"Nimesacrifice maisha yangu kwa ajili ya Watanzania masikini" Maneno ya kweli kabisa ya hayati mpendwa Rais Magufuli

Kwahiyo unataka kusema Awamu ya Magufuli Uwezo wetu wa kujitegemea kiviwanda uli-improve?! Nyie watu acheni utani jamani!!!! Sukari bei juu! Mafuta ya kula hayaonekani!! Mauzo ya nje kutoka manufacturing sector yameshuka!! Viwanda vingi uzalishaji umeshuka!! Saruji haishikiki! What exactly alichofanya Magufuli kwenye sector ya viwanda cha kutufanya tutembee kifua mbele? Are you blinded na hizi kauli za Tanzania ya Viwanda?! Kwa viwanda gani hasa?! Hiyo kauli mbiu ina tofauti gani na ile ya Kilimo Kwanza?!

Na nimesema kipindi cha Nyerere nchi ilikuwa dormant kwa sababu kama ulivyosema, Nyerere alijenga viwanda vingi sana! Lakini kama ni mfuatiliaji mzuri wa uchumi wa Tanzania, hadi Mwalimu anaondoka viwanda vingi vilikuwa havizalishi na hata vilivyokuwa operational vilikuwa vinafanya hivyo kwa hasara!!! Man, inawezekana mimi na wewe tulikuwa wadogo au hatujazaliwa lakini uliza watu wakuambie ni namna gani hata dawa ya meno ilionekana ni anasa!! Ni namna gani watu walikuwa wananunua sukari kwa kupanda foleni!!! Sasa kama ktk mazingira hayo nchi haikuwa dormant, man, labda nitafutie a better phrase lakini kwangu naona hiyo ndiyo phrase sahihi hasa! Kwamba, hapo kabla nchi ilikuwa na uhai lakini from late 1970's nchi ikalala kabisa kiuchumi!!!
Kama ulifuatilia kampeni za hii awamu ya pili, JIWE hakuzungumza chochote kuhusu viwanda! Ajenda ya viwanda iliishia ile awamu ya kwanza na ni baada ya JIWE kuona kabisa Bongo hatuwezi kuwa na viwanda bila kwanza kuboresha mambo kadha wa kadha. It's that simple!
 
POROJO AT WORK! Eti "sisi wengine tuliokuwa tunafahamu maskini anavyodharaulika"! Hivi wale aliowaambia juzi juzi kwamba wabaki na mimavi yao nyumbani ni matajiri wale?! Hivi wale aliokuwa anawaambia maneno ya kejeli baada ya kuwa wamekumbwa na tetemeko la ardhi ni matajiri wale? Hivi wale aliowaambia kama hawana 100 wapige mbizi enzi hizo akiwa waziri ni matajiri wale?! Wale waliokuwa wanaokotwa kwenye viroba badala ya kuwafikisha mahakamani ni matajiri wale?!
Kuna wale aliwavunjia Ubungo, alipoenda Mwanza akasema waachwe wasivunjiwe kwa vile walimpigia kura, ina maana wa Dar hawakumpigia?. Kuna walioachishwa kwa vyeti feki na wengine hawakufoji, ila kwa sababu moja au nyingine wakajikuta hawana, Lakini Makonda alifoji kabisa na aliendelea kumuacha. Pia kuna pesa yetu amekufa nayo Bilion 1.2,hakuwahi kutuambia aliifanyia nini na aliichukuaje hazina bila Bunge kujua. Wacha Aende katufanya watu tumekuwa masikini sana
 
Rais wetu alijitoa kweli kwaajili yetu na amepumzika sasa, sio lazima sasa ila soon yan Very soon ninyi mnashangilia mtakuja kutubu na kukiri baada ya kuuzwa!
 
I will always believe that Magufuli's death was not Natural.
Hakika mkuu,, inajulikana hivyo,,

Na hata hiyo kauli ya kutoa sadaka maisha yake kwa wanyonge,,

inamaanisha alijuwa anawindwa na mabeberu pamoja na vibaraka wao.

Ipo clip moja anaelezea alivyowekewa sumu na jinsi baadhi ya mawaziri wake walivyokuwa wakimchukia.

Hiyo ni ndani ya miaka 2 ya utawala wake.

Ilifikia hata kumfata mkapa , magufuli kuomba kujiuzulu.

Nilichokigundua Mimi ktk maisha ni kwamba ,,,

a traitor is always a traitor

an enemy is always an enemy...

Hatokaa kubadilika wala kugeuka nafsi maisha,,

Hata anayemchukia akifa.

Bado ataendeleza chuki hata kwa jeneza lake.,,na jamii yake iliyobaki nyuma.

Msiba wa Magufuli ni kielelezo tosha cha mapenzi ya jamii kwake.

Na kielelezo tosha kwa jamii kuwajuwa maadui zake wazi wazi..

Wanainchi tumejifunza vingi kupitia utawala wa magufuli,
Pamoja na kifo chake..

Wanainchi wengi wameshajuwa kumbe kuna genge la watu ,,
Ni watanzania wenzetu lakini hawana nia nzr na inchi yetu..

Wamejawa na ,
choyo
Wivu
Chuki
Tamaa na ubinafsi kwa ajili ya matumbo yao

Haswa wakati huu wa maombolezo ,,
ndy imedhihirika wazi wazi..

RIP my president
 
Hiyo democrasia anza kwanza kuitekeleza kwako na famalia mfyuuuuuu! Kwako mwenyewe unanyanyasa familia afu bila hata soni unataka mtu mwenzie ndio akufanyie, ww vipi!?
Tulia wewe msilete ujuaji mwingi kila kitu mnapinga mpk kwenye msiba mnapinga tu.
 
Maneno haya yamenipa spirit kubwa sana, kutokana na kifo na mazingira ya kifo chake hakika JPM alisacrify maisha yake kwa ajili ya watanzania hasa watanzania masikini kwa namna alivyohangaika kuwatetea.

Tatizo lake la moyo halikuhitaji stress na kazi yake ya urais ilijaa stress na aliharibu kuizuia stress na ndiyo maana hata kwenye lockdown ama partial curfew alisikika akisema "hakuna kitu kibaya kama stress na msitegemee nitaweka lockdown" hii yote ni kujaribu yeye mwenyewe kuendelea na majukumu yake bila stress huku akijua kabisa moyo wake una tatizo.

Huu ndiyo upendo wake kwetu, zawadi ya uhai kwa ajili ya watanzania hasa watanzania masikini. "Huu ndiyo upendo wa kweli, upendo wa mtu kutoa uhai wake kwa ajili ya MTU mwingine".
Pombe Magufuli hajawai kumtetea mnyonge au maskini yeyote bali alitumia wanyonge kujijenga kisiasa. Kama ni kutetea wanyonge alipaswa kuwafidia wale wananchi wa Kimara- Kibaha aliowavunjia nyumba kupisha barabara.

Angekuwa mtetezi wa wanyonge asingetumia mabilioni kujenga Chato kijijini kwao miundombinu inayostahili kuwa makao makuu ya Mkoa wa Geita. Huku watoto wa Watanzania wanasoma kwenye kwenye miti na wengine hawana madawati. Au kununua madreamliner wakati 80% ya Watanzania hawapati maji safi.

Magufuli ilikuwa ni LAANA, na Mungu ametuepushia, tujenge Tanzania yetu nzuri isiyo na ubaguzi wa kiitikadi, kikabila na kikanda
 
Watanzania wameonesha heshima kubwa sana leo kwa Magufuli.

Kama ulivosema a traitor is a traitor tu, Tundu lissu atakufa atazikwa kama iddi amini endapo atafia Tanzania, basi nina hakika maiti yake itachezewa na kuharibiwa
Na kueleza kweli mkuu,,Magufuli hakuwa wa kawaida.

Watu wapenda inchi yetu na Africa kwa ujumla ni pigo kubwa sana..

-- alikataa safari za ng'ambo.

-- akikataa kuwapigia magoti mabeberu matokeo yake wakamwita dictator.

-- wale wasiofata mstari na sheria za inchi walibanwa na kukimbia inchi.

-- akikataa Lock down. alichekwa lakini mwisho akaonekana mshindi.

-- alipuuza corona tuendelee kuishi nao,
Mwisho akaibuka mshindi.

-- inchi kujengeka kwa kasi ya ajabu tena inchi nzima..

Hakika sifa zake zinazongumzwa kote duniani.

He was not a politician but a true leader
 
Kwahiyo unataka kusema Awamu ya Magufuli Uwezo wetu wa kujitegemea kiviwanda uli-improve?! Nyie watu acheni utani jamani!!!! Sukari bei juu! Mafuta ya kula hayaonekani!! Mauzo ya nje kutoka manufacturing sector yameshuka!! Viwanda vingi uzalishaji umeshuka!! Saruji haishikiki! What exactly alichofanya Magufuli kwenye sector ya viwanda cha kutufanya tutembee kifua mbele? Are you blinded na hizi kauli za Tanzania ya Viwanda?! Kwa viwanda gani hasa?! Hiyo kauli mbiu ina tofauti gani na ile ya Kilimo Kwanza?!

Na nimesema kipindi cha Nyerere nchi ilikuwa dormant kwa sababu kama ulivyosema, Nyerere alijenga viwanda vingi sana! Lakini kama ni mfuatiliaji mzuri wa uchumi wa Tanzania, hadi Mwalimu anaondoka viwanda vingi vilikuwa havizalishi na hata vilivyokuwa operational vilikuwa vinafanya hivyo kwa hasara!!! Man, inawezekana mimi na wewe tulikuwa wadogo au hatujazaliwa lakini uliza watu wakuambie ni namna gani hata dawa ya meno ilionekana ni anasa!! Ni namna gani watu walikuwa wananunua sukari kwa kupanda foleni!!! Sasa kama ktk mazingira hayo nchi haikuwa dormant, man, labda nitafutie a better phrase lakini kwangu naona hiyo ndiyo phrase sahihi hasa! Kwamba, hapo kabla nchi ilikuwa na uhai lakini from late 1970's nchi ikalala kabisa kiuchumi!!!
Labda utanielewa kwa mifano kidogo.

Kuna msemo kwamba mfundishe mtu kuvua badala ya kumpa samaki kila wakati. Ni tafsiri yenu mbovu ya maisha yalivyokuwa enzi iza ujamaa ndiyo mnaita "dormancy". Nchi ndio mara tu imekuwa taifa huru, watu wanajifunza kujitawala na katika jitihada zao wakafanikiwa kujenga viwanda vyetu tukawa na "made in Tanzania" nyingi tu. Ni kutokana na watu wa aina yenu walioshindwa kuwa na uvumilivu kwamba wapo katika hatua ya kujifunza "kuvua" viwanda vilikufa. Watu hawakufanya kazi kwa moyo kwa sababu ya ubinafsi. Mameneja wa viwanda wakavihujumu viwanda, maana walitaka "utajiri" badala ya kuona mbele. Mliona mnacheleweshwa sana "kupata" samaki wenyewe mkataka mpewe samaki tu. Na kweli viwanda vilikufa, waliotaka wawapatie "samaki" walifanikiwa (nguo kutoka nje, viatu kutoka nje, n.k, n.k), na naona hayo ndio maisha mnayotaka hata leo.

Magufuli alitaka tuvue samaki wetu wenyewe. Msisitizo wake wote wa Tanzania ya viwanda ilikuwa ni kuhuisha ile spirit waliokuwa nayo waasisi wa taifa letu. Viwanda vilivyojengwa ndani ya awamu ya tano vinaweza visiwe na hadhi ya viwanda vya nchi za Magharibi au Uchina, lakini ndio hivyo, ni kipindi cha mpito, tunajifunza kuvua samaki wetu wenyewe. Na ndio uliokuwa msukumo wake wa miradi mikubwa, Tanzania iweze kujitegemea yenyewe. Kupanda kwa bei za vitu, n.k. utalichukulia positive tu iwapo unajua Tanzania inaelekea wapi. Katika jitihada zetu za kujitegemea lazima kutakuwepo na mambo kama hayo, ila yachukulie kama necessary transition.

Mbona concept simpo tu? Au we mwenzangu unapenda sana kubaki nchi maskini milele?
 
Labda utanielewa kwa mifano kidogo.

Kuna msemo kwamba mfundishe mtu kuvua badala ya kumpa samaki kila wakati. Ni tafsiri yenu mbovu ya maisha yalivyokuwa enzi iza ujamaa ndiyo mnaita "dormancy". Nchi ndio mara tu imekuwa taifa huru, watu wanajifunza kujitawala na katika jitihada zao wakafanikiwa kujenga viwanda vyetu tukawa na "made in Tanzania" nyingi tu. Ni kutokana na watu wa aina yenu walioshindwa kuwa na uvumilivu kwamba wapo katika hatua ya kujifunza "kuvua". Mliona mnacheleweshwa sana "kupata" samaki wenyewe mkataka mpewe samaki tu. Na kweli viwanda vilikufa, waliotaka wawapatie "samaki" walifanikiwa, na naona hayo ndio maisha mnayotaka.

Magufuli alitaka tuvue samaki wetu wenyewe. Msisitizo wake wote wa Tanzania ya viwanda ilikuwa ni kuhuisha ile spirit waliokuwa nayo waasisi wa taifa letu. Viwanda vinavyojengwa vinaweza visiwe na hadhi ya viwanda vya kimataifa nchi za Magharibi au Uchina, lakini ndio hivyo, ni kipindi cha mpito, tunajifunza kuvua samaki wetu wenyewe. Na ndio uliokuwa msukumo wake wa miradi mikubwa, Tanzania iweze kujitegemea yenyewe. Kupanda kwa bei za vitu, n.k. utalichukulia positive tu iwapo unajua Tanzania inaelekea wapi. Katika jitihada zetu za kujitegemea lazima kutakuwepo na mambo kama hayo, ila yachukulie kama necessary transition.

Mbona concept simpo tu? Au we mwenzangu unapenda sana kubaki nchi maskini milele?
We acha ujinga alikuwa anatufundisha kuvua Samaki, wakati huohuo anaendelea kuua shughuli za watu kwa kutoza kodi isiyolingana na tunachouza,Hali ile ingeendelea Biashara zote zingefungwa. Anachukua hela zetu anaenda kujenga Chato
 
Halafu achana na mawazo ya kuridhika na utajiri wa kitoto uliojengwa kwenye msingi wa uchumi wa uchuuzi. Wengi waliokuwa hawakubali sera za Magufuli ilikuwa sababu mlionjeshwa maisha fulani enzi za Kikwete ya maisha ya utajiri feki. Watu mnasema maisha yalikuwa afueni chini ya Kikwete kwa sababu ya uchumi huo feki unaotegemea pesa za wizi wizi. Uchumi halisi, na utajiri wa kweli ni ule unaopatikana kwa nguvu zako na uzalishaji wako mwenyewe.
 
Hamuelewi kitu kimoja.... Issue huwa sio chanzo cha utajiri issue ni mzunguko wa hela. Mfano ukipandisha mishahara obvious mzubguko utapaa n.k ssa JPM kwanza alipoka tender zote za ujenzi from private sector kwenda TBA, mikopo akawa anafoka why wakope benki za biashara sio benki za serikali, aliondoa account za wizara kadhaa kule BOT, Reserve ratio requirement BOT ilipandishwa hivyo kuwanyima ukwasi benki za biashara, kuondoa ma conference kufanyika hoteli binafsi n.k

Ila kma angebana ufisadi alafu akachochea private sector kukua mbona watu wasingepovuka.

Nadhani NGOs zianzishe jukwaa la uchumi lieleweshe wananchi macro economics zinavyofanya kazi maana wengi mnapotoshwa kuwa wanaolia eti wapiga dili.
 
Labda utanielewa kwa mifano kidogo.

Kuna msemo kwamba mfundishe mtu kuvua badala ya kumpa samaki kila wakati. Ni tafsiri yenu mbovu ya maisha yalivyokuwa enzi iza ujamaa ndiyo mnaita "dormancy". Nchi ndio mara tu imekuwa taifa huru, watu wanajifunza kujitawala na katika jitihada zao wakafanikiwa kujenga viwanda vyetu tukawa na "made in Tanzania" nyingi tu. Ni kutokana na watu wa aina yenu walioshindwa kuwa na uvumilivu kwamba wapo katika hatua ya kujifunza "kuvua" viwanda vilikufa. Watu hawakufanya kazi kwa moyo kwa sababu ya ubinafsi. Mameneja wa viwanda wakavihujumu viwanda, maana walitaka "utajiri" badala ya kuona mbele. Mliona mnacheleweshwa sana "kupata" samaki wenyewe mkataka mpewe samaki tu. Na kweli viwanda vilikufa, waliotaka wawapatie "samaki" walifanikiwa (nguo kutoka nje, viatu kutoka nje, n.k, n.k), na naona hayo ndio maisha mnayotaka hata leo.
Sasa hayo uliyotaja kwani ndo yanaondoa ukweli kwamba nchi ilikuwa dormant kwa uchumi wake kuchungulia kaburini?! Man, tuache porojo!!! Uchumi wa Tanzania ulisimamiwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi... hilo ndo tatizo!! Na Mwalimu alikuwa mkali maradufu kwa wapinzani wake kisiasa kuliko waliovuruga uchumi, hilo nalo ni la pili! Lakini mbali na hapo, Vita vya Kagera ambavyo ukivichunguza sana vilitokana na Mwalimu kutaka kumsaidia Swahibu wake Obotte ndo vikaja kuvuruga kila kitu! Hadi vita vile vinaisha, nchi ikabaki hoe hae! Uchumi haukui! Viwanda havizalishi!

Kwamba eti ndo maisha mnayotaka hadi leo; ni maisha wanayotaka akina nani?! Na unasema ndo wanayotaka leo kwa kutumia vigezo vipi?! Leo hiii uzalishaji upo chini ya sekta binafsi! Ni nani atataka kufanya kiwanda chake kisizalishe kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu?!

Magufuli alitaka tuvue samaki wetu wenyewe. Msisitizo wake wote wa Tanzania ya viwanda ilikuwa ni kuhuisha ile spirit waliokuwa nayo waasisi wa taifa letu. Viwanda vilivyojengwa ndani ya awamu ya tano vinaweza visiwe na hadhi ya viwanda vya nchi za Magharibi au Uchina, lakini ndio hivyo, ni kipindi cha mpito, tunajifunza kuvua samaki wetu wenyewe. Na ndio uliokuwa msukumo wake wa miradi mikubwa, Tanzania iweze kujitegemea yenyewe. Kupanda kwa bei za vitu, n.k. utalichukulia positive tu iwapo unajua Tanzania inaelekea wapi. Katika jitihada zetu za kujitegemea lazima kutakuwepo na mambo kama hayo, ila yachukulie kama necessary transition.

Mbona concept simpo tu? Au we mwenzangu unapenda sana kubaki nchi maskini milele?
Tanzania ya Viwanda ni kauli mbiu tu lakini ukweli ni kwamba alikuwa na sera mbovu za kiuchumi ambazo ndizo ziliifanya sekta binafsi idorole!! Kwamba eti viwanda vilivyojengwa awamu ya tano vinaweza visiwe na hadhi na ya vile vya Uchina na Western; ni viwanda vipi hivyo?! Ni viwanda vipi vimejengwa ambavyo ni very exceptional kushinda viwanda vyote vilivyojengwa kabla yake?! Unaweza kutaja angalau vitano hapa? Kwamba kupanda kwa vitu nitachukulia positive; kwanini nichukulie positive wakati ukweli ni kwamba bei inapanda kwa sababu uzalishaji umeshuka?! Tangu lini kushuka kwa uzalishaji kukachukuliwa positive?!

Sipendi nchi ibaki maskini lakini kwa sera za Magufuli nchi ingeendelea kuwa maskini kwa sababu uchumi wake ulikuwa wa kipropaganda zaidi kuliko uhalisia!!!
 
Utaukalia tu maliza kubweka..unakusubili
Kusubili ndo nini?! Hata kuandika kwa Kiswahili fasaha hujui!!! Btw, nani anabweka kati yangu na wewe uliyeibuka from nowhere na kuanza matusi na kunitisha? Jinga sana wewe jamaa!!! Hivi kwa akili yako unajiona kabisa kwamba una uwezo wa kunitisha?! Huyo Mungu Mtu wenu katisha wangapi na mwenyewe hivi sasa yupo wapi?! Kageuka kuwa "bidhaa ya maonesho"!
 
Hivi ni kwa nini wachukua picha za video hawachukui sehemu ambayo na sisi tunaoomboleza tukiwa nyumbani tunaweza kuona sura ya Mh. Kwa dakika za mwisho? Au wanakatazwa? Au ndio maadili ya kazi yanawataka hivyo!? Ningetamani waonyeshe kama ilivyokuwaga kwa Hayati Baba Wa Taifa!
 
Back
Top Bottom