Nimeshasajili kampuni LTD ya udalali wa Nyumba za kupanga/kuuza, viwanja na mashamba. Naomba ushauri

MJASIRIA MALI

Member
Aug 13, 2012
79
0
Heshima mbele.

Wandugu nimeshasajili kampuni kamili LTD by share. Lengo lake muhimu ni kufanya kazi ya udalali wa Nyumba za kupanga,kuuza, viwanja mashamba hasa mkoa wa pwani. Tunategemea kuweka magari baadaye.

Hata hivyo, nimekumbana na Changamoto ya madalali wa chini ya mti ambao hawataki kunipa ushirikiano. Wengi wameniambia live kwamba tukishirikiana na wewe na baadaye wateja wakijua ofisini kwako watakuwa wanakuja moja kwa moja kwako na sisi itakula kwetu. Ni kama wanaambina sasa hapa ubungo tena sipati ushirikiano wao. Kwa unyenyekevu sana naomba ushauri wenu nitokeje?

Pili, nina tatizo la matangazo. Siwezi kutumia magazeti redio na TV kwa sasa kwa sababu ya kiuchumi. Kidogo kidogo nilkuwa naanza kuweka broshure ( black and white) si nzuri sana lakini pia haijaniletea matokea mazuri. Naombeni ushauri wenu kabla sijakata tamaa. Mlioanzisha biashara mlivukaje changamoto hizi?
 
Bosco Ntaganda

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
710
500
Tumia teknolojia mkuu. Unaweza kuwa na Facebook Page, Twitter, Blog na baadae Website. Nakutangaza kazi zako huko, hakika habari zako zitaenea kama moto wa petroli
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,379
2,000
Heshima mbele.
Wandugu nimeshasajili kampuni kamili LTD by share. Lengo lake muhimu ni kufanya kazi ya udalali wa Nyumba za kupanga,kuuza, viwanja mashamba hasa mkoa wa pwani. Tunategemea kuweka magari baadaye.

Hata hivyo, nimkumbana na Changamoto ya madalali wa chini ya mti ambao hawataki kunipa ushirikiano. Wengi wameniambia live kwamba tukishirikiana na wewe na baadaye wateja wakijua ofisini kwako watakuwa wanakuja moja kwa moja kwako na sisi itakula kwetu. Ni kama wanaambina sasa hapa ubungo tena sipati ushirikiano wao. Kwa unyenyekevu sana naomba ushauri wenu nitokeje?

Pili, nina tatizo la matangazo. Siwezi kutumia magazeti redio na TV kwa sasa kwa sababu ya kiuchumi. Kidogo kidogo nilkuwa naanza kuweka broshure ( black and white) si nzuri sana lakini pia haijaniletea matokea mazuri. Naombeni ushauri wenu kabla sijakata tamaa. Mlioanzisha biashara mlivukaje changamoto hizi?

Hii biashara ni nzuri.

Ukijitangaza na kuainisha tofauti kati yako na hao madalali tapeli utapata wateja wengi. Wengi wamechoshwa na hao madalali wanaoongeza kodi za nyumba. Jipange tu
 
Papizo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
4,705
2,000
Ingia instagrm msearch jamaa mmoja anaitwa dalali wa nyumba anza kwanza kama yeye tangaza kila kitu online na weka details zako na ofisi yako ilipo and everything then lazima itakutoa achana na hao madalali
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,655
2,000
Real Estate Agent inalipa sana ila inabidi uwe serious, biashara mwanzoni ni mgumu ila kama una huduma za uhakika bila kubabaisha lazima itakutoa tu.

Nakushauri yafuatayo:
1. Ukiweza tengeneza website ya kampuni yako, ambayo inatakiwa iwe updated mara kwa mara ukishindwa tumia blog.
2. Tumia mitandao kama facebook, twitter, instagram, pinterest, kutangaza biashara yako.
3. Ajiri vijana kama wanne hivi ambao kazi yao kuzunguka mitaani kukusanya taarifa za vyumba, nyumba, viwanja haafu unawazitangaza mtu akipanga au kununua unamlipa kwa kamisheni, kama 10% ya kile anachokileta.
 
Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
1,500
Heshima mbele.
Wandugu nimeshasajili kampuni kamili LTD by share. Lengo lake muhimu ni kufanya kazi ya udalali wa Nyumba za kupanga,kuuza, viwanja mashamba hasa mkoa wa pwani. Tunategemea kuweka magari baadaye.

Hata hivyo, nimekumbana na Changamoto ya madalali wa chini ya mti ambao hawataki kunipa ushirikiano. Wengi wameniambia live kwamba tukishirikiana na wewe na baadaye wateja wakijua ofisini kwako watakuwa wanakuja moja kwa moja kwako na sisi itakula kwetu. Ni kama wanaambina sasa hapa ubungo tena sipati ushirikiano wao. Kwa unyenyekevu sana naomba ushauri wenu nitokeje?

Pili, nina tatizo la matangazo. Siwezi kutumia magazeti redio na TV kwa sasa kwa sababu ya kiuchumi. Kidogo kidogo nilkuwa naanza kuweka broshure ( black and white) si nzuri sana lakini pia haijaniletea matokea mazuri. Naombeni ushauri wenu kabla sijakata tamaa. Mlioanzisha biashara mlivukaje changamoto hizi?
Naomba unidokeze juu ya utaratibu wa kusajili kampuni ya udalali wa nyumba za kupanga na kuuza viwanja
 
Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
1,500
Real Estate Agent inalipa sana ila inabidi uwe serious, biashara mwanzoni ni mgumu ila kama una huduma za uhakika bila kubabaisha lazima itakutoa tu.

Nakushauri yafuatayo:
1. Ukiweza tengeneza website ya kampuni yako, ambayo inatakiwa iwe updated mara kwa mara ukishindwa tumia blog.
2. Tumia mitandao kama facebook, twitter, instagram, pinterest, kutangaza biashara yako.
3. Ajiri vijana kama wanne hivi ambao kazi yao kuzunguka mitaani kukusanya taarifa za vyumba, nyumba, viwanja haafu unawazitangaza mtu akipanga au kununua unamlipa kwa kamisheni, kama 10% ya kile anachokileta.
naweza vipi kusajili kampuni ya udalali wa nyumba za kupanga na viwanja
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom