kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,888
Covid-19 imeanza kula watu kwa umati.
Leo asubuhi nilielekea pande hizo kujinunulia mahitaji si unajua mfungo huu? Na ikizingatiwa nimekimbia Corona week sasa nipo huku ila soon narudi maana ndugu zangu ndo tufanyeje sasa Dar ndo maisha na family ipo huko.
Leo nimeshuhudia kwa macho yangu mawili Soko moja Moshi, Masama jamaa mmoja ambaye ni dereva wa malori yanayobeba ndizi akizidiwa na dalili zote za Corona na kuanguka pale sokoni ndo ikabidi namba ya dharura ipigwe na likaja gari na wale jamaa na jezi zao wakaja kumbeba na kumkimbiza Mawenzi.
Hali ni mbaya Tanzania kweli nimeamini Taifa linaenda kuangamia kabisa.
Halafu kuna tetesi kwamba Mawenzi imejaa wagonjwa kiukweli hali ni mbaya.
Kwa wale mliokimbia Corona Dar mkaja Moshi nawasihi bebeni tahadhari, Corona ishawasili huku tayari mpaka migombani kule. Mungu atunuru "Ya allah tunusuru sisi waja wako"
Nitaendelea kuilaumu Serikali tu kwa asilimia 100%. Taifa linaenda kuangamia kwa sababu ya sera za mtu mmoja tu mbinafsi
Napata uchungu sana nawafikiria kina mama,na kina bibi ambao wanaishi kwa kutegemea biashara masokoni hali yao itakuaje na wanawake wajane wanaoishi kwa kuuza nyanya na vitunguu masokoni kulisha watoto wao kimahitaji itakuaje?
Taifa linakwenda kuangamia ndugu zangu nikiwaza Tanzania kwa mwendo huu naiona Italy ya pili inauma sana
Endeleeni kuficha tu serikali ya ajabu hii
Sent using Jamii Forums mobile app