Nimeridhika kabisa: Mbwana Samatta hakuwa msaada kwa Aston Villa, Watkins ameonesha utofauti mkubwa

Ndo mana huwa nilitamani sana bahati aliopata samatta angepata msuva angekua zaidi ya pale alipo samatta sasa hivi!!!

Msuva ni fighter hata uchezaji wake katika timu ya taifa mnauona kuliko huyo samatta!
 
Itakuwa huna au uwezo wako wa kuelewa Mambo ni mdogo.pole

Yupo njiani sasa anarudi kuja kulitetea Taifa lake kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi. Lazima mkubali kumpa heshima yake.

Haiwezekani kijana amepambana mpaka hapo alipofikia, halafu nyinyi kutwa kumpiga tu majungu.
 
sawa MCHAWI...endelea kumuwangia pia akiwa huko uturuki mana ndio kazi uliyonayo
 
Wewe ni wa tofauti! Mwenzako salary inasoma kila wiki. Wewe kila wiki uko mahakamani kuvizia watuhumiwa wa uhujumu uchumi ili upate chochote.

Unazingua Wakili msomi. Tusimkatishe tamaa mtu ambaye ni mpambanaji kuliko sisi. Ni Mtanzania wa kwanza kati ya Watanzania karibia milioni 60 kucheza EPL, kucheza GENK, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa Ligi! Nk.

Halafu unasema Samatta ni wa kawaida sana!! Sikubaliani na wewe.
. kila wiki yuko mahakamani
 
Wewe unapata sh ngapi kwa week?
 
Hoja hapa ni kiwango cha uwanjani cha Samatta kama mcheza soka. Hakuna haka ya kuzungumzia kipato na kazi za watu. Mkuu, tujadili kiwango cha Samatta cha uwanjani na kuacha mambo mengine yasiyohusika hapa. Kumbuka, kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
 
Mbona kama umepaniki? Na wewe ni Wakili Msomi? Hata kwenye hicho kiwango, bado huwezi kumuongelea Mbwana Samatta kama mchezaji wa kawaida!

Labda umlinganishe na Messi au Ronaldo! Ukija kwenye mafanikio ya hicho kiwango, Samatta siyo mchezaji wa kawaida! Rekodi yake inambeba. Na nimeielezea hapo juu! Au hata macho nayo tu huna?

Kumponda Samatta anayelipwa mamilioni ya fedha kwa wiki iwe kwa hicho mnachokiita kiwango chake cha kawaida, na huku wewe ukikimbizana na Magufuli bado litabakia kuwa jambo la kushangaza sana.

Kama mnamuona ana kiwango cha kawaida, si muende nyinyi sasa mkachukue nafasi yake kama ni jambo rahisi! Watanzania majungu yatakuja yatuue siku moja.
utamaliza nguvu zako tu mkuu kwa raia wa aina hio ...mambo ya uchaguz pia yanatuchanganya
 
Kwa kiwango chake, ufungaji wake, kazi yake, umakini wake na mchango wake kwa timu mchezaji mpya wa Aston Villa Ollie Watkins amedhihirisha kuwa mshambuliaji Mbwana Samatta hakuwa msaada wowote kwa timu hiyo.

Watkins ambaye amefunga mabao matatu katika kipigo cha mbwakoko alichokipata Liverpool ambaye ni bingwa mtetezi leo cha mabao 7-2, ni wazi kuwa Samatta alikuwa mzigo kwa Aston Villa.

Ukweli usemwe, Samatta hakuwa na kiwango cha kuwika Premier League na kuwa msaada kwa Aston Villa. Labda awike huko Uturuki alipo. Watkins ni moto!
Sisi Wahaya tunasema, "Ekyawe kijunda nokara"! Mimi nitaendelea kumuona Samatta ni kiboko sio zaidi ya Watkins tu bali zaidi ya Messi na Ronaldo!
 
Yupo njiani sasa anarudi kuja kulitetea Taifa lake kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi. Lazima mkubali kumpa heshima yake.

Haiwezekani kijana amepambana mpaka hapo alipofikia, halafu nyinyi kutwa kumpiga tu majungu.
Mtoa mada kaongelea uwezo wake kuwa Epl sio kutetea taifa, tatizo huwezi kuchanganua Mambo. Kwani kujitetea Taifa Kamzidi Ngasa, Canavaro, Msuva au Juma kaseja?? Tena kea taarifa yako msaada wake n mdogo Sana kwenye timu ya Taifa kuliko kina Msuva
 
Huu mjadala tuufunge. Naona unanichosha tu. Nisije nikawa nabishana na mke wa mtoa mada humu! maana jina lako halijafungamana na jinsia yoyote ile na kwa namna unavyonitolea maneno ya dharau na maudhi, inanipa walakini.
 
Wewe unapata sh ngapi kwa week?

Laki mbili na nusu! Nina digrii huku Samatta akiwa kaishia kidato cha nne tu! Ndiyo sababu namheshimu na kuwapuuza wale wote wanao mchukulia kama mtu wa kawaida katika kipengele chochote kile, akiwemo huyo Mrs Petro hapo juu.
 
Nyinyi watu wengine sijui mpira huwa mnautizama vipi!? Hebu leta takwimu sammata alipoteza clear chances ngapi, alianza game ngapi alifunga ngapi, hapo nfio tutaweza kujadili..

Ni kwamba katika game takriban kadhaa zilizochezwa villa hii sio villa ile. Tizama takwimu za aston villa hii na aston villa aliyoikuta samatta.

Unaposema samatta kimeenda kimerudi, samatta mwenyewe aliikuta timu dhofulhali, kaenda pale dirisha dogo kaikita villa ipo hovyo kama alivyoiacha.
 
Kwa kiwango chake, ufungaji wake, kazi yake, umakini wake na mchango wake kwa timu mchezaji mpya wa Aston Villa Ollie Watkins amedhihirisha kuwa mshambuliaji Mbwana Samatta hakuwa msaada wowote kwa timu hiyo.

Watkins ambaye amefunga mabao matatu katika kipigo cha mbwakoko alichokipata Liverpool ambaye ni bingwa mtetezi leo cha mabao 7-2, ni wazi kuwa Samatta alikuwa mzigo kwa Aston Villa.

Ukweli usemwe, Samatta hakuwa na kiwango cha kuwika Premier League na kuwa msaada kwa Aston Villa. Labda awike huko Uturuki alipo. Watkins ni moto!
Hamna kitu mle,hata kwenye reserve hawezi kupata nafasi
 
Kwa kiwango chake, ufungaji wake, kazi yake, umakini wake na mchango wake kwa timu mchezaji mpya wa Aston Villa Ollie Watkins amedhihirisha kuwa mshambuliaji Mbwana Samatta hakuwa msaada wowote kwa timu hiyo.

Watkins ambaye amefunga mabao matatu katika kipigo cha mbwakoko alichokipata Liverpool ambaye ni bingwa mtetezi leo cha mabao 7-2, ni wazi kuwa Samatta alikuwa mzigo kwa Aston Villa.

Ukweli usemwe, Samatta hakuwa na kiwango cha kuwika Premier League na kuwa msaada kwa Aston Villa. Labda awike huko Uturuki alipo. Watkins ni moto!
Naomba pia utuambie Watkins katengenezewa nafasi ngapi na Samatta alitengenezewa ngapi ili tuwianishe. Mnaoichambua Aston Villa baada ya Samatta sijui ni kwa nini huwa hamtaji mabadiliko mengine yaliyofanywa na timu. Asiyefuatilia mpira anaweza dhani kuwa Aston Villa wamemsajili Watkins pekee.

Pia asiyejua mpira anaweza kudhani kuwa Aston Villa bado wanacheza na mfumo wao uliowagharimu msimu uliopita wa 3-4-3. Ambapo walau nusu ya kwanza ya msimu uliopita walikuwa wakishambulia bali kuanzia Januari ya Samatta hawakuwa tena na attacking threat kwa wapinzani. Sababu mojawapo ikiwa kushuka kiwango na uchoyo wa mchezeshaji wao bwana Grealish.

Napenda wachambuzi wa sakata la Samatta Aston Villa wawe wanakuja uchambuzi uliokamilika.
 
Hoja hapa ni kiwango cha uwanjani cha Samatta kama mcheza soka. Hakuna haja ya kuzungumzia kipato na kazi za watu. Mkuu, tujadili kiwango cha Samatta cha uwanjani na kuacha mambo mengine yasiyohusika hapa. Kumbuka, kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
Ingekuwa vizuri kama ungeanza na kiwango chako uwanjani
 
Back
Top Bottom