Kiranga nakubaliana na hoja zako ila nina wasiwasi unapost mfululizo kumyima Regia aituhabarishe kilichojiri huko jimboni Kilombero au umetumwa na mafisadi nini?
hivi inakuwaje kura zinashindwa kuibiwa Ubungo na Kawe lakini zinaibiwa kwenye majimbo mengine?
(Asprin, kama masuala ya aina hii pia hayatakiwi kwenye hii thread naomba kufahamishwa)
Sawa mzee wa ligi!!
inawezekana kabisa hususan ktk jitihada za kutengeneza perception za kujengea hoja kama hiyo ya msingi wa swali lako maana kila mara wapenda haki tutakapolalama mtanyoosha vidole na kusema mbona mnyika na sugu wameshinda
hivi inakuwaje kura zinashindwa kuibiwa Ubungo na Kawe lakini zinaibiwa kwenye majimbo mengine?
(Asprin, kama masuala ya aina hii pia hayatakiwi kwenye hii thread naomba kufahamishwa)
Mkuu Kiranga, unaonekana una kitu personal na dada Regia.
Ushauri wangu kwa dada regia ni kuhakikisha kuwa anakuwa na ukaribu zaidi na wananchi wa Kilombero katika shughuli za maendeleo kwa kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia kuondoa kero zao mbalimbali hasa maji na pengine kusaidia wasiojiweza kulipia karo/ada za shule watoto wao ili watoto wao watumie nafasi wanazopata katika kujiendeleza kielimu. Ukifanya hayo mawili nje ya ubunge na uhakika utaweka ukaribu zaidi na wananchi na mwaka 2015 god willing utarudi kwa kishindo kikuu. Mungu akubariki na akutie nguvu. Amen
badala ya kutafuta kiini cha tatizo na kujua kwa nini mkakati wa kuzuwia kura zisiibiwe ulifanikiwa ubungo na na kushindwa katika majimbo mengine imekuwa muuliza suali miongoni mwa watakaonyoosha vidole kupinga wapenda haki.
kazi kweli kweli.
Niseme haya machache. Mpaka sasa regia hajasema mipango yake ya baadaye ni ipi - kama atagombea tena au la. Na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye kamuuliza kuhusiana na mustakabali wa mipango yake ya baadaye. Katamka "karudi" ndiyo imekuwa nongwa hadi kupelekea kuitwa "mamluki". Ni kama vile regia hana haki ya kupumzika baada ya mikikimikiki ya kampeni. Kibaya zaidi hakuna ambaye kamuuliza kuhusu mipango yake ya baadaye (ya kisiasa). Vipi kama keshaamua kuwa siasa yeye basi? Aendelee kukaa tu kilombero? Wakati mwingine ni vizuri kuuliza kwanza kuliko kusadiki na/au kutoa hukumu haraka haraka
kwa mujibu wa orodha ya Chadema ya viti maalum kwa wanawake iliyochapishwa magazetini, Regia yupo kwenye orodha kwenye nafasi za mwanzo mwanzo
labda ndio maana wengi hawajamuuliza kwa kuwa iko wazi kuwa ni mbunge wa viti maalum vya chadema.
Niseme haya machache. Mpaka sasa regia hajasema mipango yake ya baadaye ni ipi - kama atagombea tena au la. Na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye kamuuliza kuhusiana na mustakabali wa mipango yake ya baadaye. Katamka "karudi" ndiyo imekuwa nongwa hadi kupelekea kuitwa "mamluki". Ni kama vile regia hana haki ya kupumzika baada ya mikikimikiki ya kampeni. Kibaya zaidi hakuna ambaye kamuuliza kuhusu mipango yake ya baadaye (ya kisiasa). Vipi kama keshaamua kuwa siasa yeye basi? Aendelee kukaa tu kilombero? Wakati mwingine ni vizuri kuuliza kwanza kuliko kusadiki na/au kutoa hukumu haraka haraka
Wapwaz na Binamuz wote.
Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.
Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.
Nimewamiss si kidogo!!!Natafuta muda nionane na baadhi yenu.
With love
Regia
Sasa atakuwaje karibu na wananchi wa Kilombero kwa speed hii ya kuwakimbia wiki moja tu baada ya uchaguzi? I mean hata hakuwa na decency ya kukaa nao kidogo baada ya uchaguzi kuangalia maisha yao wajue alikuwa na interest beyond campaign za uchaguzi ?
basi jifunze namna ya kuunda na kuuliza maswali ili pindi unapouliza usionekane kama unatia shaka au usionekane upo upande fulani wa hoja. Msikiko wa sauti (tone) ni suala muhimu sana ktk mawasiliano. Kumbuka 'its not what you say but how you say it'