**Nimesalimu - Mikono Juu**Siwezi kumudu Kasi ya JF: Kuna Mwenye Mawazo Tofauti**

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,138
82
Wana JF,

Mimi nimekuwa mwanachama hapa JF kwa miaka...lakini kwa kipindi hiki cha sasa mambo yamebadilika kwa kasi kiasi kwamba napitwa na mijadala mingi.

Naombeni tupeane mbinu za kuwa "On Top" hapa jamvini kwenye mijadala mbali mbali; natumai wengi wetu humu ni watu wenye shughuli zao kama mimi ambao pia muda wao ni mdogo. Sasa hebu tumegeane mbinu mbadala.

Yeyote mwenye kuona kuwa mbinu zake ni nyeti basi tafadhali nitumie kwenye ujumbe binafsi.

Nia yangu ni kujua wenzangu mnafanyaje ili kwenda sambamba na hii kasi mpya...kama wapo wengine wengi wenye tatizo kama la kwangu basi huenda wakati umefika wa kubadili namna ambavyo topic zinabandikwa na kuchangiwa.

Ni vizuri kama habari inawekwa hapa basi ifikie walengwa wote kwa nafasi zao ili matunda yapatikane kikamilifu. Nikiwa na maana kuwa yeyote aliyejindikisha hapa forum asiachwe nyuma katika mapambano haya ya fikra kwa sababu zinazoweza kuepukika.

Safari ni ndefu, pamoja tutafika.

Naombeni mawazo.
 
Yebo I feel you.

Muda si mrefu nimeposti article kumbe tayari washashi washaiposti.

Kuna watu wanatembea na vimondo mikononi kutwa wanabofya, ndiyo siri ya uzuri.
 
I am with you Yebo Yebo on this one.

Mfano tu; I was gone for three and a half days, as of this morning, sijui nisome(na ni kusoma tu) kwa kuanzia wapi, na mpaka sasa sijasikiliza the new CD; I am not sure I can keep up with news at the speed I want anymore. I, too, could use some useful tips...
 
Ni kweli umekuwa adimu kipande hii.

Japo sijakuelewa iwapo unamaanisha kuwa UNAKOSA baadhi ya mijadala au uwezo wako wa kuposti mada unakwazwa na majukumu mengine,binafsi ninajitahidi kutembelea JF kila baada ya muda mfupi ninapokuwa na laptop yangu au wakati mwingine huwa nacheki kama kuna jipya kupitia kwenye mobile device yangu.

Pia njia nyingine inayonisaidia kujua maendeleo kwenye forums ni kwa ku-subscribe feeds za JF.

Hata hivyo,yote yanategemea ratiba na access to the web.
 
Wana JF,

Nikiwa na maana kuwa yeyote aliyejindikisha hapa forum asiachwe nyuma katika mapambano haya ya fikra kwa sababu zinazoweza kuepukika. [/I][/COLOR]

Safari ni ndefu, pamoja tutafika.

Naombeni mawazo.
Usinilazimishe kuwa katika hayo mapambano yasio na mwanzo wala mwisho
 
Wana JF,

Mimi nimekuwa mwanachama hapa JF kwa miaka...lakini kwa kipindi hiki cha sasa mambo yamebadilika kwa kasi kiasi kwamba napitwa na mijadala mingi.

Naombeni tupeane mbinu za kuwa "On Top" hapa jamvini kwenye mijadala mbali mbali; natumai wengi wetu humu ni watu wenye shughuli zao kama mimi ambao pia muda wao ni mdogo. Sasa hebu tumegeane mbinu mbadala.

Yeyote mwenye kuona kuwa mbinu zake ni nyeti basi tafadhali nitumie kwenye ujumbe binafsi.

Nia yangu ni kujua wenzangu mnafanyaje ili kwenda sambamba na hii kasi mpya...kama wapo wengine wengi wenye tatizo kama la kwangu basi huenda wakati umefika wa kubadili namna ambavyo topic zinabandikwa na kuchangiwa.

Ni vizuri kama habari inawekwa hapa basi ifikie walengwa wote kwa nafasi zao ili matunda yapatikane kikamilifu. Nikiwa na maana kuwa yeyote aliyejindikisha hapa forum asiachwe nyuma katika mapambano haya ya fikra kwa sababu zinazoweza kuepukika.

Safari ni ndefu, pamoja tutafika.

Naombeni mawazo.

Ukumbi wenye wanachama 4,300 si rahisi kuwa on top of everything. Jitahidi lakini labda atatokea mwanaJF akupe mikakati ambayo inaweza kukusaidia
 
Ni kweli umekuwa adimu kipande hii.

Japo sijakuelewa iwapo unamaanisha kuwa UNAKOSA baadhi ya mijadala au uwezo wako wa kuposti mada unakwazwa na majukumu mengine,binafsi ninajitahidi kutembelea JF kila baada ya muda mfupi ninapokuwa na laptop yangu au wakati mwingine huwa nacheki kama kuna jipya kupitia kwenye mobile device yangu.

Pia njia nyingine inayonisaidia kujua maendeleo kwenye forums ni kwa ku-subscribe feeds za JF.

Hata hivyo,yote yanategemea ratiba na access to the web.

Bila shaka hizi ndizo baadhi ya njia zinazotuwezesha wengine, si kumudu; bali kuwa angalau karibu na matukio. Haiwezekani kabisa kuwa 'upto date' na kila kitu kilichomo JF. Wengine tuliamua maksudi kabisa ku-narrow our preferences. Kwa hiyo, huwezi kwa mfano kutuona kule kwa ndugu yetu BRAZAMENI na kwingineko.

Hata hapa kwenye jamvi hili, mengine tunayapisha yapite bila kuyagusa.

TAHADHARI: Ukitaka kuona kila kitu cha JF, utaacha kulala, kula, na kazi au biashara vitaota miguu.
 
Ni kweli umekuwa adimu kipande hii.

Japo sijakuelewa iwapo unamaanisha kuwa UNAKOSA baadhi ya mijadala au uwezo wako wa kuposti mada unakwazwa na majukumu mengine,binafsi ninajitahidi kutembelea JF kila baada ya muda mfupi ninapokuwa na laptop yangu au wakati mwingine huwa nacheki kama kuna jipya kupitia kwenye mobile device yangu.

Pia njia nyingine inayonisaidia kujua maendeleo kwenye forums ni kwa ku-subscribe feeds za JF.

Hata hivyo,yote yanategemea ratiba na access to the web.

Mijadala imekuwa ikinipita iwapo sijatia macho hapa kwa siku 2..!!

Hilo la ku-subscribe feeds za JF ni geni kwangu; tafadhali fafanua zaidi..nimeangalia kwenye forum lakini bado sijangamua.
 
Yebo I feel you.

Muda si mrefu nimeposti article kumbe tayari washashi washaiposti.

Kuna watu wanatembea na vimondo mikononi kutwa wanabofya, ndiyo siri ya uzuri.

Duh kweli hapa JF kuna watu sijui huwa wanafikiria nini,yaani hiyo quote hapo juu imenichekesha sana mpaka boss kidogo astukie sifanyi kazi,yani hiyo quote imesukuma mbele frustrations zangu za maisha na kunifanya angalau niwe na furaha siku ya leo.Ni kweli ukitaka kuwa uptodate hapa jamvini unaweza kuanza kupewa memo za uzembe kazini,heri yao wenye laptops na private connection au wale ndugu zetu walio huko kijijini...ama kweli JF kuna watu.
 
Yebo Yebo
Hapa JF kama unavyopajua pana mada motomoto ambazo lazima tu zitakuvutia kuchangia. Pia miye nafundisha,wakati mwingine inabidi uondoke tu kwenda darasani bila kupenda.La muhimu ni kuwa update tu ni nini kunaendelea nchi hii,kwani ukitaka kuwa ontop ni ngumu mkubwa,kuna watu wanapost news everytime kwasababu wanatechnologia nzuri mikononi mwao,ukiwa kama mimi mpaka ufike ofisini,lazima ukubali kila unachokipata basi wengine wamekwisha kiona. La muhimu,endelea kupata news toka JF na ikitokea umepata new post basi tuletee
 
Mkuu just narrow ur preferences and be selective.

Kuna thread ukisoma heading tu unajua huu ni udaku and there nothing inside pita juu tu.

Jaribu kuwa na list (yako mwenyewe) ya wachangiaji makini na ofcourse wale akina mwenzangu mie, as u read thread uwe unaruka michango ya "akina sie"

Ukiona unaboreka mtembelee Brazameni kule ataku huisha!
 
Off topic inaenda kwa Masatu.
Mtani wako wa jadi Joseph C Lunyungu yuko wapi mbona muda sasa hatumuoni ama yuko Monduli na Lowasa anamfuatilia ?
 
Ndio demokrasia, kazi ni kwa msomaji kuamua ipi mali na ipi upupu. Lakini udaku mwingine unafurahisha na kuibua mijadala, kama ule wa Membe na EL; http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=10471
 
Off topic inaenda kwa Masatu.
Mtani wako wa jadi Joseph C Lunyungu yuko wapi mbona muda sasa hatumuoni ama yuko Monduli na Lowasa anamfuatilia ?

Tibwilix2 huyu mkuu kapotea kwenye "rada" yangu sijui yuko wapi.

I hope is OK
 
Mtu wa aina yaonyesha mnajuana basi akipotea unamtafuta maana michango yake sasa humu haipo tumeanza kuwa na wasi wasi asije kuwa kaingia kwenye patyroll ya akina Salva
 
Kwi! kwi! kwi! mara ya mwisho alikuwa na tenda ya kutafuta Ma RC na Ma Dc akaweka tangazo kwa wana JF wanaofaa nimempenyezea CV yangu naona kimya mpaka sasa.

Sasa sijui nae "anaandaliwa" kuwa DC walau kule Mvomero....
 
Yebo2

Ndio mambo hayo, kama huwezi kukeep pace unaadimika kidogo. Halafu usisahau baada ya Serikali kuitangaza JF kila member anataka kuonyesha ushuhuda wake.
 
Back
Top Bottom