Nimeshinda jaribu la Shetani/Ibilisi bila Kukanyaga Mafuta ya Nabii

Lugumgya

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
629
1,997
Siku ya Jumatatu nikiwa natoka job niliapata bahati ya kukaa na mdada mmoja mzuri tu! Alikuwa dizaini ya Mobeto, Hamisa, lkn kiumri alikuwa Mdogo kwa Mobeto (hapa wote sijui umri wao).

Gari vuuuuuu! Vuuuuuu! Mara Ubungo! Tulikuwa tunaelekea Mbezi Louis, wengi wanaita Mbezi Mwisho au Mbezi ya Kimara! Tumemaliza ule mzunguko wa mchina tukashika barabara ya kuelekea Mbezi, dada akashika simu kupiga, mara akasema daaah, kumbe sina salio! Basi kiroho Safi nikampa simu yangu apige, akapiga, akasema huyo mtu haipatikani! Baadae kumbe akajibipu yeye! Then, akanipa simu yangu!

Nimefika home, mida ya saa 3 usiku naona meseji! Mamboz! Nikajibu, poa! Vip na Nani? Akasema, mm Nyamweko Salala, tulikuw wote kwenye daladala! Umenisaidia simu, ahsante Kaka! Okay, usijali!
Basi jana, tukachati Sana tu Ila kwa heshima kabisa, akaniuliza nafasi yangu, nikamwambia J5( Leo Sasa) niko free kabisa! Akasema kaka una roho nzuri Sana! Nikamwambia kawaida tu Mdogo wangu! Basi akanambia ana zawadi yangu, anataka anipatie Kama Shukrani! Nikajiuliza Shukrani ya nn tena! Basi, nikamwambia poa!

Baadae kidogo nikasita, nikamwambia nambie ni zawadi gani kwanza, akasema sijanunua chochote, ila utakachosema niko tayari! Basi wazo la kula kimasihara likaja, nikamwambia basi ngoja nitafute room ili unipe faraghani kabisa mrembo!

Akasema! Mmmh! Nikamwambia sorry Kama nimekukwaza! Akasema, hahahahah, hamna, lkn uwe na condom bila condom sikupi zawadi! Akanambia nimpe nusu saa atakuwa amefika sehem tuliyopanga kukutana!

Basi, baada ya chatting za hapa n pale, nikabaki najiuliza kichwani, kichwa kidogo kinaanza kushindana na kichwa kikubwa! Shahawa zinataka kushinda ubongo! Sijui kwa kuwa vyote ni vyeupe!!!

Mara nikapata wazo, nikimbie Mwenge niwahi kwa Manabii! Lkn dk zikawa zinakaribia! Nisingeweza kumuwah mlimbwendwe, maana nilitaka nikajipige mm fireeee na yeye ashindweeeee! Buy nafasi hiyo sikuipata!

Muda ukayoyoma, Mara nimefika Mageti, nimefika njia panda, yaani akitaja kituo kingine ndo ananifikia! Ningekuwa mwanamke ningemwambia niko period, mwanaume nimwambie nimetailiwa juzi bado haijapona? Mbona nitatia aibu! Mara huyu hapa! Roho ikawa inaniambia, lkn kwa nn, juzi tu Leo huyu mdada anataka kunitunuku! Basi kimoyo moyo, nikasema ee- bwana, najua sijazaliwa Nazareth, siko katika ufalme wa Daud, lkn mm ni mja wako! Naomba, Mimi na huyu mdada mzuri utuepushe na mwovu ibilisi!

Kama baba umetuunganisha kwa nia njema, sawa, kama baba ni msukumo wa shetani basi tuondolee tamaa inayotuwakia muda huu! Nikamalizia kusema kwa Nguvu fayaaaaaaaaaaaaaaa, masakla, masakla ya masakla bhanga! Nikaweka na mikono juu kidogo! Bwana tenda miujiza, ulifanya njia pasipo kuwa na njia, nasi tuondolee hii tamaa!

Nikamalizia, ahsante Yesu! Mara nasikia mwenzangu, kumbe wew ni mlokole ndo maana ni mpole hivo, nikamwambia ndiyo, tena shahidi wa Yehova!
Akanambia, muda unaenda, unajua mm silali, mbona hatufiki, nikamtumia meseji jamaa yangu, anipigie kuwa nahitajika haraka kuna dharura! Dk hazikupita jamaa, katwanga, Lugumya wahi, nikamwambia dk 10 nitakuwa hapo! Nikampa 5000, nikamwambia tutaonana!

Akachukua hela, akasema pole, so lini? Nikamwambia tutapanga! Nikawa nimeshinda jaribu bila kukanyaga Mafuta! Mpaka saiv, nasema, Yesu ni Bwana! Najipiga kifuani, kuhushudia utukufu wa Mungu bila Mafuta!

Je, Kuna yeyote aliyewah kushinda jaribu bila kukanyaga Mafuta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ghafla siku ya mwisho unajikuta jehanamu. Sipati picha atakavyokuwa unalia na kusaga meno ukikumbuka hili tukio

God save us
 
Hahahaah, ni ngumu kuruka bicons zote Mkuu! Nimeweza Jana, simaanishi itakuwa hivo milele! Naamini hata wew Kuna sehemu uliwahi kushinda, lkn Kuna sehemu ulikwama! Maana mengine yanakuja si kwa akili yako, lkn Mungu anatumia Nguvu yake kukuepusha na jambo fulani!

So huo ni ushuhuda wa Jana, lkn simaanishi kuwa msafi zaidi yako!
Ghafla siku ya mwisho unajikuta jehanamu. Sipati picha atakavyokuwa unalia na kusaga meno ukikumbuka hili tukio

God save us

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom