Nimeshaelimisha jamii sana hapa JF ngoja Leo nijisifu,ofcoz ukiweza kuwa neutral kama Mimi jisifu

Kwetu Musoma.

Nimesoma na kuishi Bukoba miaka 3.

Nimekaa na kufanya kazi Kilimanjaro.

Nimeshaembea sana na kuzunguka hii nchi ingawa ndio kwanza nina miaka 32.

Ninachotaka kukwambia Wahaya na Wachagga walikiwa zamani. Na hii ni kwasbabu za kiutamaduni tu.

Sasa hivi hakuna kabila lenye maajabu yoyote. Siku hizi hata MMASAI anajua nini anataka, anaijua PESA na ELIMU.

Tena vijana wengi huko Uhayani na Uchaggani zimebaki SIFA tu za wazee wao, wao hakuna cha maana wanafanya.

Narudia tena.

Sasa hivi hakuna mjinga.

Ukileta UBAGUZI wewe jiandae na MATOKEO ya ubaguzi.

Ni TIT FOR TAT.
 
Kuna kakijana kameniuliza mwaka 2016 masaki palikuwa na viwanja? Naomba kumjibu kwamba hata Leo viwanja vipo ni pesa Yako tu? Hata kariakoo viwanja vipo wewe TU useme unatamani kubadiliasha kilicho juu ya ardhi uweke Nini..Sijui unanielewa?

Kuna anayesema alisikia nimekufa, Nadhani ukifa uwezi kuandika Ila ukiugua unaweza kuacha wosia. Sijui nimeeleweka

Kuna amesema nimewapiga wagogo madongo, hapana nataka kusema nikiwa Waziri nitamtumikia mwananchi na nikiwa spika ntamtumikia mwananchi sutatamani kukaa nyuma ya mkuu wa nchi masaa 24 ,kazi zangu nitafanya muda gani.

Dhima ya Uzi huu nikuanzisha kampeni ya TUKATEMBEE NJE TUJIONEE MAENDELEO YALIPO, ITATUSAIDIA KUACHA KUSHANGILIA DARAJA LA UBUNGO NA TAZARA KWENYE VYOMBO VYA HABARI,UKIELIMIKA UKATAMBUA DUNIANI MIUNDOMBINU IPO VIPI UTAONA HAYA KAMA MADARAJA TU NA UTOTHUBUTU KUTAMKA KWA KIINGEREZA.

JUZI NIMESIKIA KUNA DARAJA HUKO KIJIJI MBEZI LUIS NIKASHTUKA, KWAMBA WAKATI WANAJENGA BARABARA DARAJA HATUKULIONA? WAKANDARASI NA WATU WA TANROADS KATEMBEENI DUNIANI MWACHE KUTUTIA HASARA NA AIBU.
Nia yako ni nzuri sana lakn itapendeza zaidi ukitumia uzoefu wako kuelezea yafuatayo?

1.Njia zipi za kufika ulaya na USA maana siyo mchezo kupata viza.

2.fursa zipi za kufanya baada ya kufika ulaya na USA?
 
Umezungumza mambo mengi sana sijui niegemee wapi, lakini yote kwa yote asante kwa changamoto ulioyupa vijana, maybe tunaweza kuthubutu kufanya kitu mwisho wa siku tukapata lugha bora ya kuzungumza kuliko sasa.
 
Lakini pia nilichogundua sera za ujamaa zilifanya vijana wa Tanzania wawe waoga wa kusafiri maana duniani utawakuta wa Nigeria, wakenya, waghana, wasouth Africa, Waganda, Wacongo, tena Warundi na Wanyarwanda ni wengi nje kuliko sisi wabongo nadhani uoga unachangia maana mtu mwenye akili timamu graduate huwezi kukaa miaka mitano unatafuta ajira na ajira haupati utegemee uko sawa sawa hapana hapana, kujiongeza kusoma nursing sawa kuna wanaojiongeza kwenda kwenye majeshi zote ni hustle tu ukithubutu.
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Mpaka hapo ninegundua hukuolewa ila umezalishwa tuu.
Sory kama nimekuudhi maana hapo mambo ya ndani (kuolewa ndoa)hujagusia kabisa
 
Yaani umewaponda wagogo wakati wenzio wametembea hadi Galilaya na kumuona yesu na mkewe.

Anyway huko nimekupa teuzi kuwa waziri mmoja wapo ndani ya JF
 
Mpaka hapo ninegundua hukuolewa ila umezalishwa tuu.
Sory kama nimekuudhi maana hapo mambo ya ndani (kuolewa ndoa)hujagusia kabisa
Naomba kukumbisha maneno yafuatayo: usikubali katika maisha Yako kulala na kutamka na mkeo au mmeo, jitahidi sana kuamini kwamba ngono(sex) inaweza kusubiri Kwa muda flani na kama ni usaliti upo hata mngeishi nyumba Moja.

Nataka unielewe hivi, ndoa zilizojengwa kwenye sex zinadumaza MAENDELEO na fikra chanya; ndoa zinazojengwa kwenye uaminifu uondoa wivu nakufuatiliana hivyo mwenzi wako atakuamini ukiwa karibu au ukienda mbali naye.

Nina ndoa Tena siyo ndoa yakuachika Leo nakurudiana kesho ni ndoa strong ambayo watoto wangu hawajawahi kusikia nikigombana na baba yao Wala haijawahi kutokea wakajifili wapweke Kwa umbali uliopo baina yetu wawili.

Mme wangu amefanya kazi kwenye mashirika ya meli chungu nzima Duniani ,ofcoz siyo Mbongo hivyo tumeishi hivyo kabla ya WhatsApp na hata Sasa kipindi Cha WhatsApp.

Ndo isikwamishe safari zako kijana, hata unapokwenda kazini mkeo kama ni mzinzi atazini tu. Tukubaliane kwamba exposure ni pamoja na uwezo wakuondoa fikra za kusalitiwa, ukimganda mkeo au mmeo kama hakuzaliwa na fikra pevu zakutambua thamani ya ndoa, kutambua Kuna gono, kutambua kuna HIV na kutambua kuchepuka kunaweza vunja ndoa basi wewe ujaoa/kuolewa Bali unaishi utumwani na wewe kampeni ya TWENDE TUKATEMBEE HAIKUHUSU.
 
Huyu mutu anajua kuandika kwa kupangilia nkiona uzi wake sipiti bila kuusoma! Ngoja nkasake passport kwanza
 
Beatrice kumbe umeolewa na Mzungu! Bojoooo waiyukayo....
 
tunaangaika kujadili udini wakati wenzetu wanaacha hata kwenda nyumba za ibada baada ya kutambua Dini sahihi haipo kanisani wala msikitini, Dini ni maisha binafsi ya mtu ambayo yakiwapendeza wanadamu yamempendeza MUNGU na yakimchukuza Mwanadamu yamemchukiza MUNGU; ndipo inapozaliwa dhana kwamba ametuumba kwa mfano wake.
Wenzetu gani wanaacha kwenda Misikitini?
 
Naitwa mwana wa Kamugisha, mzaliwa wa Bugandika nakukulia mtaa wa Pepsi Bukoba Town. Nikawa Mwalimu weee but no mafanikio. Nikaenda chuo kikuu kuongeza maarifa( SI unajua mhaya asifiwi wingi wa Mali anasifiwa Kwa ukubwa wa CV) nakufanikiwa kupata lower second in short sikuwahi kuwa na akili sana ila nikifanya mtihani nafaulu.

Miaka 1990 nikaenda kusoma diploma ya Nursing huko USA Ili nipate kujishikiza nitafute kuelewa Dunia inakwendaje. Usishangae wapo Mawaziri na wakuu wa mikoa sijui makatibu wakuu awajawahi kusafiri nje, Mimi siyo Kwamba nimesafiri Bali nimekaa Ulaya na Amerika. Nipigieni makofi.

Nimekaa huko weee but finally nikarejea Tanzania mwaka 2009 na kukaa Kidogo Kisha nikaenda kusoma ramani Ulaya. Ulaya nikagundua namna binadamu anavyobaguliwa kwa rangi, nikaelewa Kwamba wanachofanya wahaya waliowengi ni ubaguzi uleule wa Ulaya ila unafanywa Afrika. Ukitaka usibaghiliwe some tafuta pesa zunguka Dunia, wakikuuliza unapajua Newyork waambie mwaka 1996 nilipita Dubai kuelekea Afghanstani Kisha china nakuzungukia Dell kabla sijatinga Harizona kuangalia soko la bidhaa za asili. Mhaya unamziba mdomo

Tuachane na wahaya tuendelee, mwaka 2016 nikarejea home na umri nao ukawa umesonga ila nashukuru nilifanikiwa kujenga kibanda Bukoba na Masaki .So nikawa naishi Masaki na Bukoba go and return. Fedha ya kulisha Tumbo langu zipo so haba na uzuri Sina Mtoto Wala mjukuu anayenitegemea na Hii inatokana na ukweli Kwamba niliishi Marekani kwa malengo, familia yangu yote inajitegemea na nimshukuru MUNGU Kwamba alinifungua akili pamoja na kuwa na degree lakini akaniambia usife maskini jishushe kasome nursing upate nafasi ya kusomesha wanao elimu Bora na nzuri kuliko kukaa bongo ambapo hata madarasa Bado kukamilika kujengwa.

Nini nataka kusema, Kwa kipindi chote ambacho nimekaa hapa nchini nimegundua tunakwenda kutawaliwa siku si nyingi. Tunakwenda kutawaliwa Kwa sababu wapo viongozi wanaoamini Kwamba Dunia ipo imesimama ikisubiri tuelimike itubebe. No. Dunia inakwenda Kasi sana, wenye fedha na maarifa wapo njiani kuelekea mwezini sisi tunabishana kukopa au tusikope, tunabishana Uchaguzi 2025 bila kujua tutakuwa hai au tutakuwa kaburini, tunajisifu kujenga madarasa bila kujua wenzetu wanaangaika kwenda mwezini, tunaangaika kujadili udini wakati wenzetu wanaacha hata kwenda nyumba za ibada baada ya kutambua Dini sahihi haipo kanisani wala msikitini, Dini ni maisha binafsi ya mtu ambayo yakiwapendeza wanadamu yamempendeza MUNGU na yakimchukuza Mwanadamu yamemchukiza MUNGU; ndipo inapozaliwa dhana kwamba ametuumba kwa mfano wake.

Niwaombe Watanzania hasa vijana tokeni mkasake maisha nje ya mipaka Hii, tokeni mkasake maisha Ili wakitaka kuteua basi waone CV zenu huko kwenye mashirika makubwa Duniani. Tokeni mwache roho mbaya yakusema mbona wanaoteuliwa ni wahaya na Wachaga TU? Hakuna namna utafundisha mzizima ukajulikana Duniani,tembea. Ntatoa mfano wa makabila yaliyofanikiwa na ambayo hayatawaliki kirahisi na utagundua huko ndipo upinzani hata wa Kisiasa ulipo.

Tanzania Ina makabila mengi yaliyowekeza kulalamika kuhusu tatizo la ajira nchini na watasubiri watawala wawapige siasa mwisho watawatawala na ndicho kilichotokea kwenye Baraza jipya la Mawaziri Kwamba wamedhamiria kututawala. Lakini makabila yafutayo Wahaya, Wachaga, Wanyakyusa, Wameru, Wapare, Waha, Wamasai wakurya, wajaluo na Wapemba ni vigumu kwa umoja wao kulalamika ajira au kusubiri kutawaliwa maana walianza kujitawala miaka mingi. Mfano mzuri ukisoma historia unabaini Watu wa Kaskazini wakiongozwa na Mzee Japhet Crylo waliweza kuuza kahawa wakamtuma Mzee huyu wa Kimeru akawaombee Uhuru kabla hata ya Mwalimu nyerere. Tunalalamika wakina mtei n Msuya kujenga Barbara kwao , tunalalamika wakina na Waha kumiliki biashara nchini tukiwasingizia wachawi lakini ukweli nikwamba Hawa Watu wameachana na kuajiriwa . Maana yake Hawa Watu wanazo akili za kujitawala kabla hata hatujapata Uhuru na wameshatambua umuhimu wa kujiandaa wasitawaliwe. Wachaga wamesambaa Duniani na JPM alishindwa kupambana nao Kwa sababu wapo Kila familia nchini na nje ya nchi. Sisi wahaya na makabila mengine ya mpakani tumesafiri nje na tunaelewa Dunia inakwenda wapi. Hivyo ni muda Sasa wakukubali kwamba familia zetu zitoe wawakilishi waende wakaishi Duniani , tutoe wawakilishi watupunguzie tatizo la ajira nchini, tutoa wawakilishi waende nje wakatuletee remittance. Wahaya tumechoka kukutana huko ulaya wenyewe Kwa wenyewe tunatamani na wagogo nao wakatembee ulaya wajifunze kuwa na misimamo na waache maisha yakujipendekeza hadi uchokwe.

Tusipokubali kutoka tukaamini katika sera ya JPM ya Tanzania ni tajiri ipo siku tutadanganywa na udongo wa mwezini tukauza rasilimali zetu. Hivi mnajua kwanini mikataba inakwenda kusainiwa nje, unajua kwanini Ndugai alitandikiwa red carpet china akazungukwa na wachina wakimpa huduma zaidi ya RAIS, ni kwa sababu walitaka kupitia Bunge wauziwe bandari ya Bagamoyo na alirejea akasifia kama limbukeni. Tunatakiwa tuwe na Mawaziri na makatibu wakuu waliotoka Duniani siyo waliotolewa jalalani. Tunataka Wabunge waliopita angalao nchi kadhaa siyo Watu wanajisifia kwamba wanaishi Dar wakitokea Mikoani. Mbunge kama Waitara anaishi Gongo la Mboto sijui Chanika atawaza sawasawa kuhusu biashara za Kimataifa? Tukubali kwamba ni muda Sasa wa kusambaa Kama tunataka kuwadhibiti watawala wasiuze nchi.

Nimetumia ukongwe wangu hapa JF kuwahimiza mtoke mkatafute Rizick, tunataka kuwa na Watu wenye Upeo wa akina Masele ambaye anaweza kupingana na spika huko South Kwa hoja Hadi spika akatumia wasio na akili bongo kumnyamazisha Kwa kivuli Cha utovu wa nidhamu. Tunataka vijana kama akina Nasari ambao pamoja na kupokwa fursa hawakukubali kubaki hapa walikwenda kwa Obama, tunataka wasomi kama akina Mhongo ambapo walipotumbuliwa walikwenda kupiga lecture south, tunataka vijana kama akina Lema ambao baada yakuona maisha yao yapo hatarini na wanapambana na wauaji waliamua kwenda nje, tunataka hoja zenye exposure kama za Lisu, tunataka wawekezaji kama MBOWE ambaye anarasimali Dubai sijui South ili kesho tukikwama huko tuwe na ndugu wakutupokea.

Tuachane na ushamba wakuiba

….wanatumia tweeter kutupa update za fursa za elimu na kazi.
Kweli wewe mhaya!!!!! Baadala ya kufikiria biashara unawaza kazi!!!! Bure kabisa
Kweli wewe mhaya kweli
 
Naomba kukumbisha maneno yafuatayo: usikubali katika maisha Yako kulala na kutamka na mkeo au mmeo, jitahidi sana kuamini kwamba ngono(sex) inaweza kusubiri Kwa muda flani na kama ni usaliti upo hata mngeishi nyumba Moja.

Nataka unielewe hivi, ndoa zilizojengwa kwenye sex zinadumaza MAENDELEO na fikra chanya; ndoa zinazojengwa kwenye uaminifu uondoa wivu nakufuatiliana hivyo mwenzi wako atakuamini ukiwa karibu au ukienda mbali naye.

Nina ndoa Tena siyo ndoa yakuachika Leo nakurudiana kesho ni ndoa strong ambayo watoto wangu hawajawahi kusikia nikigombana na baba yao Wala haijawahi kutokea wakajifili wapweke Kwa umbali uliopo baina yetu wawili.

Mme wangu amefanya kazi kwenye mashirika ya meli chungu nzima Duniani ,ofcoz siyo Mbongo hivyo tumeishi hivyo kabla ya WhatsApp na hata Sasa kipindi Cha WhatsApp.

Ndo isikwamishe safari zako kijana, hata unapokwenda kazini mkeo kama ni mzinzi atazini tu. Tukubaliane kwamba exposure ni pamoja na uwezo wakuondoa fikra za kusalitiwa, ukimganda mkeo au mmeo kama hakuzaliwa na fikra pevu zakutambua thamani ya ndoa, kutambua Kuna gono, kutambua kuna HIV na kutambua kuchepuka kunaweza vunja ndoa basi wewe ujaoa/kuolewa Bali unaishi utumwani na wewe kampeni ya TWENDE TUKATEMBEE HAIKUHUSU.
Amen.
Umejibu ka msisitizo sana na nilichowaza ndio mle mle asnte kwa kuja.kila la heri
 
Huu ni Uzi wangu Bora Sana kwa mwaka huu. Asante sana umeandika masuala fikirishi sana.

Endelea kushusha nondo mkuu,
 
Lakini pia nilichogundua sera za ujamaa zilifanya vijana wa Tanzania wawe waoga wa kusafiri maana duniani utawakuta wa Nigeria, wakenya, waghana, wasouth Africa, Waganda, Wacongo, tena Warundi na Wanyarwanda ni wengi nje kuliko sisi wabongo nadhani uoga unachangia maana mtu mwenye akili timamu graduate huwezi kukaa miaka mitano unatafuta ajira na ajira haupati utegemee uko sawa sawa hapana hapana, kujiongeza kusoma nursing sawa kuna wanaojiongeza kwenda kwenye majeshi zote ni hustle tu ukithubutu.
Wala tatizo siyo sera za ujamaa. Ukweli ni kwamba Tanzania maisha siyo magumu saana kiasi hicho cha kumfanya mtu mpaka akimbie.

Tanzania unaweza kupanda gari ukaenda hata Songea huko na hakuna mtu unamjua lakini ukala na kulala kwa kusaidiwa tu Na watu.

Ila huwezi kukuta kitu kama hicho Kenya, Ethiopia n.k.

Na nchi nyingi zenye wahamiaji wengi nje lazima ni zile nchi zenye MACHAFUKO kama Somalia, Congo, Ethiopia au nchi zenye maisha magumu sana kama Zimbabwe, India, Nigeria, Kenya n.k.

Tanzania mtu akitoka amependa tu kwenda kutafuta na wengi wakifikaga huko maisha yanawashinda maana Bongo ni tambarare sana.
 
Back
Top Bottom