Nimerudi Salama ingawa................

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
WanaJf Natumaini hamjambo. Nimerudi salama ingawa sikuaga. Nilikuwa niliondoka kupanda mlima wetu Kilimanjaro tarehe 30 Nov 10. Safari ilianza pale machame gate as expected. I were with friends from Norway na walikuwa 13. Mkosi ulianza mapema tu! Siku ya pili tu mmoja wa rafiki zangu (mwanamke) aliugua na kuamualiwa arudi chini. We had a great time infact. On a summit push (that was 5th December) at about 5300meters absl niligundua kuwa mmoja wa rafiki hakuwa salama. Nilikubaliana na mmoja wa technical adviser from Norway kwamba he should go down to Barafu camp haraka. While tukiongea aliomba kukaa chini. Kwa mshangao tulipomsemesha within 5 seconds! Hakujibu. We was gone. My friend DIED at 5300mts ABSL saa 03:20. Tulipata ushirikiano wa kutosha toka uongozi wa KINAPA kusema ukweli. Tunategemea kusafirisha mwili wa O C Pettersen kesho Jumamosi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Wakuu niko salama na nitakuwa nanyi hapa.
 
pole sana.......ni msiba wa kusikitisha huo....alizidiwa na hali ya hewa au alikuwa mgonjwa?.....
 
Pole sana kwa msiba
Najua kwa sasa midomo itakuwa imechubuka kunywa chai ya moto kama maji ya kunywa, utakuwa umepauka kama wajipaka unga, uongo? but its good to venture na rest in peace huyo alofariki!
 
pole sana.......ni msiba wa kusikitisha huo....alizidiwa na hali ya hewa au alikuwa mgonjwa?.....
Asante sana. Taarifa za madaktari wa Muhimbili zinasema kuwa alikufa kwa pulmonary edema. Binafsi sijaridhika na taarifa hii kwa kuwa kifo chenyewe kilikuwa cha ghafla sana. Pulmonary Adema hudumu kwa kitambo kidogo na huwa inaambatana na dalili kadhaa kama kukohoa kusikokoma na kupumua kwa haraka sana. Kwa kesi ya hu jamaa yangu haikuwa hivyo, Aliyumba mara moja mbili hivi tu na alipoomba kukaa hakuamka tena. Nimeongea na ndugu zake kwa kirefu kidogo na kuna baadhi ya vitu nimegundua. Nasubiri taarifa ya madaktari wa Norway ndo nitoe taarifa rasmi.
Nawashukuru sana

 
Pole sana kwa msiba
Najua kwa sasa midomo itakuwa imechubuka kunywa chai ya moto kama maji ya kunywa, utakuwa umepauka kama wajipaka unga, uongo? but its good to venture na rest in peace huyo alofariki!

Mkuu nimejipanga sana. Wala huwezijua kuwa ndo nimeteremka toka kileleni. Najua ni nini cha kufanya niendapo huko.
 
'Aeka mangi kutire mangi', kama ulipita machame gate nafikiri ulipitia nkwarungo, kialia,nkweseko. Unanikumbusha nyumbani nimepamisi sana maisha ya machame ni faraja tele baridi murua,ndizi,maziwa,mbege,mtori,kiburu,nyama choma nk.da we acha tu! hiyo baridi ya mlimani inaelekea kali sana hata hao waliozaliwa na baridi kali ya arctic zone wanashindwa kuimudu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom