Nimeshangaa kuona leo Rais Samia, katika kikao Cha maadhimisho ya 20 ya Baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika, akiwa hana walinzi!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,526
30,239
Kwa mara ya kwanza katika historia ya tokea Rais Samia awe Rais wa nchi hii, takribani miaka 3 iliyopita, sijawahi kumshuhudia Rais Samia, akihudhuria shughuli yoyote Ile, iwe ni Kwenye mkutano wa hadhara au kikao Cha ndani na hata shughuli za kidini, Rais Samia akiwa hana wale walinzi wake (body guards) wakimlinda.

Leo Kwa mara ya kwanza nimemshuhudia Rais Samia akiwa hana wale walinzi wake (body guards) tuliowazoea!

Nimetafakari sana hatua hii, pengine ni katika kuwaonyesha wale viongozi wengine wageni, kuwa nchi yetu Iko salama na ina amani tele.

Hata hivyo nimeipenda hii staili aliyoianzisha Rais Samia, ya kutowategemea walinzi wake, ambao ni Binadamu wenzake kumlinda. Kwa kuwa Mimi naamini ulinzi pekee wa uhakika wa sisi Binadamu unatoka Kwa Mungu pekee.

Unaweza ukawa na ulinzi wa mabunduki ya rashasha, lakini Mungu akiamua kuchukua roho yako Wala hashindwi

Tumeshuhudia vifo kadhaa ya viongozi wakubwa sehemu mbalimbali duniani, wakitwaliwa na Mungu, pamoja na kuwa walikuwa na walinzi wao binafsi, wakiwa na mabunduki ya rashasha!

Kwa hiyo nitoe ushauri kwenu viongozi, msiwategemee sana Binadamu wenzenu Kwa ulinzi wenu, Bali mtegmee ulinzi wa Mungu wetu, ambao ndiyo wa uhakika kabisa.
 
Wala usiwe na wasiwasi wa aina yoyote ile kwa kuwa Rais wetu Yupo Salama katika mikono Salama ya Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa akimlinda ,kumpigania na kumtetea wakati wote.

Lakini pia ni kuwa nchi na Taifa letu ni salama na amani imetawala kabisa.pia vyombo vyetu vya ulinzi vimeendelea kufanya kazi nzuri na njema na vinaujuwa vinafanya nini.

vyombo vyetu vipo makini na macho katika ulinzi wa Rais wetu na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na hapo alipo usalama ni wakutosha na hata sisiminzi hawezi kufanya chochote wala kusogelea maiki ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi.

Hapo huwezi hata kusogelea Rais wala kujitokea huko kwenye kiti chako ukajifanya unaenda kumsalimia Mheshimiwa Rais,huwezi hata kujipitisha mbele yake hovyo hovyo.kila kinachofanyika na kutokea hapo kipo katika utaratibu na mpangilio unaofahamika .

Ulinzi wa Rais siyo sawa na ule kama wa kina Diamondi na Harmonize wa kubeba tu watu wenye vifua vikubwa na mikono mikubwa bila kuzingatia ukubwa wa akili zao za kutumia milango sita ya kung'amua jambo.
 
Wala usiwe na wasiwasi wa aina yoyote ile kwa kuwa Rais wetu ni Yupo Salama katika mikono Salama ya Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa akimlinda ,kumpigania na kumtetea wakati wote.

Lakini pia ni kuwa nchi na Taifa letu ni salama na amani imetawala kabisa.pia vyombo vyetu vya ulinzi vimeendelea kufanya kazi nzuri na njema na vinaumjuwa vinafanya nini.

Vmvyombo vyetu vipo makini nacho katika ulinzi wa Rais wetu na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na hapo alipo usalama ni wakutosha na hata sisiminzi hawezi kufanya chochote wala kusogelea maiki ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi
Wewe baki huko huko kwenye kusifia watu bila nukta, wachana na mambo ya Mungu. Mungu hana maslahi yoyote kwenye uzembe wa mtu kujilinda au kujipigania. Ndio mana hata Waisrael walikuwa na jeshi ili kujilinda sio tu kusubiri miujiza ya Mungu.
 
Hebu tutafakari, namna yule Mwendazake alivyokuwa akiambatana na walinzi kibao wenye mabunduki ya rashasha, Kwenye misafara yake, lakini hatimaye Mungu alimtwaa!

Tupate Somo hapo
 
Wewe baki huko huko kwenye kusifia watu bila nukta, wachana na mambo ya Mungu. Mungu hana maslahi yoyote kwenye uzembe wa mtu kujilinda au kujipigania. Ndio mana hata Waisrael walikuwa na jeshi ili kujilinda sio tu kusubiri miujiza ya Mungu.
Mambo ya kiusalama waachie vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wa Rais .Rais wetu yupo Salama na hapo hata sisiminzi hawezi kuisogelea meza yake wala kiti chake na hakuna mtu yeyote anayeweza kumsogelea wala kumgusa wala kumshika mkono Mheshimiwa Rais kwa bahati mbaya au bila utaratibu.
 
Africa sanaa sana. Viongozi wa Africa wapo wanakula bata huku wenzao DRC ,Sudani ......nk wanakufa na hakuna lolote la maana baraza limefanya.
Amani ya Congo na sudani inatakiwa itengenezwe na wakongo na wasudani wenyewe.wasipojitambua na kutambua hilo wataendelea kuuana na kuchinjana wao kwa wao kwa maslahi ya watu wengine.
 
Mambo ya kiusalama waachie vyombo bmvyegu vya ulinzi na usalama wa Rais .Rais wetu yupo Salama na hapo hata sisiminzi hawezi kuisogelea meza yake wala kiti chake na hakuna mtu yeyote anayeweza kumsogelea wala kumgusa wala kumshika mkono Mheshimiwa Rais kwa bahati mbaya au bila utaratibu.
Hapo umesema. Lakini kuniambia eti rais analindwa na Mungu ni uwongo wa mchana kweupe.
 
President Kabila aliuawa na walinzi wake. Pengine mama kastuka.
Absolutely true👏👏

Hata Kwenye Biblia imeandikwa kuwa alaaniwe yule mtu anayemtegemea Binadamu mwenzie
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Kwa mara ya kwanza katika historia ya tokea Rais Samia awe Rais wa nchi hii, takribani miaka 3 iliyopita, sijawahi kumshuhudia Rais Samia, akihudhuria shughuli yoyote Ile, iwe ni Kwenye mkutano wa hadhara au kikao Cha ndani na hata shughuli za kidini, Rais Samia akiwa hana wale walinzi wake (body guards) wakimlinda.

Leo Kwa mara ya kwanza nimemshuhudia Rais Samia akiwa hana wale walinzi wake (body guards) tuliowazoea!

Nimetafakari sana hatua hii, pengine ni katika kuwaonyesha wale viongozi wengine wageni, kuwa nchi yetu Iko salama na ina amani tele.

Hata hivyo nimeipenda hii staili aliyoianzisha Rais Samia, ya kutowategemea walinzi wake, ambao ni Binadamu wenzake kumlinda. Kwa kuwa Mimi naamini ulinzi pekee wa uhakika wa sisi Binadamu unatoka Kwa Mungu pekee.

Unaweza ukawa na ulinzi wa mabunduki ya rashasha, lakini Mungu akiamua kuchukua roho yako Wala hashindwi

Tumeshuhudia vifo kadhaa ya viongozi wakubwa sehemu mbalimbali duniani, wakitwaliwa na Mungu, pamoja na kuwa walikuwa na walinzi wao binafsi, wakiwa na mabunduki ya rashasha!

Kwa hiyo nitoe ushauri kwenu viongozi, msiwategemee sana Binadamu wenzenu Kwa ulinzi wenu, Bali mtegmee ulinzi wa Mungu wetu, ambao ndiyo wa uhakika kabisa.
Wameharibu sana hotuba. Ukalimani wa aina hiyo haufai kabisa. Utadhani news reporter.
Muacheni JK ashuke bilq sauti yake kuingiliwa na mkalimani. Nikechukia sanaa.
 
Kwahiyo hata mabenki nayo yaondolewe ulinzi yatalindwa na Mungu? Nchi isiwe na Jeshi tuache ilindwe na Mungu?

Hata mitume walipigana vita na walikua na wafuasi wao/Jeshi lao.
 
Wala usiwe na wasiwasi wa aina yoyote ile kwa kuwa Rais wetu Yupo Salama katika mikono Salama ya Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa akimlinda ,kumpigania na kumtetea wakati wote.

Lakini pia ni kuwa nchi na Taifa letu ni salama na amani imetawala kabisa.pia vyombo vyetu vya ulinzi vimeendelea kufanya kazi nzuri na njema na vinaujuwa vinafanya nini.

vyombo vyetu vipo makini na macho katika ulinzi wa Rais wetu na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na hapo alipo usalama ni wakutosha na hata sisiminzi hawezi kufanya chochote wala kusogelea maiki ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi.

Hapo huwezi hata kusogelea Rais wala kujitokea huko kwenye kiti chako ukajifanya unaenda kumsalimia Mheshimiwa Rais,huwezi hata kujipitisha mbele yake hovyo hovyo.kila kinachofanyika na kutokea hapo kipo katika utaratibu na mpangilio unaofahamika .

Ulinzi wa Rais siyo sawa na ule kama wa kina Diamondi na Harmonize wa kubeba tu watu wenye vifua vikubwa na mikono mikubwa bila kuzingatia ukubwa wa akili zao za kutumia milango sita ya kung'amua jambo.
Dah! hii ni zaidi ya uchawa
 
Back
Top Bottom