Nimeshtushwa Polisi kutishia uhai wa watoto kwa silaha za kivita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeshtushwa Polisi kutishia uhai wa watoto kwa silaha za kivita

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Candid Scope, Aug 1, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG]


  Hii ni dalili kwamba Tanzania hatuna sheria ya kutetea haki za watoto. Maandamano ya hawa watoto au wanafunzi hayakuwa uvujaji wa amani au sheria, bali kuisaidia serikali kufungua zaidi na kuona madai ya walimu yafikiwe mwafaka ili wasiendelee kukosa vipindi madarasani sababu ya mgomo wa walimu.

  Askari polisi kutumia silaha za kivita kutishia uhai wa wanafunzi ni jambo hatari kabisa kwa malezi ya watoto hawa, la ajabu, na lisilo la kistaarbu kabisa, na kabisa kisaikolojia ni kuwaharibu hawa watoto. Athari za matukio ya polisi kutishia watoto kwa silaha kali za kivita ni kubwa katika maisha yao, na hapo ndipo busara inapokosekana kwa serikali na jeshi la polisi nchini ni kielelezo tosha.


  [​IMG]

  Tanzania hatuna wanasaikolojia wanaoweza kuwasaidia hawa watoto kuongea nao wakaelewa na pengine wakachukua mawazo ya watoto hawa na kuyafanyia kazi, na badala ya watoto hawa kuwatisha wanafunzi uhai wao ka mitutu ya bunguki na mabomu ya machozi, je walikuwa na silaha gani kama si mikono mitupu kudai haki yao ya kupata elimu jambo ambalo linaeleweka kwa kila mmoja? Wizara ya jamii na watoto kazi yao nini , na wanafanya nini kutetea hawa watoto?

  [​IMG]

  Hawa watoto ni haki yao kudai muda unaopotezwa na walimu wanapodai haki zao wakati wanakosa masomo madarasani. Binafsi sioni kosa la watoto kama maandamano yao yalikuwa ya amani, na kama waliziba njia ni bora kutumia njia za kisaikolojia kuwatuliza wanafunzi kuliko tishio la silaha za kivita.

  Serikali iko tayari kusikiliza kilio cha wanasiasa wabunge kuwaongezea mishahara na malupulupu, lakini wanaosota maisha yao yote kuandaa hili taifa la kesho wamewapiga danadana siku nyingi na leo wanapochukua hatua serikali inaamua kumalizia hasira kwa hawa malaika wasio na makosa, waadhiriwa na mgomo wa walimu.

  Je, serikali inapotumia jeshi la polisi kutishia watoto hawa ambao ni waadhirika wa kukosa masomo bila ridhaa yao kwa uzembe wa serikali yenyewe, je inajengwa taswira gani katika maisha, malezi na future ya watoto hawa?

  :nono:Hili ndilo tatizo la vyombo vya dola vinapotumika zaidi kisiasa.:nono:​
   
 2. DEMBA

  DEMBA JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 7,295
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  hiyo ndo tanzania kila kitu kinawezekana ndugu.
   
 3. d

  dagjrtz Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mmmh Jamani?!!!
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Candid Scope, something is very wrong somewhere! I wish leaders could know what it is before too late.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 881
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Ile picha ya mtoto akipanda karandinga pasipo uoga inaongea mengi sana. I hope watawala wanasoma kinachoendelea - wasipuuzie na kudharau
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Hata Ufalme wa Mfalme Jean Bedel Bokassa uliangushwa kwa kunyanyasa watoto wa shule.

  Endeleeni kuwafunza protest ni nini hawa watoto ili waujue kiuhalisi udhalimu wenu mapema kabisa.
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anguko la serikali
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuwatishia uhai watoto hawa kwa bunduki ni kitu ambacho hakiingii akilini mwangu, siwezi kuelewa seikalini kuna matatizo gani. Hakuna chombo cho chote cha serikali kijamii kukemea tukio hilo, maana yake imehalalishwa, I don't understand at all, can't be acceptable
   
 9. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dah...nakumbuka mimi wakati nipo darasa la saba hata ningeulizwa mgomo ni nini nisingeweza kujibu lakini leo hii hata mtoto wa darasa la kwanza anaujua mgomo na kale ka wimbo ka "tunaka haki yetu".
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mchelea mwana mwisho hulia, kama hatua stahiki zingechukuliwa toka awali na kutolimbikiza madai hayo, leo isingekuwa tatizo kugombana na walimu na kusababisha vitisho vya uhai wa wanafunzi kitu ambacho ni aibu sana tunayojitwika ukilinganisha na mataifa yanayojali haki za mtoto.
   
 11. k

  kofiliko Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo ni mazoea ya kufilikili kwamba kila maandano ni vurugu na kushindwa kutambua jinsi ya kukabili maandamano kulingana na nature yake wao wanachojua ni kila maandano ni vurugu.Kweli inasikisha sana kuona askali wetu wanakimbilia mitutu ya bunduki kwa watoto wadogo hapa ni mwanzo wa kuwafundisha ujasili wa kivita kabla ya umri wao na hii tutegemee watoto wasiojali maslai ya nchi hapo baadae.Tufikilie njia za kisakologia katika jambo linalo husu watoto wetu.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Nimepoteza imani na mambo mengi sana yanayoendelea. Yaashiria tumeamua kukosa umakini kwa makusudi kabisa. I don't understand....
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Huyu Kikwete sasa naona anakaribia kaburi ,Kifo ndicho kilichobaki nchi imesaini na imeridha mkataba wa kimataifa wa 1990 wa ulinzi wa watoto, sheria ya watoto ya mwaka 2010 Kikwete kasaini ataamrishaje Polisi na mitutu ya bunduki wawakamate watoto na kuwatia kwenye karandiga huu ni uozo uliopitiliza huyu kweli ni Raisi wa nchi ya mmaamuma you cant just swallow this nosense
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  I dont understand...ninashindwa kuelewa tunaelekea wapi. Tunataka kutengeneza Taifa la watu wakorofi korofi? Kwa faida ya nani?
   
 15. a

  andrews JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​wacha watoto wazoee mitutu siku wakiingia mtaani kijani na njano mna hali mbaya
   
 16. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Candid Scope, tatizo kubwa tulilo nalo sisi Wabongo ni kufikiri kuwa tuna serikali. Hiki tulicho nacho ni genge la mafisadi (kleptocractic regime). Kwa hivyo, kusema huwezi "kuelewa serikalini kuna matatizo gani" ni bahati mbaya kufikiri hivyo -Bongo hakuna serikali!
   
 17. m

  massai JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  unawajua hao watawala kweli?mambo mazito kama hayo hawayaoni.wanachukulia poa ,mabweg.e yale hayana jipya
   
 18. S

  Sessy Senior Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukiona mpaka watoto wa miaka saba wanaandamana na kubebwa na polisi kama majambazi ujue tumefika mwisho tunahitaji maombi sana....
   
 19. commited

  commited JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  So sad... Kila chenye mwanzo kina mwisho
   
 20. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha kwakweli. Mlolongo wa matukio ya kipuuzi huku kukiwa hakuna sauti zenye mwangwi wa kutosha kuyakemea imefanya mambo kama haya kuonekana ya kawaida. TUKO WAPI WATANZANIA? TUKO WAPI WAZAZI? Hali tusiwasimamie watoto hawa na madai yao hadi waonekane ni watukutu tu waliotumwa na si wenye kilio cha kweli
   
Loading...