Nimeshtushwa Polisi kutishia uhai wa watoto kwa silaha za kivita

Yaani hata km Baba akiwa FFU asipande gari la POLISI mbona mtoto hana kosa pale ila ni Mwl wake? Nchi ina Amani huku kwetu kuna Kambi ya FFU Nzuguni ndio magari wanayoyatumia msiyaogope kwani hata na wao ni WaTZ kwani Nchi ikienda vibaya hata wao inawahusu ni km wale wa Cairo Misri. Huwezi mdanganya askari kuhusu Nchi hii wao wakianzisha mgomo kila mtu atajificha ndani, tuwaache wafanye kazi zao, wanazuia mawe na uporaji kwa kisingizio cha maandamano na migomo
 
Kitumbua kishaingia mchanga,Police kikubwa kiwatesacho ni njaa na kujipendekeza'na wengi ni QT,Sasa safari hii wao na serikali yao lazima waisome namba. Walimu hatutishiwi nyau'tutalala home mpaka baba Rizi anyoshe maelezo
 
Hao wanazi wa intelejensia fake lazima watakuwa waliwakamata ili wawatishe waseme nani kawatuma, akili zao zooote ni CHADEMA!
 
Hawa askari kweli wamediriki kufanya hayo kwa watoto ? Madhara yake wanayajua in a long run ?

mkuu hawa jamaa hata kama asilimia yao kubwa ni form 4 zero au wakufoji vyeti lakini nadhani hata uwezo wao wa kufikiri mambo ya kawaida ni mdogo sana, hivi hao watoto wanahatarisha nini hasa... nani aliyesababisha wao wakose masomo??? nani alisababisha walimu wagome.. wao ni third part na ni haki yao kufundishwa... sasa serikali inapesa ya kutoa maposho na mamishahara mpaka 11 milioni kwa wazinziaji, na walevi wa bunge, na kupiga rushwa za mabilioni wanashindwa kuwajali watu wake?? halafu hivi kweli sisi tunaendelea kweli.. miaka 50 ya uhuru ni migomo kila kona, kila kitu tumeuza, anzia utu wa kibinaadamu,elimu, madini, viwanda, reli.. mpaka ardhi yetu..... kwa kweli... tuatafika tukiwa tumechoka na kufa woote. Hii serikali yenyewe inaweza kukimbilia mahakamani tu mengine ni zero tu.... Mungu awalaani hawa watawala..
 
Candid Scope, tatizo kubwa tulilo nalo sisi Wabongo ni kufikiri kuwa tuna serikali. Hiki tulicho nacho ni genge la mafisadi (kleptocractic regime). Kwa hivyo, kusema huwezi "kuelewa serikalini kuna matatizo gani" ni bahati mbaya kufikiri hivyo -Bongo hakuna serikali!

Nakubaliana nawe, mambo yote haya kama kungekuwa na viongozi makini serikalini yasingejirudiarudia kamwe.
 
Hawa askari kweli wamediriki kufanya hayo kwa watoto ? Madhara yake wanayajua in a long run ?

Absolutely! Tukio hili limenifikirisha mno najisikia mawazo yangu yamefika mbali isivyokawaida. Huruma kwa watoto wale wanavyonyanyaswa na polisi kama wavunja sheria wakati tamani yao ya kupata elimu ndiyo inayowapekeka kutishiwa na mitutu ya bunduki.
 
Ile picha ya mtoto akipanda karandinga pasipo uoga inaongea mengi sana. I hope watawala wanasoma kinachoendelea - wasipuuzie na kudharau

Maneno ya busara sana lakini watawala wetu ni kama Wakoloni,wanatawala kama vile siyo wazawa wa nchi hii.
 
Mbona sijaona hizo silaha za kivita ?

1.jpg


Hizo ni pistol ya polisi kulinda amani au ni sub-machine-gun zitumikazo vitani? Tembea nchi za walioendelea na kujua maana ya kulinda usalama wa raia polisi wana silaha ndogo ndogo sana za kujikinga wenyewe tu, si za kupiga masafa kama wapo vitani zitumikazo
Tanzania.
 
Tumefika hapa pa kukosa hekima na hata kuwatisha watoto na mabunduki ni kwa sababu ya Udhaifu wa ccm na serikali yake na hii inatokana na ccm kutokukubalika kabisa na watanzania na ccm imebaki na kazi ya kutisha, kukimbilia mahakamani, kufungia magazeti na kukiri udhaifu wakwamba hatuna hela za kulipa ila tunazo hela za safari,posho, na za kwenda kucheki afya zetu India. CCM SASA NI KUHARIBU 2
 
Mnakumbuka Movie ya Sarafina? Haya yalikuwa yanatokea pale Soweto. Freedom is Coming Tomorrow
 
Ile picha ya mtoto akipanda karandinga pasipo uoga inaongea mengi sana. I hope watawala wanasoma kinachoendelea - wasipuuzie na kudharau

Kitu wasichojua serkali ni kuwa mwaka 2010 walilazimisha wanafunzi wa vyuo wasipige kura. 2015 Hawa watapiga kura za kisasi maana hawakururahishwa na uonevu waliofanyiwa. Je mtoto anayepigwa bomu leo na kupandishwa karandinga lini atakuja ipenda serkali ya ccm na kuisadia polisi katika mpango wake wa polisi jamii. Mtoto huyu atakua na chuki na shauku ya kisasi. Siku akipata nafasi anafanya kweli. Inanikumbusha sinema ya Sarafina.
 
Kitu wasichojua serkali ni kuwa mwaka 2010 walilazimisha wanafunzi wa vyuo wasipige kura. 2015 Hawa watapiga kura za kisasi maana hawakururahishwa na uonevu waliofanyiwa. Je mtoto anayepigwa bomu leo na kupandishwa karandinga lini atakuja ipenda serkali ya ccm na kuisadia polisi katika mpango wake wa polisi jamii. Mtoto huyu atakua na chuki na shauku ya kisasi. Siku akipata nafasi anafanya kweli. Inanikumbusha sinema ya Sarafina.

Omulangi,ninaanza kukata tamaa na mageuzi kwasababu Watanzania ni wasahulifu sana.
 
there is something terribly wrong na bongo za hii MIPOLISI yetu......damn!
 
Hii ni aibu iliyoje!!! Eti Tanzania kisiwa cha amani. There is no peace without justice. Tuna viongozi mbumbu ambao hawana uwezo wa kunyambulisha mambo hata mikataba waliyoridhia kimataifa. They cannot articulate critical issues in the day to day government performance. Serikali inaruhusu je polisi kuwashikia watoto bunduki kama majambazi? Jamii tuko wapi kuwatetea watoto, wajukuu, vilembwe, wapwa n.k. Wanawake wote tuliozaa tumwage razi. After all wengi katika serikali ni wanaume wasioujua uchungu wa mwana. Wale wanawake wachache waliopo serikalini/bungeni wengi wao wanajitahidi kuwa kama wanaume ili wakubalike katika system (rotten) na waendelee kujinufaisha nafsi.
 
Nayakumbuka ya SOWETO pale serikali ya Makaburu walipowaangamiza watoto kama hawa.
 
Serikali dhaifu inaogopa mpaka watoto wa chekechea ati wanaweza ingia ikulu hao.
 
THE SADDEST PART NI PALE WAKUBWA WANAPOKUA WAPOFU WA MATENDO DHALIMU KAMA KUOKOTA VITOTO VYA PRIMARY NA KARANDINGA, WATOTO WA KIKE WAMENYANYASWA ZAIDI KIJINSIA NA NI LAANA isiyoepukika
 
Back
Top Bottom