chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,961
Ndugu Polepole katika vipindi vyake vya Shule ya Uongozi anazungumzia mambo mengi lakini theme kuu ni kupinga mataifa ya magaharibi.
Katika moja ya mafundisho yake Polepole anasema tusitumie vigezo vya nchi za Magharibi kupima maendeleo ya nchi yetu.
Akitolea mfano suala la watu kujua kusoma na kuandika (literacy rate) katika nchi fulani halipaswi kuchukuliwa kama moja ya kipimo cha maendeleo.
Akasema pia kuna takwimu kama vile kasi ya ukuaji uchumi (GDP growth rate) na takwimu za magonjwa na vifo vyote hivi ni vipimo vya kimagharibi vya kupima maendeleo na hatutakikiwi kuvitumia.
Akaendelea kutoa mfano mfugaji Mmasai mwenye ng'ombe 1000 Tz lakini kwa vigezo vya kimagharibi huyu mmasai ni masikini lakini tunapaswa kumuita ni tajiri kwani mtu mwenye ng'ombe 1000 Ulaya anaitwa tajiri.
Polepole anataka tutumie vigezo vya nchi kama China au Singapore kupima maendeleo.
Sasa nilichojiuliza ni China na Singapore zinapoitwa ni nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kwani ni vigezo vipi hutumiwa?
Si ndio hivi hivi vya kimagharibi? Zinaitwa zimeendelea kwa sababu wananchi wake wana makazi bora, huduma nzuri za afya, usafiri, nishati ya uhakika , high litetacy rate n.k.
Wamasai wenye ng'ombe 1000 ila wanakunywa maji machafu na mifugo, kuhama hama na kulala kwenye nyumba zinayovuja zisizokuwa na umeme, hawa kwa vigezo vya China au Singapore ni wananchi walioendelea?
Halafu Polepole anasema tukae mbali na nchi za magharibi kwani hawana nia nzuri na nchi yetu na kutaka tuwe karibu na China, lakini China hii ndio waliituhumu kutaka kuingiza nchi mkenge kwenye bandari ya Bagamoyo.
China ndio imekopesha nchi za Africa kama Kenya mikopo mikubwa ya kimtego isiyolipika kwa lengo baya.
China ndio hii tunasikia wametifisha bandari baadhi ya nchi zilizoshindwa kulipa mikopo yao.
Polepole sababu anachukia nchi za magharibi imemtia upofu hadi kushindwa kuona vitu vya logic ndogo tu, huyu mtu na walio nyuma yake ni hatari na hawapaswi tena kupewa nafasi ya kuongoza nchi yetu, wataturudisha Tanzania mbovu kuliko ile ya miaka ya 1980s.