Nimeshangaa sana NSSF, asilimia kubwa wanaodai mafao ni vijana na si wazee kama ilivyokuwa zamani

Fao la kukosa ajira si ndo la kulipwa kwa miezi sita 33% ya mshahara wako wa mwisho? Mimi namaanisha Kuna possibility ya kuchukua michango yako yote kwa mkupuo?.
Hiyo huwezi mzee labda ukaipate Kenya, Tanzania hakuna biashara ya hivyo
 
Wanakupa asilimia 33% ya mshahara wako uliokuwa unapata kabla ya kuachishwa kazi kwa muda wa miezi sita then usubiri tena miezi 18 ndio watakupa pesa yako iliyobakia.
Sidhani kama baada ya miezi 18 wanakupa hela iliyobakia. Sheria yao inasema baada ya miezi 18 unaweza kuomba kuhama kwenda kwenye mfuko wa kuchangia kwa hiyari na hawasemi watakupa hela zilizobakia ila wanasisitiza uendelee kuchangia kwa hiyari. Kama kuna mtu amechukua michango yake baada ya miezi 18 atoe ushahidi.
 
Kuna haja voluntary retirement age ya nchi hii iwe 35 na mandatory retirement age iwe 40! Tatizo litakuwa limekwisha. Beyond 40 tuwaachie wanasiasa tu maana wao kazi zao hazifungwi na umri; ajabu sana!
Ushauri huo ni wakishirikina mkuu, utakua unafanya biashara wewe unachukia walioajiriwa
 
Wanatoa asilimia 33 ya mshahara wako wa mwisho.! Kwa wale wasio na professional wanalipwa yote ndani ya miezi mitatu ila Kwa wale wenye professional wanalipa hiyo 33 asilimia Kwa miezi sita ya kukosa ajira baada ya hapo
Wanakutaka ukae miezi 18 yaani uendelee kutokuwa na ajira then ndio utaruhusiwa kuomba kutoa pesa yote.!
Kwani mafao, bado yanatolewa, si kuna tamko Hadi mtu afikishe miaka 60.Ama Mimi nimelala usingizini bado?
 
Kuna haja voluntary retirement age ya nchi hii iwe 35 na mandatory retirement age iwe 40! Tatizo litakuwa limekwisha. Beyond 40 tuwaachie wanasiasa tu maana wao kazi zao hazifungwi na umri; ajabu sana!
Be serious mkuu! Kwa mfumo wa elimu ya kibongo naona kama kwa huo umri ni kuwaonea watu.
 
Juzi Kati nikiwa kwenye jiji la maraha niliingia kwenye ofisi moja ya mkoa ya NSSF. Nilichokuta pale kilinishangaza sana, kulikua na watu wazima wawili wengine wote zaidi ya 50 Ni vijana under fourty years. Wote wamesimamishwa kazi wamekuja kudai mafao.

Ilibidi yule Askari wa suma pale getini awe na kazi ya ziada ya kuruhusu waingie kumi kumi kupunguza msongamano ndani.

Zamani NSSF ulikua hukuti mtu asiye na mvi au kipara. Leo hii wanaodai mafao vichwani Ni viduku na Rasta kwa wadada kichwani Ni twende kilioni.

Kwa anayefuatilia habari za kitaifa na za kimataifa hiyo sio ajabu....
Haujui mji wa Arusha unategemea biashara ya utalii kwa kama 60% ambayo kwa kiasi kikubwa imeathiriwa na Korona
hivyo makampuni mengi hasa yale yenye wafanyakazi wengi yameshindwa kujiendesha na kulazimika kupunguza wafanyakazi...
 
Kwa anayefuatilia habari za kitaifa na za kimataifa hiyo sio ajabu....
Haujui mji wa Arusha unategemea biashara ya utalii kwa kama 60% ambayo kwa kiasi kikubwa imeadhiriwa na Korona
hivyo makampuni mengi hasa yale yenye wafanyakazi wengi yameshindwa kujiendesha na kulazimika kupunguza wafanyakazi...
Mimi nimesemea Dar kwenye viwanda. Huku ziko hizo kampuni za watalii lakini number ni negligible.
 
Back
Top Bottom