Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,744
Ni mara nyingi amekuwa akija kwangu kulalamika jinsi ambavyo baba mmoja anamsumbua sana kumtaka kimapenzi. Bidada hajaolewa lakini ana mchumba. Ila ni mdada mkubwa tu (over 35 years).
Ushauri ambao mara kwa mara nimekuwa nampa ni kujitahidi kuwa mbali na huyo baba. Akutane naye tu kama kuna ulazima wa kufanya hivyo (wanafanya wote kazi) zaidi ya hapo awe mbali naye.
Jana yule dada kanipigia simu kuniuliza kama nitahudhuria workshop ambayo huyo baba kaiandaa (baba ni boss mkuu hapa tulipo, na mimi nafanya kazi nyingi sana na huyo boss). hiyo workshop ni ya nje ya ofisi, kazi yake binafsi, ila alituomba kama tunataka kushiriki kwa njia yoyote ile na ikiwezekana tumsaidie katika maandalizi.
Nikamwambia yule dada kuwa sitahidhuria, akanishangaa kwa nini, nikamwambia kwanza nina kazi nyingi sana lakini pia haikuwa lazima, na kwa nilivyobanwa nisingeweza kujitolea. huyo dada kwanza hafanyi kazi chini ya huyo baba, ingawa tupo idara moja, yeye ana bosi wake. lakini alipoona ile email aliamua kujitolea kumsaidia. kwa vile hafanyi kazi tunazozifanya, kwa hiyo kajitolea kumsaidia logistics wakati wa workshop.......
Hebu naomba mniambie huyu mdada anataka nini? nina uhakika wakitoka huko workshop (maana wanalala huko huko hotel) atakuja kunilalamikia jinsi alivyosumbuliwa.
Hapa nahitaji majibu yale makali kabisa ya kumjibu ili either (i) asije tena kunilalamikia upuuzi anaouendekeza mwenyewe, or (ii) aone clearly kuwa yeye ndo mchochezi mkuu wa hayo mambo kwa hiyo asiendelee kumlaumu baba wa watu.