Nimeshangazwa sana na majibu ya mama wa rafiki yangu

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,601
4,085
NIMESHANGAZWA SANA NA MAJIBU YA MAMA WA RAFIKI YANGU.

Wakuu,

Kuna rafiki yangu huku kitaa amekuwa aki_date na manzi fulani ambaye kiumri wanalandana,
Ila huyo manzi ana mtoto wa miaka minne ambaye baba yake alimtelekeza kitambo.

Sasa huyu mshikaji wangu amefikia maamuzi ya kutaka kumuoa huyu binti,
Na akaona jambo la kwanza ni kumjuza Bi. Mkubwa wake.

Hivyo akanifuata kama rafiki/ndugu wa karibu ili nimsindikize kwa mama yetu (mama yake) tukampe habari njema,
Ikizingatiwa mama amekuwa akiulizia sana kipengele cha mwanaye kuoa.

--------------
Kiukweli Mama alitupokea vizuri kwa shangwe na bashasha tele,
Kwani jamaa alishamdokeza mama kuwa mazungumzo yanahusu habari njema za kubeba jiko.

Msh'kaji alifunguka vema sana kwa Mama,
Na mama akaonekana kuwa furaha, nderemo na shauku kubwa sana ya kumwona mkwewe tarajali.

Akiwa na uso wenye tabasamu pana,
Akaniangalia huku akisema,

" Seneta Wa Mtwiz,
You see ??
It's high time now you young men need to have fruitful social decisions of this kind,

Mind you that,
Our sons getting hitched is amongst notable prides of we parents-

In so doing,
Let your friend start,
And so you follow the very same path-
Since your parents are alongside you in any move towards a prosperous future of you guys.

Simply saying,
We'll support you morally and materially-
Go on guys!!! "

Bi. Mkubwa aliongea meno yote yakiwa nje kwa furaha.

-----------
Ila kiukweli mchizi wangu kuna kipengele alikikwepa kumwambia maza wake kwenye mazungumzo yake-
Hakumwambia 'Maza' kuwa mkwe tarajali alishazaa na jamaa mwingine miaka minne iliyopita.

Mother alipotoka sebuleni kwenda kuturekebishia menyu jikoni-
Mi' nikaona kuna haja ya kuvunja ukimya,

Nikamchana mwana,
Nikamwambia,
"Mwanangu hapa usifiche kitu-
Huyu ni maza wako mzazi,
Mwambie ukweli wa kila kitu ili Bi. Mkubwa aujue uhalisia,
Kuliko kuficha vitu sensitive kama hivyo- baada'e mtaanza kulaumiana.
Kumwambia 'maza' hicho kipengele ni typical unkwepable!!!"

----------
Basi maza aliporejea,
Mchizi akaanza kujing'atang'ata pale-
Kisha akamwambia kuhusu hicho kipengele.

Aisee !!!
Maza mzuka wote ukamwishia,
Hadi sura yake yenye bashasha, shangwe na nderemo ikakunja ndita kiaina.

Huyu maza ni mtu fulani mkarimu sana,
Mwenye busara, hekima na maadili ya hali ya juu,
Ni mtu ambaye amekuwa akiheshimika sana katika jamii kwa upeo wake wa juu na matumizi sahihi ya elimu yake ya shahada mbili (kitaaluma yeye ni gynecologist i.e daktari 'specialist' wa magonjwa ya wanawake).

Kilipita kimya kama cha dakika 11 na sekunde 4 hivi huku mama akionekana kutafakari jambo,
Na sisi tukiwa tumetulia kimya tukisubiri madini atakayoyatema huyu mama (maana'ke ni mtu fulani mwenye hoja kuntu mithili ya zile za Mbunge Lissu dhidi ya 'Mashilingi').

-------
Tofauti na ambavyo tulitarajia,
Bi. Mkubwa aliongea maneno matatu tu-
Maneno ambayo hayakutarajiwa kusikika katika kinywa chake kwa hadhi, umri na nafasi yake.

Maza alituangalia,
Akasema,
"Madogo, Acheni Us*nge!!!"

---------
Na nd'o ukawa mwisho wa mazungumzo kwa kikao hicho.

Mpaka hivi sasa sijaielewa mantiki ya majibu ya huyu maza wa rafiki yangu kwa kweli.

"ILA MAISHA LAZIMA YAENDELEE."
 
Dakika 20 kabla mpira kuanza goli ni 0 : 3.... Hapo vipi wewe wa nyumbani utashinda...???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bi mother ame kufananisheni na wanaume wa mikoani 🤣🤣

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom