Nimesalitiwa ila nashindwa kumuacha. Je, nimuoe?

MoonBoy

Senior Member
Jul 15, 2016
195
133
Naombeni ushauri ndugu zangu, acheni kunicheka au kunikejeli, nitawashukuru sana

Tukizungumzia swala upendo, Kiukweli sijui namna ya kupenda ipoje,

Ni miaka minne ya mahusiano ya mbali, yaani mkoa hadi mkoa. Kiukweli nampenda na pia ananipenda sana. Haikuwa rahisi kuonana kwetu, lakini mwaka jana mwishoni niliweza kwenda mkoani kwao kwa nia ya kulipa kila kitu niweze kuondoka nae. Lakini jambo la kushangaza, nilimkuta ana mtoto mdogo kuliko mahusiano yetu.. Ni dhahiri kuwa nilisalitiwa, iliniuma sana, ukilinganisha ndie mwanamke wa pekee katika moyo wangu,

Kiukweli ilikua ni ngumu kumtoa moyoni kwa haraka, nilishindwa kumuacha kabisa, ishu ni kwamba ni mwanamke aliekubali kuendana na maisha yangu. Na pia amejutia kwa kitendo cha kunisaliti na kupata mtoto ndani ya mahusiano yetu, Kiukweli amejutia sana. Na amekubali kumuacha mtoto wake wa miezi 10 na kuja kuishi namimi.

Mwezi wa jana aliweza kutoroka toka mkoani kwao na kuja mkoani kwangu. Ila nilimrudisha kwao nikimtaka asubiri nimfuate.

Sasa nawaza sana, nimuoe yeye au nifanyeje, mana kuna wakati nawaza sana.. Hivi wanawake wameisha mpaka nioe mwanamke alie nisaliti...

Naombeni ushauri wenu. Kiukweli nashindwa kumuacha ila napata mawazo kuhusu usaliti alio ufanya... Nipeni ushauri wenu tafadhali
 
Yusufu baada ya kugundua kua mchumba wake Mariam ni mjamzito akakata shauri amwache kabisa..lakini baadae alibadili maamuzi baada ya kujua haukua ujauzito wa kawaida..! Sasa mkuu huyo mchumba wako alijazwa ujauzito hilo hukugundua kabisa..then mpaka akajifungua hukugundua..mpaka umekuja kusituka ana mtoto..!!! Anyway huyo hakufai kabisa..hata kama ukimuoa hamtaishi kwa amani..bado utakua na kinyongo tena sana..!
 
Kweli kabisa kaka, hicho kinyongo ninacho mpaka sasa.... Aisee yani nina kinyongo afu nampenda saa zingine, yaani sielewi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa kaka, hicho kinyongo ninacho mpaka sasa.... Aisee yani nina kinyongo afu nampenda saa zingine, yaani sielewi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbna u mtu mzima af unamapenzi ya kitoto kwani umegundishwa kwake???,we uyo mwanamke alishindwa kujiheshimu mpk akapata mtoto unazani anakupenda?? Na uyo kakubali ndoa sababu ana pa kukimbilia saiv Ila mambo yakianza kuwa Safi mbna ataliwa sana na atakuzalia vitoto vingi nje ya ndoa.
NB; biblia inasema usimwache mke wako Kwa sababu yyte Ile kasoro uzinzi/uhasherati.
KUPANGA NI KUCHAGUA.
 
Back
Top Bottom