Elections 2010 Nimeshinda kwa kishindo!!!

Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
475
22
Ndiyo, nimeshinda kwenye kura za maoni tena nimewaacha mbali sana wapinzani wangu. Sina shaka na kupitishwa na chama kwani sikupata tuhuma zozote zinazothibitika za rushwa ama nyinginezo zinazoweza kukwamisha kupitishwa na chama japo watu wa takukuru walikuwa wengi jimboni na kuna wakati walitaka kuchafua hali ya hewa.

Nilicho-note ni kuwa TAKUKURU wanahitaji kufanya kazi zao kwa kuzingatia professional ethics na sio kama wanavyofanya sasa, nitawapasha baadaye yote kwa kirefu, sasa naenda kupumzika.

Nawashukuru wote walionipa moyo wa kuendelea. Nitawaarifu yote yaliyojiri kwa kirefu kidogo baada ya kuthibitishwa na vikao vya juu vya chama.

Mbarikiwe wote

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Hongera Mkuu na nina kutakia mafanikio mema katika kampeni.

Nina uhakika huko bungeni utakuwa ni mwiba kwa mafisadi kama sijakosea kukufananisha
 
Hongera zako nyingi sana, usisahau kumpa kura yako shujaa Slaa. Hakuna dhambi yoyote kugombea Ubunge kupitia CCM na kujipigia kura halafu kumpigia kura shujaa Slaa.
 
Hongera sana kwa kumaliza ngazi ya makundi, sasa fainali ndo inakuja, kaza buti.
 
Kumbe wewe ni sisiemu!!
Hongera lakini. unaweza kuwa kama kina selelii, Mwakyembe, Sitta, Kilango et al.
kumbuka kumpa kura yako Dr. Slaa
 
jamani wewe km mwana jf tafadhari hakikisha unapata watu kumi na zaidi, hakikisha mnapiga kura za ndio kwa chadema kuanzia rais dr slaa,mbunge wa jimbo lako kupitia chadema, na diwani wa chadema. usijipe moyo kwa ule umati unaotokea wakati wa kampeni, yasijetokea yale ya mrema 1995. kura kwa chadema.
 
wewe ni nani? tupe jina na jimbo ulilogombea...:A S-heart-2:
 
asante sana na sitakwa na suluhu na mafisadi, believe me!!

Hongera zako nyingi sana, usisahau kumpa kura yako shujaa Slaa. Hakuna dhambi yoyote kugombea Ubunge kupitia CCM na kujipigia kura halafu kumpigia kura shujaa Slaa.

umenena mkuu, lakini kumbuka mtu mtulivu huchagua kw utulivu. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Nani kakuuliza?

sio swali zuri hata kidogo kwani upashanaji habari si lazima uwe wa aina ya interview ama usaili!

Hongera sana kwa kumaliza ngazi ya makundi, sasa fainali ndo inakuja, kaza buti.

nashukuru kwa kunitia moyo. sina woga wala wasiwasi hata kidogo, nimejiandaa vizuri na chama changu kiko sawasawa mkuu, jimboni kwangu tutashinda ngazi zote

Hongera sana mwana JF.Endelea kutumia sera za CHADEMA.

hapana mkuu, natumia za CCM, za cadema bado hazijatamadunishwa kitanzania

Kumbe wewe ni sisiemu!!
Hongera lakini. unaweza kuwa kama kina selelii, Mwakyembe, Sitta, Kilango et al.
kumbuka kumpa kura yako Dr. Slaa

kati ya watu ambao sipendi kufanana nao ni hao uliowataja. binafsi niliunga mkono sita alipotakiwa kupokonywa kadi ya ccm. huwezi kuwa CCM kisha ukapiga siasa za kudandia kama unacheza santuri za muziki, hao uliowataja wamepungua sana kwenye mizani ya weledi

jamani wewe km mwana jf tafadhari hakikisha unapata watu kumi na zaidi, hakikisha mnapiga kura za ndio kwa chadema kuanzia rais dr slaa,mbunge wa jimbo lako kupitia chadema, na diwani wa chadema. usijipe moyo kwa ule umati unaotokea wakati wa kampeni, yasijetokea yale ya mrema 1995. kura kwa chadema.

mimi ni mwanasiasa na mrema hajapata kuwa mwanasiasa hata siku moja bali siku zote anafanya biashara

wewe ni nani kwa jina?

utajua soon mkuu, vuta subira

wewe ni nani? tupe jina na jimbo ulilogombea...:A S-heart-2:

jina na jimbo vinafuata soon
 
sio swali zuri hata kidogo kwani upashanaji habari si lazima uwe wa aina ya interview ama usaili!

Sasa hapa umetupasha habari kweli?? Hii ni habari au kitendawili?

Hii taarifa yako kama uliona huwezi kuikamilisha kwanini uilete jamvini??
 
Ndiyo, nimeshinda kwenye kura za maoni tena nimewaacha mbali sana wapinzani wangu. Sina shaka na kupitishwa na chama kwani sikupata tuhuma zozote zinazothibitika za rushwa ama nyinginezo zinazoweza kukwamisha kupitishwa na chama japo watu wa takukuru walikuwa wengi jimboni na kuna wakati walitaka kuchafua hali ya hewa.

Nilicho-note ni kuwa TAKUKURU wanahitaji kufanya kazi zao kwa kuzingatia professional ethics na sio kama wanavyofanya sasa, nitawapasha baadaye yote kwa kirefu, sasa naenda kupumzika.

Nawashukuru wote walionipa moyo wa kuendelea. Nitawaarifu yote yaliyojiri kwa kirefu kidogo baada ya kuthibitishwa na vikao vya juu vya chama.

Mbarikiwe wote

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Hongera mkuu maana safari hii mambo magumu,sana kaza buti maana uko uendako ni kugumu zaidi...achana na longolongo za wananchi..hiyo ni lazima kwa kila mkusanyiko wa watu
 
Hongera Mgombea Ubunge kura yako ya Urais iende kwa DR Slaa ..tunapenda mabadiriko yatokee
 
Back
Top Bottom