Nimepoteza uwezo wa kujiamini kabisa na sielewi hatma yangu

Kwaninavyo fikiri ni kuwa huna malengo kwa kifupi umeridhika pengine hapo ulipofika ndo ulipokuwa umejiwekea malengo kabla hivyo unajiona ushatimiza kila kitu. Jaribu kupanga malengo mapya naamini yatakupa msukumo wa kupambana zaidi ili uweze kuyatimiza
Daah... Nimekuelewa Sana mkuu.
Asante
 
Epuka sana muda wa kuwa peke yako, huo ni muda wa shetani, muda wa peke yako au upweke ni mbaya sana ni muda wa shetani kukutumia na kukujeuza kuwa mdhambi na kujiwazia vibaya
Asante sana
 
hao unaosema wanalia uchumi mbovu ushaawaambia hayo maneno?nchi nzuri sana tena sana tu watu wanalalamikia sera za awamu hii ushaona mtu analalamikia nchi ?
Nyie ndo wale Tundu lissu akimlaumu ndugai mnasema anaitukana nchi
Upo wrong mkuu
 
Hapa ndio unapokosea..ni kweli umerogwa na aliyekuroga ni wewe mwenyewe kwa imani na fikra yako hii.
Thought shape Reality, kama unaona umerogwa basi utaishi Hivyo hvyo maana we Create our own demons...
Hakuna kurogwa wala nini change mindset yako kwanza
Najibadirishaje? Ndio maana nimeomba ushirikiano hapa.
 
Maandiko yanasema Mungu alikujua wewe ungali upo tumboni mwa mama yako, amekuleta duniani anajua u utakua mtu fulani, amekupitisha vikwazo vingi kama ungekua ni wa kufa ungekufa muda tu
Daah mkuu ubarikiwe sana
 
Mkuu pole sana kwa hio hali iliyokukuta ila sio peke yako kusema ukwel. Ni wengi tu wwnye hiyo shida km hiyo hususani hyo ya kuwa na low self esteem hasa kipindi hiki ila kweny visababishi yamkini tunaweza kutofautiana, walio wngi ni kutokana na matarajio kwenda sivyo

Jiasess mwenyewe ujue hasa sababu ni nn. Yawezekana Settle for Average imechangia

Yawezekana ni LOW SELF ESTEEM tu ambayo kisaikolojia ni hali ya kawaida tu ambayo
 
Kama hujui na kuamini kuwa shughuli zako zinaathiriwa na siasa unafikiri utajua hatma yako kama hujui jambo dogo kama hilo?

Hujui siasa ndio maendeleo?
Hujui siasa ndio hukuletea wateja au kukupunguzia?
Hujui siasa zinaweza kukufanya upate faida nyingi au ndogo katika biashara zako?

Wewe kama huoni hayo basi jua bado hujajitambua, na maisha yatakuendesha mpaka akili ikukae.

Mimi mijitu kama hii ikijaga kuomba msaada kwangu, huwa naiuliza maswali machache nikishajua naongea na punguani, nakufukuza kama paka shume upeleke upunguani wako huko.
Mkuu Jamaa ni mjinga sababu hajui kitu mbaya zaidi ukijaribu kumuelewesha mbishi so ana upumbavu pia ndani yake..huyu anafikiri urefu wa size ya pua yake. Wakati wa Mwalimu enzi ya PM Sokoine watu walikuwa wanatupa pesa kwenye mito,vichakani,barabarn,wengine wakifukia chini sababu ya Sera zilizokuwapo wakati huo.watu walifilisika,waliokuwa matajiri wakawa maskin wa kutupwa ukimueleza Siasa ndio maisha hakuelewi.Siasa ndio inasababisha machafuko ktk baadhi ya nchi na kuzaa wakimbizi,kufanya hali ngumu ya kimaisha or kuboresha maisha ya watu inategemea na Sera na mitazamo ya watawala waliopo.
Hivi mwenye bomba kubwa LA maji ambae ana supply kwa wengine akiregulate kufungua kwa kiasi kidogo sana nyie mnaotegemea kusambaziwa na huyo mwenye bomba juhudi zako binafsi za kutaka maji mengi kutoka ktk chanzo hicho zitakusaidia nn??Unasema huna ari ya kufanya kazi utaipata wapi wakati kila ukifanya tija haionekani??Ila kwa sababu ya ujinga wa kutokujua tatizo umekimbilia kurogwa na nilijua mawazo yako yakoje ndio mana nikakupa angalizo mapema kuwa usije ukafikiri umerogwa.
 
Mimi sio hao wanaolia na serikali. Kwanza siamini km Kuna aina yasiasa inayoweza kubadili maisha yangu binafsi. Kwanza hakuna siasa inayosababisha mtu akae ndani asitoke kutafuta. Nisome vizuri utanielewa nimepoteza hari yamapambano. Hili nitatizo langu binafsi
Yaan kutokuamini kwako or kutokujua kwako hakubadilishi ukweli or uhalisia wa mambo.Aliekudanganya kuwa hakuna Siasa inayomfanya MTU akae ndani asitoke kutafuta nani?uwe una tafuta maarifa ndugu yangu sio mpaka jambo likukute ww au ulione kwa macho yako ndio ujue kuwa lipo..
 
Kwanza pole sana Mkuu,
Nikutake kitu kimoja uchukulie ni sehemu ya mapito yako na ni sawa kupitia hali hiyo ila usifikirie kama umerogwa huo ndio mwanzo wa kupotea.

Mim kuna kipindi nimepitia madeni yakawa ni mengi hadi nikakosa amani ya kuishi na kuanza kuona nimepotea sana kwa kukumbuka mafanikio yangu ya nyuma.

Ila kitu kilichonisaidia niliamua kutenga muda mwingi wa kuwa peke yangu na kujitafakari wapi nakosea huku nikimshirikisha Mungu shida zangu kabla ya kumshirikisha binadamu yeyote . Kiukweli baada ya muda nilifanikiwa sana kuwa na amani moyoni na kuchukulia matatizo yangu kama daraja la kuniongoza kufika upande wa pili.

Nikutake kwanza jitafakari pia kwa imani yako muombe Mungu akupe nguvu ya kushinda hali hiyo(usilaumu) kwani ukikosa changamoto duniani ujue mwisho wako umekaribia.

Jaribu kuhesabu baraka ulizonazo badala ya kuhesabu matatizo uliyonayo.

Usijaribu kumlaumu mtu yeyote kwa matatizo ulionayo sasa bali jione kama wewe ndio mwajibikaji mkuu(hii itakujenga kuona wapi ulikosea na kujifunza).

Usimtegemee binadamu yeyote akutatulie matatizo yako bali mwenyezi Mungu kwani imeandikwa amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa.

Tenda wema bila kujali malipo yeyote hata kwa wale wanaokutendea mabaya(hapa kuna siri kubwa sana ya kupata amani na mafanikio) trust me fanya hivyo utanipa mrejesho.

Mwisho tambua Mungu anakupenda sana haijalishi umemkosea kiasi gani, ila yeye hawezi kukuacha. Wajibika kwa nafasi yako na umshirikishe Yeye kwa kila jambo kwani akili yako inapokomea Yeye ndipo anapoanzia.

Asante!
 
Nimejikuta nashawishika kwa mara ya kwanza kuandika uzi humu jukwaani kwani miaka yote nimekuwa msomaji na mchangiaji tu!

Hii ni baada ya jana kupitia uzi wa mkuu TORABORA akiwa haelewi hatma ya maisha yake.

Picha linaanza. Nina elimu ya kawaida ambayo Watanzania wengi wanayo kwa sasa. Sijawahi kuajiriwa kwani ajira haijawahi kuwa kipaumbele ktk maisha yangu.

Tangu nikiwa home kipindi hicho usukani sahani break mkeka (kula bure kulala bure) nilikuwa mtu wa kujichanganya sana kwenye mishe tofauti hadi nikafanikiwa kutengeneza kigheto changu cha kitozi chenye full furniture kwa kipindi hicho nikiwa bado home.

Nikaaga home nikaingia street kupanga. Hapo hasira zikaongezeka mara dufu kila fursa + kazi, zilizopita mbele yangu hazikunipita. Kwa ujumla nilijituma sana na kukubalika sana.

Starehe zangu tangu nikiwa school ni hizi za kawaida yaani ganja sana, mziki, tungi kiaina. Japo kwa sasa nimepunguza sana.

Mungu akazidi kuwa upande wangu nikanunua kiwanja Chanika, nikanunua shamba heka moja Mvuti pia nikafanikiwa kununua eneo lingine Zingiziwa.

Mungu hakuniacha, nikaanza ujenzi Chanika. Mwaka 2016 nikahamia rasmi kwenye banda langu.

Nikakodi fremu mtaani nikafungua duka tigo pesa + gesi na makorakoro kibao.

Hapo ndipo picha kamili likaanza maisha yangu yakawa hayaeleweki mishe zangu haziendi. Yaani kila ninachofanya kinaleta matokeo hasi.

Nimepambana hadi 2019 mwanzoni hali yangu ya uchumi ikazidi kuwa mbaya zaidi. Kiduka nacho kikafilisika japo bado kipo kinachechemea baada ya kumpa mtu wa mshahara.

Mambo yamegoma kwenda, nimepoteza hadi marafiki sababu nadhani hawanielewi nimekuwaje. Nimekuwa mtu wa hofu bila sababu sijiamini kabisa yani.

Kuna kipindi nawaza kuinyofoa roho yangu ila nikiiangalia family nasita kidogo.

Mbaya zaidi nimekuwa mtu wa kushinda ndani muda mwingi sana. Nimekuwa mpweke balaa. Kichwa kimekuwa kizito, ubunifu zero kabisa!

Ni imani yangu kuna mahala nilikosea au kuna shida mahali. Nimelileta kwenu wakuu maana nadhani kwa ukubwa wa jukwaa hili kuna uwezekano kuna waliopitia haya nnayopitia au kuna wenye maono + maoni ya kujua na kushauri kuhusu hili tatizo langu.

Asanteni

Pole sana huwa utakoea kwa baadhi ya vijana wa umri wako!! Ni mapito yatapita usikate tamaa tu....PAMBANA.
 
nimegundua mpaka hapo hujajua maana ya SIASA, unadhani ni vyama vya CCM na CHADEMA hapa wanakueleza hali halisi ya kiuchumi mpaka kwenye duka lako kutonunua kitu kunatokana na mipango mibovu au mizuri iliyowekezwa katika Nchi yako kwa kipindi unachokizungumzia
Kuna walio-ona nafuu utawala wa Trump na wakawashangaa wanaoandaman
kuna walio-uona uongozi wa JK Nyerere kwani walipata nafuu
wakaja wa Mwinyi ruksa, Mkapa, J Kikwete na sasa tunakuambia Utawala huu una amani na umekubali maafisa wanaokusanya kodi yako wanalipwa 12M zaidi ya Mshahara wa Rais
sasa kwanini usikubali ni Siasa na itapita tu
basi Ma mbio wewe tatizo tumeshalijua hatuna msaada zaidi acha sisi tupambane
Kusingizia siasa ni kuongeza ugonjwa mwingine. Ila nimeupenda ushauri wako wamwisho.
Asante
Yaan kutokuamini kwako or kutokujua kwako hakubadilishi ukweli or uhalisia wa mambo.Aliekudanganya kuwa hakuna Siasa inayomfanya MTU akae ndani asitoke kutafuta nani?uwe una tafuta maarifa ndugu yangu sio mpaka jambo likukute ww au ulione kwa macho yako ndio ujue kuwa lipo..
Mkuu Jamaa ni mjinga sababu hajui kitu mbaya zaidi ukijaribu kumuelewesha mbishi so ana upumbavu pia ndani yake..huyu anafikiri urefu wa size ya pua yake. Wakati wa Mwalimu enzi ya PM Sokoine watu walikuwa wanatupa pesa kwenye mito,vichakani,barabarn,wengine wakifukia chini sababu ya Sera zilizokuwapo wakati huo.watu walifilisika,waliokuwa matajiri wakawa maskin wa kutupwa ukimueleza Siasa ndio maisha hakuelewi.Siasa ndio inasababisha machafuko ktk baadhi ya nchi na kuzaa wakimbizi,kufanya hali ngumu ya kimaisha or kuboresha maisha ya watu inategemea na Sera na mitazamo ya watawala waliopo.
Hivi mwenye bomba kubwa LA maji ambae ana supply kwa wengine akiregulate kufungua kwa kiasi kidogo sana nyie mnaotegemea kusambaziwa na huyo mwenye bomba juhudi zako binafsi za kutaka maji mengi kutoka ktk chanzo hicho zitakusaidia nn??Unasema huna ari ya kufanya kazi utaipata wapi wakati kila ukifanya tija haionekani??Ila kwa sababu ya ujinga wa kutokujua tatizo umekimbilia kurogwa na nilijua mawazo yako yakoje ndio mana nikakupa angalizo mapema kuwa usije ukafikiri umerogwa.
hao unaosema wanalia uchumi mbovu ushaawaambia hayo maneno?nchi nzuri sana tena sana tu watu wanalalamikia sera za awamu hii ushaona mtu analalamikia nchi ?
Nyie ndo wale Tundu lissu akimlaumu ndugai mnasema anaitukana nchi
 
Kwanza pole sana Mkuu,
Nikutake kitu kimoja uchukulie ni sehemu ya mapito yako na ni sawa kupitia hali hiyo ila usifikirie kama umerogwa huo ndio mwanzo wa kupotea.

Mim kuna kipindi nimepitia madeni yakawa ni mengi hadi nikakosa amani ya kuishi na kuanza kuona nimepotea sana kwa kukumbuka mafanikio yangu ya nyuma.

Ila kitu kilichonisaidia niliamua kutenga muda mwingi wa kuwa peke yangu na kujitafakari wapi nakosea huku nikimshirikisha Mungu shida zangu kabla ya kumshirikisha binadamu yeyote . Kiukweli baada ya muda nilifanikiwa sana kuwa na amani moyoni na kuchukulia matatizo yangu kama daraja la kuniongoza kufika upande wa pili.

Nikutake kwanza jitafakari pia kwa imani yako muombe Mungu akupe nguvu ya kushinda hali hiyo(usilaumu) kwani ukikosa changamoto duniani ujue mwisho wako umekaribia.

Jaribu kuhesabu baraka ulizonazo badala ya kuhesabu matatizo uliyonayo.

Usijaribu kumlaumu mtu yeyote kwa matatizo ulionayo sasa bali jione kama wewe ndio mwajibikaji mkuu(hii itakujenga kuona wapi ulikosea na kujifunza).

Usimtegemee binadamu yeyote akutatulie matatizo yako bali mwenyezi Mungu kwani imeandikwa amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa.

Tenda wema bila kujali malipo yeyote hata kwa wale wanaokutendea mabaya(hapa kuna siri kubwa sana ya kupata amani na mafanikio) trust me fanya hivyo utanipa mrejesho.

Mwisho tambua Mungu anakupenda sana haijalishi umemkosea kiasi gani, ila yeye hawezi kukuacha. Wajibika kwa nafasi yako na umshirikishe Yeye kwa kila jambo kwani akili yako inapokomea Yeye ndipo anapoanzia.

Asante!
Ushauri bora kabisa huu
 
Mkuu km umenisoma vizuri ni kuwa nimepoteza hari ya mapambano. Nimekuwa tofauti na asilia yangu. Moyo wangu umejawa na uoga na kutojiamini. Kiumri bado ni kijana na nimepambana vilivyo. Nilipotoka ni pagumu kuliko hapa nilipo. Na kwamtazamo wa wengi wanaonizunguka ( majirani) wananiona Mimi boss flan. Ila ukweli ndio huo hapo juu.
huwa siwezi kumwambia mtu undani washida zangu.
Usikate tamaa kirahisi hivyo, najua utakua unawaza utaanzaje upya
 
Nimejikuta nashawishika kwa mara ya kwanza kuandika uzi humu jukwaani kwani miaka yote nimekuwa msomaji na mchangiaji tu!

Hii ni baada ya jana kupitia uzi wa mkuu TORABORA akiwa haelewi hatma ya maisha yake.

Picha linaanza. Nina elimu ya kawaida ambayo Watanzania wengi wanayo kwa sasa. Sijawahi kuajiriwa kwani ajira haijawahi kuwa kipaumbele ktk maisha yangu.

Tangu nikiwa home kipindi hicho usukani sahani break mkeka (kula bure kulala bure) nilikuwa mtu wa kujichanganya sana kwenye mishe tofauti hadi nikafanikiwa kutengeneza kigheto changu cha kitozi chenye full furniture kwa kipindi hicho nikiwa bado home.

Nikaaga home nikaingia street kupanga. Hapo hasira zikaongezeka mara dufu kila fursa + kazi, zilizopita mbele yangu hazikunipita. Kwa ujumla nilijituma sana na kukubalika sana.

Starehe zangu tangu nikiwa school ni hizi za kawaida yaani ganja sana, mziki, tungi kiaina. Japo kwa sasa nimepunguza sana.

Mungu akazidi kuwa upande wangu nikanunua kiwanja Chanika, nikanunua shamba heka moja Mvuti pia nikafanikiwa kununua eneo lingine Zingiziwa.

Mungu hakuniacha, nikaanza ujenzi Chanika. Mwaka 2016 nikahamia rasmi kwenye banda langu.

Nikakodi fremu mtaani nikafungua duka tigo pesa + gesi na makorakoro kibao.

Hapo ndipo picha kamili likaanza maisha yangu yakawa hayaeleweki mishe zangu haziendi. Yaani kila ninachofanya kinaleta matokeo hasi.

Nimepambana hadi 2019 mwanzoni hali yangu ya uchumi ikazidi kuwa mbaya zaidi. Kiduka nacho kikafilisika japo bado kipo kinachechemea baada ya kumpa mtu wa mshahara.

Mambo yamegoma kwenda, nimepoteza hadi marafiki sababu nadhani hawanielewi nimekuwaje. Nimekuwa mtu wa hofu bila sababu sijiamini kabisa yani.

Kuna kipindi nawaza kuinyofoa roho yangu ila nikiiangalia family nasita kidogo.

Mbaya zaidi nimekuwa mtu wa kushinda ndani muda mwingi sana. Nimekuwa mpweke balaa. Kichwa kimekuwa kizito, ubunifu zero kabisa!

Ni imani yangu kuna mahala nilikosea au kuna shida mahali. Nimelileta kwenu wakuu maana nadhani kwa ukubwa wa jukwaa hili kuna uwezekano kuna waliopitia haya nnayopitia au kuna wenye maono + maoni ya kujua na kushauri kuhusu hili tatizo langu.

Asanteni
unapiga punyeto?
 
Asante mkuu.

Nimepata ushauri huo mara kadhaa natamani ila nashindwa kutekeleza.

Sijui nakwama wapi. Naweza kupanga kesho asubuh mapema naenda kwenye maombezi nikiamka hiyo asubuh nakuwa mzito balaa.

Kunaa waliofika mbali zaidi nienda kwa waganga wa tunguri huko sijawahi hata kufika tangu nizaliwe.

Kwa imani yangu mimi hapa tayari kuna uwalakin, kwanini uwe mzito esp kwenye mipango ya maombi.... kwenye waganga wa tunguri mimi sipo na binafsi sishauri... tafuta muda hata robo saa kila siku piga goti muombe Mungu akuepushe na hiyo hali ya uzito. Kabla hujaombewa anza kujiombea mwenyewe tena kwa kupiga goti na uombe ukimaanisha. Nakutakia kila la kheri
 
Hata mm nimeshangaa kuona anasema maisha yake hayana uhusiano na siasa wakati kula yake biashara yake, kulala kwake ni siasa sasa ninadhani huyu kapigwa kipapai. Ndo jibu rahis

Kama hujui na kuamini kuwa shughuli zako zinaathiriwa na siasa unafikiri utajua hatma yako kama hujui jambo dogo kama hilo?

Hujui siasa ndio maendeleo?
Hujui siasa ndio hukuletea wateja au kukupunguzia?
Hujui siasa zinaweza kukufanya upate faida nyingi au ndogo katika biashara zako?

Wewe kama huoni hayo basi jua bado hujajitambua, na maisha yatakuendesha mpaka akili ikukae.

Mimi mijitu kama hii ikijaga kuomba msaada kwangu, huwa naiuliza maswali machache nikishajua naongea na punguani, nakufukuza kama paka shume upeleke upunguani wako huko.
 
yaani una nyumba kiwanja na shamba na bado una biashra juu,,, alfu unasema uelewi elewi daaaaah

sisi tuliopanga chumba kimoja na tuna wake na watt tusemaje mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom