Nimeshangaa kuona Bajaji iliyobuniwa na Mtanzania kunyimwa vibali!

Kwakweli inauma sana,ndio maana mimi nasemaga vyombo kama bajaji na pikipiki usajili wake uwe tofauti na magari,usajili wake uwe unafanyika kwenye halmashauri na manispaa tu.
 
Sio kila chombo cha moto kinaingizwa barabarani, kuna standards. Ikiruhusiwa na kusababisha ajali sababu ya kukosa viwango pia mngeilaumu mamlaka husika.
Kulikuwa kuna ubaya gani Serikali kusapoti au kuingia ubia na mhusika na kufanya investment kwenye uo ubunifu ili kumeet izo standards
 
We mleta mada unamatatizo sana. Kama wewe ni kijana basi wapaswa kielewa kuwa bajaji ni trade mark. Mtanzania ataundaje bajaj? Yaani ni sawa na kusema mtanzania amebuni rangerover? Au amebuni benz. Tutabaki kuwa hivi hivi kwasababu ya ujinga wetu watanzania kama wewe.
 
watanzania tunapenda sana "spoon feeding". sio kazi ya serikali kumboreshea huyo mzee hiyo bajaji wala sio kazi ya serikali kuwa mbia/mwekezaji kwenye hiyo biashara.
Kinachofanyika nchi za wenzetu wanaojielewe ni ukitengeneza prototype ya ubunifu wako basi unatafuta wabia (watu wenye uwezo wa kuwekeza pesa zao kwenye hiyo biashara) kisha unawashawishi na kuwaonesha jinsi ubunifu wako unavyoweza kuwaingizia mabilioni, wakikubali kuwekeza hapo ndipo utaajiri wataalamu mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu wa "quality control" na hao ndio watakao hakikisha unatengeneza bidhaa zenye ubora.
kazi ya serikali itakua ni kuhakiki ubora wa hizo bidhaa na kukusanya kodi tu!
tuache tabia za kijamaa kulilia serikali kila kitu ni mentality ya kipuuzi kabisa.
 
Sio kila chombo cha moto kinaingizwa barabarani, kuna standards. Ikiruhusiwa na kusababisha ajali sababu ya kukosa viwango pia mngeilaumu mamlaka husika.
Kwa hiyo Mabasi yanayoua Kila siku hayako kwenye viwango? Hilo karatasi la viwango vya mzungu usipotupa chooni .Huji gundua kitu.wazungu wakigundua kitu hicho ndicho wanatangaza kuwa ndio kiwango kipya.Wakigundua version ingine wanakuletea karatasi ingine ya viwango vipya utapasuka kichwa kwa kukariri viwango vya wazungu vikiwemo viwango vya vyoo anavyonyea mzungu Na masinki yake.Mswahili akigundua choo Na sink lake kazi yako utalinganisha Na hicho cha mzungu Na kukataa ukiona kiko tofauti Bila kujali kama makalio ya wazungu Na waswahili yanafanana au la.Loooooo
 
View attachment 854490
Nimeona hii habari nikasikitika Sana, hivi Tanzania ya viwanda tunataka iwe ya viwanda gani?
Nilitegemea serikali na taasisi mbalimbali wajitokeze wamsapoti Huyu mzee aliyebuni hii Bajaji
Ila walichokifanya ni kumnyima vibali eti kisa Bajaji haijakidhi viwango,sasa kama haijakidhi viwango si ndio fursa hiyo ya kuingia ubia na huyo mzee ili kuboresha hiyo Bajaji.
Soko la Bajaj lipo hapa kwetu Tanzania na Africa kwa ujumla, kwa kutumia ubunifu wa Bajaj inayobeba abiria wengi(kama 7) tungeleta ushindani na products nyingine toka China na pengine.
Rai yangu Serikali na taasisi mbalimbali tujitahidi kuinua teknolojia yetu kwa kuwasapoti wajasiriamali na wabunifu mbalimbali wa hapa kwetu ili tuweze kuifikia Tanzania ya viwanda.
EMBU WE MLETA MADA SEMA MWENYEWE HAPA KAGUNDUA NN ZAIDI YA KUUNGAUNGA HILI NI ZAIDI YA CHOTARA MARATIRI YA GARI LINGINE NODI SIJUI YA MANDOLIN AU embu tuwage wakweli kuna kugundua kuvumbua na kukopi hapo jamaa kafanya nn
 
watanzania tunapenda sana "spoon feeding". sio kazi ya serikali kumboreshea huyo mzee hiyo bajaji wala sio kazi ya serikali kuwa mbia/mwekezaji kwenye hiyo biashara.
Kinachofanyika nchi za wenzetu wanaojielewe ni ukitengeneza prototype ya ubunifu wako basi unatafuta wabia (watu wenye uwezo wa kuwekeza pesa zao kwenye hiyo biashara) kisha unawashawishi na kuwaonesha jinsi ubunifu wako unavyoweza kuwaingizia mabilioni, wakikubali kuwekeza hapo ndipo utaajiri wataalamu mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu wa "quality control" na hao ndio watakao hakikisha unatengeneza bidhaa zenye ubora.
kazi ya serikali itakua ni kuhakiki ubora wa hizo bidhaa na kukusanya kodi tu!
tuache tabia za kijamaa kulilia serikali kila kitu ni mentality ya kipuuzi kabisa.
Pia kikubwa watu wanamshabikia jamaa ni kwamba ametengeneza ila hajavumbua yeye. Hapo ametumia mechanics za uundaji wa bajaji sema yeye kaifanya kienyeji.
 
Labda wanamshauri jinsi ya kujenga .. Ujue hiko kifaa kinahusu maisha ya watu HV equilibrium imefanikiwa .. Yani safety measure were they taken into consideration

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo Mabasi yanayoua Kila siku hayako kwenye viwango? Hilo karatasi la viwango vya mzungu usipotupa chooni .Huji gundua kitu.wazungu wakigundua kitu hicho ndicho wanatangaza kuwa ndio kiwango kipya.Wakigundua version ingine wanakuletea karatasi ingine ya viwango vipya utapasuka kichwa kwa kukariri viwango vya wazungu vikiwemo viwango vya vyoo anavyonyea mzungu Na masinki yake.Mswahili akigundua choo Na sink lake kazi yako utalinganisha Na hicho cha mzungu Na kukataa ukiona kiko tofauti Bila kujali kama makalio ya wazungu Na waswahili yanafanana au la.Loooooo
Wewe ndio umeathiriwa na wazungu. Common sense tu, hata sisi tuna standards.
 
View attachment 854490
Nimeona hii habari nikasikitika Sana, hivi Tanzania ya viwanda tunataka iwe ya viwanda gani?
Nilitegemea serikali na taasisi mbalimbali wajitokeze wamsapoti Huyu mzee aliyebuni hii Bajaji
Ila walichokifanya ni kumnyima vibali eti kisa Bajaji haijakidhi viwango,sasa kama haijakidhi viwango si ndio fursa hiyo ya kuingia ubia na huyo mzee ili kuboresha hiyo Bajaji.
Soko la Bajaj lipo hapa kwetu Tanzania na Africa kwa ujumla, kwa kutumia ubunifu wa Bajaj inayobeba abiria wengi(kama 7) tungeleta ushindani na products nyingine toka China na pengine.
Rai yangu Serikali na taasisi mbalimbali tujitahidi kuinua teknolojia yetu kwa kuwasapoti wajasiriamali na wabunifu mbalimbali wa hapa kwetu ili tuweze kuifikia Tanzania ya viwanda.
Aweke Bendera za Ccm itaruhusiwa
 
EMBU WE MLETA MADA SEMA MWENYEWE HAPA KAGUNDUA NN ZAIDI YA KUUNGAUNGA HILI NI ZAIDI YA CHOTARA MARATIRI YA GARI LINGINE NODI SIJUI YA MANDOLIN AU embu tuwage wakweli kuna kugundua kuvumbua na kukopi hapo jamaa kafanya nn
Waliogundua ndege ni wright brothers sijui ni Wamarekani lakini hata China wanatengeneza.
Jamaa kabuni bajaj inayobeba abiria sita, hii ni sawa na aliyegundua simu alikuwa mwingine,lakini wakaja wabunifu wakaleeta simu za batani,mara smartphone
 
Kwakweli inauma sana,ndio maana mimi nasemaga vyombo kama bajaji na pikipiki usajili wake uwe tofauti na magari,usajili wake uwe unafanyika kwenye halmashauri na manispaa tu.
Wangeruhusu hata iwe Na leseni ya barabara za vijijini isikanyage mjini at least kumpa time ya kuona uwezo wa chombo chake .Hawajamtendea haki mamlaka husika watoe majibu kwa nini wamemkatalia mbele ya umma wanaandishi wa habari Na wabunge Bila kujali vyama saidieni kuhoji
 
Wangeruhusu hata iwe leseni ya barabara za vijijini isikanyage mjini at least kumpa time ya kuona uwezo wa chombo chake .Hawajamtendea haki mamlaka husika watoe mujibu kwa nini wamemkatalia mbele ya umma wanaandishi wa habari Na wabunge Bila kujali vyama saidieni kuhoji
Maafsaa vitambi wengine shida tu.
 
Kinachotakiwa hapa ni SIDO wamwelekeze namna ya kuifanya Bajaji hii ifikie "viwango" vinavyotakiwa. Serikali inapaswa kumpa "elimu" zaidi na siyo tu kumnyima kibali. Naamini akielekezwa atatengeneza Bajaji inayokidhi viwango vilivyowekwa.
 
watanzania tunapenda sana "spoon feeding". sio kazi ya serikali kumboreshea huyo mzee hiyo bajaji wala sio kazi ya serikali kuwa mbia/mwekezaji kwenye hiyo biashara.
Kinachofanyika nchi za wenzetu wanaojielewe ni ukitengeneza prototype ya ubunifu wako basi unatafuta wabia (watu wenye uwezo wa kuwekeza pesa zao kwenye hiyo biashara) kisha unawashawishi na kuwaonesha jinsi ubunifu wako unavyoweza kuwaingizia mabilioni, wakikubali kuwekeza hapo ndipo utaajiri wataalamu mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu wa "quality control" na hao ndio watakao hakikisha unatengeneza bidhaa zenye ubora.
kazi ya serikali itakua ni kuhakiki ubora wa hizo bidhaa na kukusanya kodi tu!
tuache tabia za kijamaa kulilia serikali kila kitu ni mentality ya kipuuzi kabisa.
Nadhani Tanzania kwa sasa ni nchi ya mlengo wa Kati so Ujamaa bado upo,unaposema nchi za wenzetu unaongelea nchi za kibepari na ambazo tayari zimeshaendelea sana kiuchumi.
Kazi ya serikali sio tu kukusanya kodi na kuhakiki ubora wa bidhaa Bali ni kuhakikisha inaweka mazingira bora kwa ajili ya maendeleo ya taifa kiuchumi, kiteknolojia na kijamii.
Sapoti kutoka serikalini sio huruma Bali ni wajibu wa serikali kuwasapoti wananchi hasa kwenye maendeleo
 
Back
Top Bottom