Nimeshuhudia vibarua kama 1000 hivi wakichakarika kama Nyumbu (Ubungo Flyover), hii haraka ya ujenzi ya ghafla inatokana na nini?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,002
40,670
Katika siku za karibuni nimeanza kuona utitiri wa vibarua wakipigika vilivyo kama siafu pale site ya ujenzi wa barabara za juu Ubungo (Ubungo Flyover), ongezeko hili la kasi limetokea ghafla sana.

Je, kuna deadline wanaiwahi au ni nini?
 
FRANCIS DA DON,

HIYO NDIO FAIDA YA KUWA NA MFUMO WA VYAMA VINGI. CHAMA KILICHOKO MADARAKANI WAKATI WOTE KITAFANYA KILA LILILO NDANI YA UWEZO WAKE KURIDHISHA WANANCHI ILI WAENDELEE KUKIPIGIA KURA WAKATI VYAMA VYA UPINZANI MUDA WOTE WANATAZAMA KILE KINACHOFANYWA NA SERIKALI YA CHAMA TAWALA (WATCH DOG) KWA LENGO LA KUAINISHA MAPUNGUFU KWA WANANCHI ILI WAACHE KUUNGA MKONO CHAMA TAWALA NA BADALA YAKE WAUNGE MKONO CHAMA PINZANI.

HIVYO MTU YOYOTE ANAYETAMANI VYAMA VYA UPINZANI VIFUTIKE KABISA HAJUI ANALOTAMANI KWANI MAENDELEO YETU YATAKUJA KWA HARAKA SANA KUKIWEPO CHAMA TAWALA IMARA NA UPINZANI ULIO IMARA
 
Hata akamilishe Leo jioni bado haitamsaidia, sisi wanaccm tumeamua kwenda na Bernard membe
 
Lini paliwahi kuwa kimya pale tangu pameanza kujengwa?

Binadamu!!!!?
 
Katika siku za karibuni nimeanza kuona utitiri wa vibarua wakipigika vilivyo kama siafu pale site ya ujenzi wa barabara za juu Ubungo (Ubungo flyover), ongezeko hili la kasi limetokea ghafla sana, je, kuna deadline wanaiwahi au ni nini?
Hayo ndio maagizo ya kidikteta yanavyoharibu mambo mbalimbali nchi hii. Nguvu na vitisho havifanyi mambo kuwa mazuri, kuna mtu anahitaji kujifunza jambo hili kabla mambo hayajaanza kumwendea vibaya.
 
Back
Top Bottom