Nimeshakata tamaa ya maisha nimepanga kujiua ( mawazo yangu ni kujiua 100%)

B

Bigcat

Member
Joined
Aug 10, 2019
Messages
11
Points
45
B

Bigcat

Member
Joined Aug 10, 2019
11 45
anaetaka kujiua ameandika uzi


Hhhhhhhhh

Bro
acha utani na maisha
Ikiwa ww ni Mwanaume,pambana
Tokea zamani
Mwanaume yake ni mateso
POLENI NA MAJUKUMU ( ee, MUNGU nisaidie)

Mimi ni kijana ambaye utoto wangu nimeishi maisha ya uyatima nasema hivi kwa kuwa tangu nizaliwe sijawahi kumwona mama wala sijui baba yangu anafananaje maana naambiwa mama alifariki nikiwa na umri wa miezi mitatu na baba hapo hapo akaniacha nikiwa na umri huo hivyo nimelelewa na bibi mzaa mama hadi kufikia umri wa kwenda shule ambapo hapo nimelelewa na baba mdogo kutoka darasa la kwanza

Baba mzazi sijawahi kumuona ila niliona maiti yake nikiwa darasa la tatu ambayo yalisafirishwa kutoka huko alikokuwa akiishi
Maisha yangu yamekuwa ya mateso muda WOTE hakuna siku nimewahi kupata raha au faraja katika maisha yangu nimeteseka sana ,nimefanya kazi kama mtumwa ,nimelala sana na njaa ( kulala siku mbili,au tatu bila kula sio jambo la kushangaza imekuwa kawaida yangu

Niseme wazi licha ya baba mdogo kuwa na hali ngumu ya maisha lakini kanisaidia kusoma hadi chuo cha UALIMU ngazi ya cheti (UALIMU shule za msingi) sina budi kumshukuru japo michango mingi na ada za shule nimelipiwa na tasisi mbalimbali hivyo yeye alikuwa mlezi wangu japo alikuwa akinipa na hela ndogo ndogo za matumizi licha ya kuwa anawatoto wake na hali ngumu ya maisha

Baada ya kumaliza chuo cha UALIMU mwaka 2015 nikaona kama ndo ukombozi wangu maana miezi na siku yoyote nitaajiriwa lakini mpaka Leo sijapata ajira ,nimefanya vibarua na kago mtaani làkini kila ninachokipata hakijawahi fanikisha malengo yangu kabisa kabisa nimeishia kukopwa na jamaa,marafiki na ndugu lakini ubaya wake hawajawai nirejeshea pesa zangu nimekuwa ni mtu wa kufanya bidii na kuhangaika huku na huku hakuna siku nimepata faraja katika maisha yangu

Kumbuka hapa nilipo siwezi kurudi kwa baba mlezi kwa maana umri wake umeenda na hajiwezi tena na Mimi nimekuwa nikijitahidi kumkumbuka kwa kadri ya kidogo nachopata lakini kadri siku zinavyoenda ndo hali yangu inazidi kuwa mbaya zaidi,

Nipo kwenye matatizo na majaribu mazito hapa nilipo sijala chochote toka juzi na macho yamevimba kutokana na kulia muda wote usingizi hamna kabisakabisa na nimeishiwa chakari kabisa hapa nimebakiwa na mia sita kwa ajiri ya kununulia sumu tu

Hali yangu ya maisha imekuwa ngumu mno na nilijaribu kuomba ushauri kwa baadhi ya watu wakaniambia nyota yako imechafuka hivyo unapaswa uende kwa wataalamu wasafishe nyota Leo Nina miezi kadhaa tangu niende huko sijapata hata tone la fanikio nimeishia kutoa pesa zangu nilizotafuta kwa jasho jingi


Nimehangaika sana nimehangaika mno sina namna ya kujikwamua sioni upenyo wowote yaani mbele sioni kabisakabisa ninaowadai wamenifungia simu zao na kuniblock mungu wape maisha mema unajua kujitoa kwangu kulikuwaje mpaka Leo nawaza hivi najua ni mapenzi yako ee mungu

Hii hali ilivyozidi kuwa mbaya siku hadi siku kule kijijini kulikuwa na mashamba ambayo walikuwa wakilima na kuyatumia wazazi wangu hivyo baada ya wao kutangulia mbele za haki baba mlezi kanipatia hayo mashamba NA kaniambia wazi kuwa niyauze ili nipate pa kuanzia lakini baada ya kuuza hayo mashamba ndo nimezidi kuumia kwa zaidi ya Mara mia zaidi

Pesa iliyopatikana niliamua kufanya ufugaji wa kuku lakini katika vifaranga 150 nilivyoanza navyo vilikufa na kubaki 11 tu na baadae vimefikia umri wa kutaga vikafa tena vikabaki 5 tu ambavyo niliamua kuuza kwa bei ya hasara

Nimefanya mengi bila mafanikio
Nimejiunga na shirika moja la ujasiriamali la utengenezaji bidhaa za viwandani lakini baadae likafungiwa maana lilikuwa halina usajiri kila nachogusa ndo kinaniumiza zaidi

Pesa niliyokuwa nimetunza sehemu iliyobaki baada ya kuuza mashamba kuna mtu kanishauri kuwekeza katika forex MUNGU WE MUNGU WE EEE MUNGU (MJINGA MM)

Jamani MUNGU nimekosa nini mm mbona kila jambo nalogusa sifanikiwi kibaya zaidi unaniacha nahangaika na kulala na njaa siku zote hizi mbona nikipata huwa nasaidia kila aliyeniomba msaada kwanini mm nipo hivi EE MUNGU NIMEKOSA NINI MM?

jamani nateseka sina cha kutegemea tena hali yangu imezorota sana nimekonda hakuna mfano, uso mzito maana Nina siku mbili ndani nimelala tu nashindia kulia tu sijala Leo naenda siku ya tatu

Jamani nimeingia huko forex nimeliwa kila kitu,TV na sabufa nimeuza kitanda nimeuza,simu nayo nataka niuze kwa ajiri ya nauli navyoenda kunywa sumu maana nimepanga kunywea mbali na meneo haya tena mtoni ili kupoteza ushahidi


Nimeshakata tamaa kabisakabisa naomba naomba kwa mwenye msaada wa mawazo yoyote ya kuninusuru maisha yangu anisaidie ,pia kama kuna mtu yeyote mwenye kuweza kunisaidia kupata ajira huko serikalini nisaidieni maana kama vyeti ninavyo na nimetuma maombi ya ajira Mara kadhaa serikalini bila mafanikio

Nisaidieni jamani nisaidieni jamani

Hapa chini utaona screenshot ya trade nilizounguza katika mfumo wa dolaNaombeni msaada wa hali NA Mali nisaidieni nisipoteze roho yangu kwa njaa ama kujiua

Naombeni msaada wenu nisaidieni mm msaada wenu tafadhali nipatiwe msaada
Wa mawazo
Au nipate ajira serikalini
Msaada hata pesa nitashukuru zaidi


AhsantePia nimeambatanisha barua niliyoandikiwa na kijiji kipindi naenda chuo kama uthibitisho


Nimeandika ukweli mtupu japo tabu na mateso mengi niliyopitia sijaandika ila utayeguswa kwa namna yoyote ile nitashukuru kwa msaada wakoView attachment 1180631View attachment 1180647
 
GEMO

GEMO

Senior Member
Joined
May 5, 2016
Messages
197
Points
250
GEMO

GEMO

Senior Member
Joined May 5, 2016
197 250
Hey wala usijiue.. mm yalinikuta hayo.. nilipoteza pesa forex 6000$ tena ya kuazima kwa watu tofauti karibu 20. Nilikaa ndan zaid ya 2 years .. sina kitu ...
But always God give second chance .. and other side of life...
Kama kufa , kupo tu subiri kikukute chenyewe ila si wewe kujiua..
Dont kill yourself
Pole sana mkuu....
 
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
12,969
Points
2,000
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
12,969 2,000
Hahaha
FOREX FOREX FOREX INATAKA KUTOA ROHO YA MTU..... ONTARIO utawaambia nini watu jamaa akijiua?


ila nini mkuu... KUJIUA SIO SULUHISHO, KUNA MAISHA MAZURI YANAKUSUBIRI MBELE, UNAPOKATA TAMAA UNAFELI SANA.

NAAMINI WATU WATAKUJA KUKUSAIDIA...MUNGU ANAONA KILIO CHAKO.
 
Marianah

Marianah

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
5,012
Points
2,000
Marianah

Marianah

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
5,012 2,000
Nilitaka niulize hivi hivi na nimetafuta labda kuna mtu mwingine atakuwa ameuliza hivi kwenye comments sijamuona hata mmoja naona watu wengi walivyomaliza tu kusoma uzi wakaanza kucomment

Hawajajihangaisha hata kuangalia hizo screenshots hebu naomba mimi na wewe tusaidiane kushangaa hapa screenshots zikatoe hadi muonekano wa simu nzima kweli? Anyway labda mimi ndiyo mshamba!
Izo screenshoot zina toa adi body la simu yote .. noma sana
 
nankotima

nankotima

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2013
Messages
559
Points
500
nankotima

nankotima

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2013
559 500
Yani we jamaa kufa unaona kama dili hivi. Ili nilichogundua kuishi unataka na ndo mana umeandika bonge la post halafu unasubiri mpaka usome comments zote sijui ndo ufe vizuri? Halafu eti unataka ushauri tena. Ushauri wangu endelea kupambana mpaka tone la mwisho la damu yako. Hutakiwi kujiua halafu wewe unamaisha mazuri sema tu unataka kupata kwa haraka. Waangalre walro chini yako utajifunza kitu,epuka kuwatazama walio kuzidi kipato. Amini usiamini kwa maisha hayo wapo uliowazidi kipato na ndo mana una mia sita mfukoni hela ambayo unataka ukanunulie sumu. Hiyo hela kanunue unga nusu usonge uji unywe upate nguvu ya kufikiri vitu vilivyokuwa sawasawa.
 

Forum statistics

Threads 1,324,983
Members 508,911
Posts 32,179,522
Top