Nimeshindwa kabisa kulalia upande wa kushoto

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,200
3,761
Naombeni msaada wa tatizo ninalokabiliana nalo tokea Sept 2012 hadi sasa.

Nikilala siwezi kutumia upande wa kushoto na pindi nikifanya hivyo naona kila kitu kinazungunga mle chumbani na mara nasikia kichefuchefu nakuanza kutapika.

Niliwahi kwenda kwa wataalamu wa Masikio akaaniambia hiyo ni center ya sikio imehama, akanipa dawa haikusaidia, nikaenda mahali pengine, wakasema kitu hicho hicho, na moja wa Madactari aliniuliza kama nimewahi kuanguka na gari, au kama nimewahi kupata ajali iliyohusisha kichwa kuumia sana, lakini hiyo haijawahi kunitokea.

Tafadhalini sana kwa mtu yeyote, daktari, mtaalamu mwenye idea na kinachonisibu anisaidie,naomba msaada wenu wadau.
 
Jamani, hakuna mwenye idea kabisa na tatizo hili, nisaidieni wakuu hata ushauri.
 
Mi nadhani ungeelea kuwatafuta watalaam tu ingesaidia. Ukiona kimya jua watu hawana idea na tatizo ilo. Nenda kwenye hosp ambazo ukwenda kabla utapata msaada.

Pole
 
Nenda tena kamuone Daktari akupime vizuri na lalia upande wa kulia ndio bora zaidi kuliko upande wa kushoto
 
Nashukuru HOPECOMFORT, nitazingatia ushauri wako.
 
Nenda tena kamuone Daktari akupime vizuri na lalia upande wa kulia ndio bora zaidi kuliko upande wa kushoto

Mkuu MziziMkavu ahsante sana kwa kunijuza hilo la kulalia kulia. Madaktari kweli wamenipima, ila nitarudi tena kule amabko bado sijaenda je una comment niende ipi? ahsante sana mkuu.
 
Jamani, hakuna mwenye idea kabisa na tatizo hili, nisaidieni wakuu hata ushauri.

hujisikii maumivu..? maelezo yako yanaonesha ni vestibular balance disoders.. mara nyng husababishwa na ear infections, head njury na vitu vngne vnavoweza kuleta madhara kwenye inner ear au brain.. ila ni vema zaid ukatafuta hosp yenye otolaryngologist atafanya yake... hili tatizo linatuchanganya wataalam weng hasa kwenye diagnosis na medication..
 
hujisikii maumivu..? maelezo yako yanaonesha ni vestibular balance disoders.. mara nyng husababishwa na ear infections, head njury na vitu vngne vnavoweza kuleta madhara kwenye inner ear au brain.. ila ni vema zaid ukatafuta hosp yenye parasitologist atafanya yake... hili tatizo linatuchanganya wataalam weng hasa kwenye diagnosis na medication..

Ahsante mkuu,ni kweli kabla ya tatizo sikio liliwahi kuumwa lakini siyo serious na nilipoenda kwa ENT specialist aliniambia, balance disorder. Aliniambia tatizo linaitwa Beniqn Positional Pararoxysual huenda nimekosea spelling (Vertigo) na huyu Dr alinipa dawa inayoitwa bataserc nilitumia kwa muda wa kutosha lkn bado tu tatizo lipo.

Mkuu nashukuru kwa muda wako na ushauri wako. Hapa kwetu Arusha hospital nimemaliza, mkuu kama unaushauri wa hospiali ipi niende nitashukuru. Be blessed.
 
nimekuelewa kaka.. dawa zpo lakini si za kumaliza tatizo 100% kuna physical therapy znasaidiaga sana,, vp umejaribu kufika KCMC, Dar pia unaweza pata ufumbuzi... all the best
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom