Nimesikiliza Shule ya Uongozi ya Polepole, nimejua Polepole hapaswi tena kupewa nafasi yoyote kubwa ya kiuongozi

Mkuu, kwani ulimsikiliza Pole Pole kwenye mada hipi siku za karibuni iliyo kufanya uanze kuwa na wasi wasi kuhusu analytical mind yake - labda tuanzie hapo.
Ana kipindi chake kinaitwa shule ya uongozi kinarushwa Youtube na Facebook kila Jumamosi usiku..nimeviangalia mara kadhaa, ila cha jana nikaona upotoshaji umezidi, nikamfungulia huu uzi
 
acha unaa wewe. Polepole anatumia kipawa chake alichopewa na Mungu kushare knowldge aliyojaaliwa
Knowledge aliyojaaliwa?!!! Kumbe amejaliwa knowledge yule mtu?? Ndo ile anayoitoa pale?!!! Ngoja nicheke mimi.....hahahahaaaaaa!

Ukweli ni kuwa amechanganyikiwa, hajui ashike wapi na afuate lipi! Anajitia kuchukia wazungu wakati ni hao waliomtengenezea v8. alifikiri pengine pindi litampa umaarufu badala yake ndo kwanza linapotea hapa mwanzoni tu........anachoongea kwa sasa kinaeleweka na wapumbavu wachache tu; lengo lake kuu la kumchonganisha mama na wananchi halionekani kushamiri kabisa
 
Literacy rate ni kipimo cha social development. Ndiyo maana hata Mwalimu Nyerere aliweka kisomo cha Elimu ya Watu Wazima ili kufuta ujjnga. Tanzania chini ya Mwalimu ilifuta ujinga kwa sehemu kubwa. Jamii isiyo na wajinga inaweza kumaster environment.
 
Nina wasi kama ana hata diploma... nakumbuka kalituacha na njaa kwenye semina iliyoandaliwa na taasisi yake kwa kufadhiliwa na wizara ya fedhap pale ukumbi wa manispaa ya Temeke miaka ya nyuma kidogo kabla hajajulikana Sana. Tetesi zilisema Pole pole alikamba fedha za chakula na vinywaji. Baadae nikasikia ameteuliwa tume ya katiba!
Hivi inaigia akilini kwamba Serikali pamoja na vyombo vyake vya Dola vyenye uwezo mkubwa waku- vent watu vinaweza kweli kupendekeza kilaza awepo kwenye team ya tume ya katiba? Naona chuki zenu zimepitiliza mipaka - msikilizeni Pole Pole anapo zungumza kiingereza anaonekana wazi wazi ni MTU mwenye taaluma ya sheria, wanao sema ni mbumbumbu hawajui walisemalo - siyo fresh kuwazulia binadamu wenzenu kwa lengo la kuwaribia kisiasa.
 
Polepole hana elimu yeyote juu ya ujamaa wala ubepari ni mtu anaekoteza okoteza angalau na yeye aonekane yumo.na hapa analenga kundi kubwa la watanzania wajinga awafanye mtaji wa kisiasa. Polepole ninaemjua ni yule wa propaganda za CCM hana ufahamu wowote wa anayoyafundisha kwakifupi siyo level yake. Aache kupotosha umma hayo awaachie walimu vyuoni na kwenye taasisi za elimu asipotoshe.
 
Ndugu Polepole katika vipindi vyake vya Shule ya Uongozi anazungumzia mambo mengi lakini theme kuu ni kupinga mataifa ya magaharibi

Katika moja ya mafundisho yake Polepole anasema tusitumie vigezo vya nchi za Magharibi kupima maendeleo ya nchi yetu

Akitolea mfano suala la watu kujua kusoma na kuandika (literacy rate) katika nchi fulani halipaswi kuchukuliwa kama moja ya kipimo cha maendeleo

Akasema pia kuna takwimu kama vile kasi ya ukuaji uchumi (GDP growth rate) na takwimu za magonjwa na vifo vyote hivi ni vipimo vya kimagharibi vya kupima maendeleo na hatutakikiwi kuvitumia

Akaendelea kutoa mfano mfugaji Mmasai mwenye ng'ombe 1000 Tz lakini kwa vigezo vya kimagharibi huyu mmasai ni masikini lakini tunapaswa kumuita ni tajiri kwani mtu mwenye ng'ombe 1000 Ulaya anaitwa tajiri

Polepole anataka tutumie vigezo vya nchi kama China au Singapore kupima maendeleo

Sasa nilichojiuliza ni China na Singapore zinapoitwa ni nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kwani ni vigezo vipi hutumiwa?

Si ndio hivi hivi vya kimagharibi? Zinaitwa zimeendelea kwa sababu wananchi wake wana makazi bora, huduma nzuri za afya, usafiri, nishati ya uhakika , high litetacy rate n.k

Wamasai wenye ng'ombe 1000 ila wanakunywa maji machafu na mifugo, kuhama hama na kulala kwenye nyumba zinayovuja zisizokuwa na umeme, hawa kwa vigezo vya China au Singapore ni wananchi walioendelea?

Halafu Polepole anasema tukae mbali na nchi za magharibi kwani hawana nia nzuri na nchi yetu na kutaka tuwe karibu na China, lakini China hii ndio waliituhumu kutaka kuingiza nchi mkenge kwenye bandari ya Bagamoyo

China ndio imekopesha nchi za Africa kama Kenya mikopo mikubwa ya kimtego isiyolipika kwa lengo baya

China ndio hii tunasikia wametifisha bandari baadhi ya nchi zilizoshindwa kulipa mikopo yao...

Polepole sababu anachukia nchi za magharibi imemtia upofu hadi kushindwa kuona vitu vya logic ndogo tu, huyu mtu na walio nyuma yake ni hatari na hawapaswi tena kupewa nafasi ya kuongoza nchi yetu, wataturudisha Tanzania ya miaka ya 1980s....
Mimi nilimuona punguwani siku nyingi tu tangu alipokuwa akitambia Vee-eite za ccm.

Mpumbavu kabisa huyo mzee kijana.
 
Hivi inaigia akilini kwamba Serikali pamoja na vyombo vyake vya Dola vyenye uwezo mkubwa waku- vent watu vinaweza kweli kupendekeza kilaza awepo kwenye team ya tume ya katiba? Naona chuki zenu zimepitiliza mipaka - msikilizeni Pole Pole anapo zungumza kiingereza anaonekana wazi wazi ni MTU mwenye taaluma ya sheria, wanao sema ni mbumbumbu hawajui walisemalo - siyo fresh kuwazulia binadamu wenzenu kwa lengo la kuwaribia kisiasa.
Nyanda... vetting za serikali zinategemea connection.
 
Hivi inaigia akilini kwamba Serikali pamoja na vyombo vyake vya Dola vyenye uwezo mkubwa waku- vent watu vinaweza kweli kupendekeza kilaza awepo kwenye team ya tume ya katiba? Naona chuki zenu zimepitiliza mipaka - msikilizeni Pole Pole anapo zungumza kiingereza anaonekana wazi wazi ni MTU mwenye taaluma ya sheria, wanao sema ni mbumbumbu hawajui walisemalo - siyo fresh kuwazulia binadamu wenzenu kwa lengo la kuwaribia kisiasa.
Kwenye tume ya katiba watu waliingia kwa professional zao baba.pale kulikua na walemavu ,wasanii , hata ambao hawajasoma.kwahiyo polepole kuingia kwenye tume ya katiba isikufanye uamini kuwa aliingia kwa tiketi ya usomi noo. Tunachopinga hapa ni huyu polepole kutoa lecture kwa mambo ambayo hayajui na hana elimu ya anayoyafundisha .
 
Hivi inaigia akilini kwamba Serikali pamoja na vyombo vyake vya Dola vyenye uwezo mkubwa waku- vent watu vinaweza kweli kupendekeza kilaza awepo kwenye team ya tume ya katiba? Naona chuki zenu zimepitiliza mipaka - msikilizeni Pole Pole anapo zungumza kiingereza anaonekana wazi wazi ni MTU mwenye taaluma ya sheria, wanao sema ni mbumbumbu hawajui walisemalo - siyo fresh kuwazulia binadamu wenzenu kwa lengo la kuwaribia kisiasa.
Polepole yule wa tume ya Warioba na Polepole Chakubanga wakikutana lazima wapigane ngumi za kutosha.

Kwani unadhani Lipumba siyo Profesa?
 
Alitaga Yai form six mkuu
Duu so akawa wa kujipendekeza na kiherehere mpaka akateuliwa.
Nakumbuka alikuja mradi mmoja ivi wa road nikamcheki nikaachana naye.yaani alipewa rungu la kuwakoromoea wakubwa saivi kiukweli anatafuta popularity ili akagombee Mana amepaona huko patamu Sana sio Kama alikotolewaga.
 
Kaunga unga elimu yake ya hapa na pale had kagraduate UD siunajua ukiwa na cheo ma lecturer full kujipendekeza.
Bora tu angetulia maana anayosema Sasa hivi na kipindi akiwa na cheo inaonyesha Kuna unafiki mkubwa, mbona kina kabudi, bashiru wako kimya, anajitaftia matatizo tu bure
 
FYI, Pole Pole is mega smart upstairs, level headed not 4getting that is unquestionably light years ahead of wannabe politician clown ambao wako hell bent kumwaribia sifa.
Polepole unaemsemea yule wa Bunge la Katiba au polepole Katibu mwenezi ... swala la muda tu atabaki katika Historia, atumie tu muda huu vzr, soon atakumbuka zile story za unaijua V8..
 
Kaunga unga elimu yake ya hapa na pale had kagraduate UD siunajua ukiwa na cheo ma lecturer full kujipendekeza.
Bora tu angetulia maana anayosema Sasa hivi na kipindi akiwa na cheo inaonyesha Kuna unafiki mkubwa, mbona kina kabudi, bashiru wako kimya, anajitaftia matatizo tu bure
Sure Kama kabudi Tena anaongea na yule wa uchina kuwa chato anatamani ifanane na majiji mojawapo ya uchina like fujian
 
Back
Top Bottom