Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,173
- 27,223
Habari za saa hizi wanaJF, poleni kwa majukumu. Kuna jambo moja ambalo kwa uhalisia wake limenifedhehesha sana. Mimi binafsi na wenzangu ni mhudhuriaji mkubwa wa mikutano ya kisiasa, hivyo nimehudhuria mikutano yote ya mgombea wetu wa CHADEMA hapa Dar es Salaam. Na nilikuwa nasikiliza vizuri sera ambazo mgombea wetu amekuwa akizinadi.
Lakini nimekuwa nikipinga sana kuchangishwa michango hadharani tena kwa utaratibu ambao haukuwa mzuri, lakini mwisho waliweza kutoa utaratibu wa mtu kuchangia kwa muda wake mwenyewe(jambo zuri). Sasa mimi pamoja na wenzangu tumeshindwa kuchangia hii michango, sababu ni kuwa tulikuwa tunatumia mtandao wa Vodacom (M-Pesa) katika kufanya miamala yetu ya kipesa kwenye simu.
Ila kama tunakumbuka vizuri kuna tatizo lilitokea na kupelekea viongozi wetu wa chama kutuambia tususie kutumia mtandao wa Vodacom na MPesa kwa ujumla na zaidi walituambia tuzitupe hizo line au kuzivunja kabisa.
Tulitii hayo maagizo na kuamua kuzivunja, hivyo tukahamia kwenye mtandao ambao ulikuwa unakuja kwa kasi sana mtandao wa Halotel na ambao pia internet yake ipo fasta sana na inapatikana katika mazingira yote hadi ya vijijini kwa sisi wasafiri.
Tumeshindwa kuchangia kwa maana pia mtandao tuliohamia wa Halotel haujawekwa kwenye list ya mitandao ambayo tunapaswa kuchangia. Naombeni chama muongeze pia mtandao wa Halotel kwenye list yenu, msitusahau sisi ambao tulizitupa line za vodacom.
Ahsante.