Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Asante kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kipindi chako chote na leo GENTAMYCINE bila Unafiki nasema Tanzania tarehe 17 March, 2021 tumempoteza "Malaika Maalum' aliyeletwa na Mwenyezi Mungu kuja Kutuamsha Watanzania, Kututhaminisha, Kutuheshimisha, Kutuaminisha na kutuletea Maendeleo ya haraka.

Kutoka Mwezi March 2021 hadi leo hii ( Mwezi Oktoba 2021 ) nimeanza Kuiona Tanzania ya tofauti kabisa ambayo imeanza kurudi nyuma na 'Kusuasua' katika Sekta nyingi na Maeneo mengi hali ambayo imeanza Kunitisha huku Machozi ya Kumbukumbu ya Kuondokewa nae Hayati Rais Dkt. Magufuli yakianza 'Kunibubujika' tena.

Nisamehe Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kukukosoa Kimihemko, nakukumbuka, nakulilia sana na namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahala pema Peponi ila huko Chato ulikolala sasa jua kuwa Viatu vyako bado ni Vikubwa na Vinawapwaya wale waliodhani kuwa aina ya Uongozi wako ulikuwa ni rahisi wakisahau kuwa Umahiri wako wa Kiuongozi uliongozwa ma kutawaliwa zaidi na Kumtanguliza Kwako Mwenyezi Mungu na Malaika wake.

Ninatamani 2025 aje tu Magufuli mpya.
Kweli siamini kama niwewe uliyeandika hapa

Ila HONGERA KWA KUTAMBUA UKWELI
 
Nchi zilizoendelea ukiondoka madarakani au ukifariki wanakuwa wamemaliziana na wewe, sisi tunaendelea kuwa na matumaini kuwa atatukomboa!
Heshimu Mtizamo wangu na Mawazo yangu. Sasa kama unajua kuna nchi nyingi tu zilizoendelea na Unazipenda huenda unatamani hata Raia wao kwanini usiende Kuishi nao huko na ukatuachia tuendelee Kuipambania Tanzania yetu na Kuwalilia akina Nyerere, Mkapa na Dkt. Magufuli?
 
Itachukua miaka mingi kumpata kama JPM.
Nakubaliana nawe tena 200% kabisa Mkuu. Nimechukua muda Kurejea 'Video' zake na Kugundua ya kwamba Mwenyezi Mungu alitupa Zawadi ya Thamani Hayati Rais Dkt. Magufuli na akaichukua mapema baada ya Kutuona Watanzania hatujamshukuru na Kuishukuru pia.

Hata Machozi yalinitoka sana tu Mkuu.
 
Tangu mwaka uanze nahisi huu ni uzi wako wa maana kuliko zote.

Anyway binafsi jpm nillikuwa namkubali kawaida tu hasa nikiwa sehemu ya changanyikeni kama humu, nilikuwa simchukii kama wengine, kuna vitu alikuwa akifanya nasema huyu kweli rais hata kama sisem ila moyoni nasema hili jembe.

Siku niliposikia habari za kifo chake trh 9 nilisikia maumivu ambayo sikujua yametoka wapi.

Miliogopa hata kumwambia mtu yeyote maana alienihakikishia kafa alinitaka nifunge mdomo wangu.
Nilikuwa nikiingia humu nakuta watu wanachangia nyuzi kibao eti jpm yupo wapi na mimi najilazimisha kuchangia as if sijui kinachoendekea.
Pili moyo haukuamini nilichoambiwa nikawa akisemea ' huyu mbwa nae mwongo jpm atakufaje kizembe hivi?

Siku moja nikataka kumwambia mama yangu moyo ukasema hapana yupo hai yule fala mzushi.
Trh 17 usiku nikaota eti kafa nikastuka usingizini nikajisemea hapana ni nawazo yaliyo kichwani mwangu coz nishapewa hiyo habari wiki moja kabla.
Niliamka nikapiga magoti nikasali mikasema hii ndoto isiwe kweli, nikaingia jf nikakuta mtu kapost eti kwa nini wasitangaze tu rais kashakufa kha! Ndo niliamini yale maneno.

Baada ya kutangaza nilipata maumivu ambayo sikujua yametoka wapi, maana niliona Tanzania ambayo jpm alikuwa akiitengeneza ikiyeyuka.

Niliona ujinga ukirudi kwa kasi, wizi, miradi yake ikifa, nidham ya watumishi ikirudi 0, ufisadi nje nje , majambazi wakirudi kwa kazi, unyanyasaji wa wanyonge, viongozi kula mishahara ya bure,kupewa kazi kwa kujuana, vyeti feki,
Nikaona lile genge sugu la majambazi wanaotesa nchi wakifurahia kifo chake, nililia sana nikasema Mungu alitupa malaika ila wengi tulichukulia poa.
Huko ulipo jpm ulale salama, hakuna siku imepita bila kukukumbuka. Binafsi nimekumiss sana.

Rip jpm.
Post yako tu hii imenifanya nianze Kulia.
 
Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Asante kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kipindi chako chote na leo GENTAMYCINE bila Unafiki nasema Tanzania tarehe 17 March, 2021 tumempoteza "Malaika Maalum' aliyeletwa na Mwenyezi Mungu kuja Kutuamsha Watanzania, Kututhaminisha, Kutuheshimisha, Kutuaminisha na kutuletea Maendeleo ya haraka.

Kutoka Mwezi March 2021 hadi leo hii ( Mwezi Oktoba 2021 ) nimeanza Kuiona Tanzania ya tofauti kabisa ambayo imeanza kurudi nyuma na 'Kusuasua' katika Sekta nyingi na Maeneo mengi hali ambayo imeanza Kunitisha huku Machozi ya Kumbukumbu ya Kuondokewa nae Hayati Rais Dkt. Magufuli yakianza 'Kunibubujika' tena.

Nisamehe Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kukukosoa Kimihemko, nakukumbuka, nakulilia sana na namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahala pema Peponi ila huko Chato ulikolala sasa jua kuwa Viatu vyako bado ni Vikubwa na Vinawapwaya wale waliodhani kuwa aina ya Uongozi wako ulikuwa ni rahisi wakisahau kuwa Umahiri wako wa Kiuongozi uliongozwa ma kutawaliwa zaidi na Kumtanguliza Kwako Mwenyezi Mungu na Malaika wake.

Ninatamani 2025 aje tu Magufuli mpya.
Amen!!Amen!!Amen!!
 
Chuma kile, kiboko cha PUMBAVU hizi...

Jambo ambalo watu wengi wanaliletea mzaha ni kufikiri demokrasi ya mzungu ya kubembelezana na kuleana leana ndio italeta maendeleo Africa..

Africa inahitaji Ubabe, unyama na kila aina ya ukatili kwa watu wake ambao wengi wao ni wapumbavu ili maendeleo ya kweli yapatikane..

RIP JPM...
Mkuu popote pale ulipo kwa post yako hii naomba nikupigie 'Salute' ya Heshima tena ile ya Kijeshi kabisa.

Hii post yako ingekuwa ni bidhaa inayouzwa hata kama ingekuwa ni Milioni ningejitajidi Kuinunua.

Umeandika vyema na Ukweli mtupu tu.
 
Back
Top Bottom