Nimerudi, bado tupo pamoja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimerudi, bado tupo pamoja!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Ibrah, Aug 13, 2009.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Namshukuru Mungu, Muumba mbigu na nchi kwa wema na fadhili zake na
  kwa neema na rehema zake nyingi zisizo ukomo.

  Wana JF, ni miezi miwili imepita tangu nionekane ndani ya Jukwaa letu na Bunge la kipekee na mwanana la JF ambapo tuna uhuru wa kutoa mawazo anwai yenye fikra mseto na mchanyato wa mambo na maswala mbalimbali kwa ajili ya mustakabali mwema wa jamii, nchi na mtu mmoja-mmoja.

  Nimekuta tangazo kwenye kibao changu kisemacho sijachangia ndani ya Jukwaa kwa majuma kadha wa kadha! Kweli JF iko makini katika kufuatilia michango ya wanachama wake!

  Nilikuwa kwenye mizunguko ya hapa na pale ndani ya TZ na nchi yetu ni kubwa; pia si pote ambapo ni rahisi kupata internet cafe kwa urahisi na sehemu nyingine gharama ni kubwa! Ni hapa hapa na ni nchi hii hii ya Tanzania! Sehemu nyingine ambazo nimepita gazeti la siku 4 zilizopita linaonekana ni jipya (current newspaper)!

  Namshukuru sana Mwanakijiji kwa kutuwekea ile ripoti ya uchunguzi ya Usalama wa Taifa! Ni kazi kubwa sana umefanya Mkuu, na kama kutakuwa na lolote chanya litakalosababishwa na ripoti hiyo, basi wewe Mwanakijiji na wenzako ulowataja kukusaidia kutuletea ripoti hiyo ndiyo mtakaostahili heshima. Mbarikiwe sana!

  Niliona kwenye gazeti la Raia Mwema likieeza jinsi WATAWALA walivyotaharuki kwa ripoti hiyo ambayo inaufunua ukweli uliofichika nyuma ya MEREMETA- ama kweli kila king'aacho si dhahabu! Hapo awali ilisemekana kuwa luipta ripoti hiyo ilikuwa shurti ulipie $ 30/- ambacho kwa walio wengi ni kiasi kikubwa sana lakini MWanakijiji amekubali kutubandikia ripoti hiyo hadharani. Mwanakijiji, matokeo ya kazi hiyo utayaona muda si mrefu; Tumwombe Mungu awaumbue wanafiki na Watawala wetu ambao wako tayari kusulibiwa na kuufia ufisadi- hao ni mitume na manabii wa uongo; Nabii wa Kweli yuko tayari kusulubiwa na kuufia ukweli maana kama maandiko yasemavyo, na kama Nabii wa kweli alivyosema: "MTAIJUA KWELI NA HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU"

  Kinachitakiwa kufanyika ni kuhakikisha mamilioni ya Watanzania waliofichwa na kuumizwa na ushetwani huo wa Meremeta wanaipata ripoti hiyo ili kuwea kufanya maamuzi sahihi.

  Ni vema pia, Watawala wetu ambao walikuwa tayari kuufia usiri wa ufisadi wa Meremeta LTD wajitokeze na kutuomba radhi na kisha wachukue hatua dhidi ya dhidi ya washiriki wa ushetwani huo iwe fundisho na somo kwa viongozi na wenye mamlaka wote na wale wanaotarajiwa kuwa viongozi siku za usoni juu ya uwajibikaji.

  Tuko Pamoja,

  Ibrah
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ndugu karibu tena hapa jamvini! Habari za safari ya mbali ya miezi miwili???
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Karibu sana kiongozi, vita bado ni mbichi jifunge mikanda tutashinda tukiwa pamoja!
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Karibu tena mkuu Ibrah.......!!! Naona umerudi kivingine, busara na hekima tele!
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Asanteni sana ndugu zangu. NL, inabidi sala maalumu zifanyike ili busara unazoziona ndani yangu ziendelee kuwepo; nchi yetu ina mambo mengi sana ya kuumiza yanayosababisha sometimes busara itoweke na uchizi uingie! MH, habari nzuri, ingawa kuliwa na mapito magumu ya hapa na pale. Masa, tupo pamoja- tendelee kumkoma nyani giladi, tupigne hadi tone la mwisho la damu, tukishindwa sisi wana wetu wataemdeleza vita hii ya kifkra.
   
Loading...