Nimerepair trucks za DAF, Scania, MAN na Benz upande wa umeme lakini MAN tuwape mauwa yao, mpangilio wa mfumo wao wa umeme ni rafiki sana

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,045
Hello bosses and roses...

Humu watu baadhi wananijua kama computer programmer ila mie ni fundi magari pia. Kiukweli hizi gari za MAN wamejitahidi sana upande wa umeme, wiring iko organized vizuri mno, ukichukua MAN moja na trucks za makampuni mengine zenye range sawa ya bei basi utakuta MAN iko organized vizuri kuzidi hao wengine.

Kwanza kwenye MAN kila waya una namba yake, maboya yote yana ID pia. Hizi gari nyingi za siku hizi kuna miwaya mingi sana, ila wengi hawana mpangilio mzuri kama uliopo kwenye MAN hivo kufanya troubleshooting kuwa ngumu. MAN bila hata kuwa na wiring diagram unatengeneza.

Ila tukija kwa ndugu zetu scania aisee ni kichefuchefu, tena hizi zilizopo humu nchini nyingi kupiga shoti gari zima ni kawaida. Kwa uzoefu wangu kesi za truck kupiga shoti gari zima zinaongozwa na scania, ngoma inapiga shoti hadi main fuse box yote haitamaniki. Hii ni kwa sababu hizi gari organization yake ya wiring ni ya hovyo sana, fundi akigusa akachanganya kdg basi ni shida tayari, kwa MAN ni ngumu sana kuchanganya labda uwe hujui kabisa unalofanya
 
Wako vzr kwenye mpangilio wa wiring lkn hawajafanya urahisishe troubleshooting kama ilivo kwa MAN, wanaficha ficha sana ndo maana wengi wenye benz wanatengenezea kwa dealers. MAN ana mpangilio mzr na kila kitu kipo wazi,
Aaah okay kuna jamaa niliwahi kuona pale TBL mwanza wana repair BENZ za hapo kwahiyo wanakuwa ni kampuni kabisa ambayo mafundi wake wana utaalamu nazo?
 
Regional mkuu.
Kama mavumba yapo yapo Chukua MAN TGA 440 ya 2006 au Scania R420 ya 2007.

Hio MAN TGA ni 6x2 kama unapiga route za kwenye rami na dreva wako anajua kupanga mizigo fresh axle ya 6x2 haitomsumbua


Kwa kua umesema ndo unaanza unaweza kwenda kwa rebuilders wakakusukia gari yako kwa bei nzr tu, kuna wasomali fln hapa town wanafanya hio kitu. Ila ukijipanga ukavuta mojawapo ya hizo mbili hapo juu hutojutia hela yako
 
Back
Top Bottom