMIA amwachie Mbowe kwa kutokupenda.
 
Ndugai ni spika wa bunge na amemkosoa rais ambaye ni kiongozi wa serikali.

Chadema mmeona kafanya kitendo kibaya mmemtukana matusi ya nguoni.
Ndugai hajaikosoa serikali
Amemuropokea Samia
Utaratibu wa vikao vya bunge na namna yakupeleka hoja bungeni inafahamika.

Huku nje hajaongea kama Spika, ameongea kama mchapa bakora mhuni.

Hoja yake ina msingi Ila imekaa kinafiki, hata kwenye hansard za bunge haijaingia.
 
Siku zote kilio chetu ni kuona Bunge linaisimamia vyema Serikali.

Lakini inasikitisha sana chama cha upinzani kinapotoa baraka Serikali isiweze kuhojiwa na bunge.

CHADEMA kimedhihirisha ni chama cha ujanja ujanja kisichosimamia misingi ya demokrasia.

Kitendo cha viongozi na mashabiki wa CHADEMA kumtukana na kumshambulia Spika wa Bunge kwa kuwa kahoji mamlaka ya Rais juu ya mambo muhimu ya nchi kinasikitisha sana na kinaonyesha bado tuna safari ndefu ya kupata chama makini cha upinzani.

Ndio maana wananchi wamekata tamaa na wamevipotezea vyama vya upinzani kwa sababu ni vyama vya kusaka vyeo na fursa.

Msigwa, Lema, John Mrema wamekivua nguo chama cha CHADEMA.
Wewe kumbe ni Zuzu ee? Ndugai anaweza kuisimamia serikali akiwa nje ya bunge? Yaani Ndugai kakusanya ndugu zake hicho Kikao ndo kitumike kuisimamia serikali?
 
Siku zote kilio chetu ni kuona Bunge linaisimamia vyema Serikali.

Lakini inasikitisha sana chama cha upinzani kinapotoa baraka Serikali isiweze kuhojiwa na bunge.

CHADEMA kimedhihirisha ni chama cha ujanja ujanja kisichosimamia misingi ya demokrasia.

Kitendo cha viongozi na mashabiki wa CHADEMA kumtukana na kumshambulia Spika wa Bunge kwa kuwa kahoji mamlaka ya Rais juu ya mambo muhimu ya nchi kinasikitisha sana na kinaonyesha bado tuna safari ndefu ya kupata chama makini cha upinzani.

Ndio maana wananchi wamekata tamaa na wamevipotezea vyama vya upinzani kwa sababu ni vyama vya kusaka vyeo na fursa.

Msigwa, Lema, John Mrema wamekivua nguo chama cha CHADEMA.
Tofautisha maoni ya speaker wa bunge na maazimio ya bunge. Speaker kaongea hayo at individual capacity . Maana kwa kanuni za bunge maamuzi yanafanyika kwenye Chambers. Kwa mfano, Speaker wa bunge Job Ndugai aliposema atamlazimisha Magufuli aongeze muda wa urais apende asipende lilikuwa bunge au maoni ya speaker. Bunge linatakiwa liwe na mamlaka ya kupitisha kiwango Cha kukopa nje na sio kulalamika na kurusha madongo Kama anavyofanya Speaker Ndugai.
 
Ndugai ni spika wa bunge na amemkosoa rais ambaye ni kiongozi wa serikali.

Chadema mmeona kafanya kitendo kibaya mmemtukana matusi ya nguoni.
Wamemtukanaje tena hayo ya nguoni, happy hebu tumegee japo mawili waliotukana.. tuone!
 
Chadema mmewaangusha sana wananchi wapenda demokrasia....mnatukana bunge kuisimamia serikali!!๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
Nia yako sio demokrasia Wala Nini Bali lengo lako ni kutaka kuingiza CHADEMA kwenye maujinga ya CCM . Pesa mnakopa Kila siku na tozo mnachukua, muda ukifika mnaanza kuumbuana wenyewe kuwa nchi itapigwa mnada. Endeleeni kuangaika na mizigo yenu achaneni na CHADEMA.
 
Siku zote kilio chetu ni kuona Bunge linaisimamia vyema Serikali.

Lakini inasikitisha sana chama cha upinzani kinapotoa baraka Serikali isiweze kuhojiwa na bunge.

CHADEMA kimedhihirisha ni chama cha ujanja ujanja kisichosimamia misingi ya demokrasia.

Kitendo cha viongozi na mashabiki wa CHADEMA kumtukana na kumshambulia Spika wa Bunge kwa kuwa kahoji mamlaka ya Rais juu ya mambo muhimu ya nchi kinasikitisha sana na kinaonyesha bado tuna safari ndefu ya kupata chama makini cha upinzani.

Ndio maana wananchi wamekata tamaa na wamevipotezea vyama vya upinzani kwa sababu ni vyama vya kusaka vyeo na fursa.

Msigwa, Lema, John Mrema wamekivua nguo chama cha CHADEMA.
Ni lini CHADEMA imetoa official statement ya kwamba inapinga maoni ya Ndugai?. Jifunze kutofautisha kauli ya chama na kauli ya mwanachama.
 
Chadema kimejionesha ni chama cha matukio na kipo kinaangalia upepo wa kula ruzuku.
Wewe nimekusoma mrengo wako. Umetoka kwenye kulitukana bunge mpaka kwenye ruzuku. Naona moyo wako hauna amani kabisa, baada ya yote mliyoifanyia CHADEMA bado ipo hai, Sasa umebakia kuokoteza vimaneno visivyo na maana na kuisingizia CHADEMA. Hautapata amani mpaka utubu.
 
Ndugai hajaikosoa serikali
Amemuropokea Samia
Utaratibu wa vikao vya binge na namna yakupeleka hoja bungeni inafahamika.
Huku nje hajaongea kama Spika,ameongea kama mchapa bakora mhuni.
Hoja yake ina msingi Ila imekaa kinafiki,hats kwenye hansard za bunge haijaingia.
Kwa hiyo Spika akiikosoa serikali Chadema mnaita ni uhuni?
 
Ndugai hajaikosoa serikali
Amemuropokea Samia
Utaratibu wa vikao vya binge na namna yakupeleka hoja bungeni inafahamika.
Huku nje hajaongea kama Spika,ameongea kama mchapa bakora mhuni.
Hoja yake ina msingi Ila imekaa kinafiki,hats kwenye hansard za bunge haijaingia.
Kwa hiyo Spika akiikosoa serikali Chadema mnaita ni uhuni?
 
Siku zote kilio chetu ni kuona Bunge linaisimamia vyema Serikali.

Lakini inasikitisha sana chama cha upinzani kinapotoa baraka Serikali isiweze kuhojiwa na bunge.

CHADEMA kimedhihirisha ni chama cha ujanja ujanja kisichosimamia misingi ya demokrasia.

Kitendo cha viongozi na mashabiki wa CHADEMA kumtukana na kumshambulia Spika wa Bunge kwa kuwa kahoji mamlaka ya Rais juu ya mambo muhimu ya nchi kinasikitisha sana na kinaonyesha bado tuna safari ndefu ya kupata chama makini cha upinzani.

Ndio maana wananchi wamekata tamaa na wamevipotezea vyama vya upinzani kwa sababu ni vyama vya kusaka vyeo na fursa.

Msigwa, Lema, John Mrema wamekivua nguo chama cha CHADEMA.
Hivi tuna bunge kweli? Au vikao vya wanafiki wanaoitumia ukumbi wa bunge?
 
Back
Top Bottom