Nimepoteza uwezo wa kujiamini kabisa na sielewi hatma yangu

mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,255
2,000
Nimejikuta nashawishika kwa mara ya kwanza kuandika uzi humu jukwaani kwani miaka yote nimekuwa msomaji na mchangiaji tu!

Hii ni baada ya jana kupitia uzi wa mkuu TORABORA akiwa haelewi hatma ya maisha yake.

Picha linaanza. Nina elimu ya kawaida ambayo Watanzania wengi wanayo kwa sasa. Sijawahi kuajiriwa kwani ajira haijawahi kuwa kipaumbele ktk maisha yangu.

Tangu nikiwa home kipindi hicho usukani sahani break mkeka (kula bure kulala bure) nilikuwa mtu wa kujichanganya sana kwenye mishe tofauti hadi nikafanikiwa kutengeneza kigheto changu cha kitozi chenye full furniture kwa kipindi hicho nikiwa bado home.

Nikaaga home nikaingia street kupanga. Hapo hasira zikaongezeka mara dufu kila fursa + kazi, zilizopita mbele yangu hazikunipita. Kwa ujumla nilijituma sana na kukubalika sana.

Starehe zangu tangu nikiwa school ni hizi za kawaida yaani ganja sana, mziki, tungi kiaina. Japo kwa sasa nimepunguza sana.

Mungu akazidi kuwa upande wangu nikanunua kiwanja Chanika, nikanunua shamba heka moja Mvuti pia nikafanikiwa kununua eneo lingine Zingiziwa.

Mungu hakuniacha, nikaanza ujenzi Chanika. Mwaka 2016 nikahamia rasmi kwenye banda langu.

Nikakodi fremu mtaani nikafungua duka tigo pesa + gesi na makorakoro kibao.

Hapo ndipo picha kamili likaanza maisha yangu yakawa hayaeleweki mishe zangu haziendi. Yaani kila ninachofanya kinaleta matokeo hasi.

Nimepambana hadi 2019 mwanzoni hali yangu ya uchumi ikazidi kuwa mbaya zaidi. Kiduka nacho kikafilisika japo bado kipo kinachechemea baada ya kumpa mtu wa mshahara.

Mambo yamegoma kwenda, nimepoteza hadi marafiki sababu nadhani hawanielewi nimekuwaje. Nimekuwa mtu wa hofu bila sababu sijiamini kabisa yani.

Kuna kipindi nawaza kuinyofoa roho yangu ila nikiiangalia family nasita kidogo.

Mbaya zaidi nimekuwa mtu wa kushinda ndani muda mwingi sana. Nimekuwa mpweke balaa. Kichwa kimekuwa kizito, ubunifu zero kabisa!

Ni imani yangu kuna mahala nilikosea au kuna shida mahali. Nimelileta kwenu wakuu maana nadhani kwa ukubwa wa jukwaa hili kuna uwezekano kuna waliopitia haya nnayopitia au kuna wenye maono + maoni ya kujua na kushauri kuhusu hili tatizo langu.

Asanteni
 
mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,255
2,000
Pole sana kaka. Umejaribu kuliingiza hili swala kiimani zaidi? Jaribu hamna linaloshindikana. Tafuta kiongozi wa dini akuongoze vizuri
Asante mkuu.

Nimepata ushauri huo mara kadhaa natamani ila nashindwa kutekeleza.

Sijui nakwama wapi. Naweza kupanga kesho asubuh mapema naenda kwenye maombezi nikiamka hiyo asubuh nakuwa mzito balaa.

Kunaa waliofika mbali zaidi nienda kwa waganga wa tunguri huko sijawahi hata kufika tangu nizaliwe.
 
Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
457
1,000
Pambana mkuu ndo ukubwa huo.. Mimi nipo kwenye changamoto kubwa sana zaidi ya hizo zako na sijawahi kukata tamaa wala kufikiria kujiua. Amini tu changamoto ndio maisha yenyewe haya. Bila changamoto maisha hayana maana.
 
kianja kyamutwara

Senior Member
Nov 4, 2020
106
225
Hivi ni macho yangu hata mm siamini ninacho kiona na kusikia. Kuanzia kwa watu walionizunguka watu wanalia balaa uchumi umekua mgumu pesa hamna na kiukweli unaona hata sikukuu kuna marafiki zangu walishindwa kutoka hata ndani. Ninapogeukia upande wa jukwaa hili huu ni uzi wa tatu mfululizo watu wengine wanatishia kujinyonga hivi ndo hii Mama Tanzania ya kikwete au na kama maisha yanakua hiv wakati jiwe ndo kwaanza hata miez haijakatika je tunamaliza mitano hii na kama ghafla akaogeza mda yaan jiwe for life si tutakua vichaa wote. Ee mungu tunusuru na kikombe hiki
 
Mimi sio hao wanaolia na serikali. Kwanza siamini km Kuna aina yasiasa inayoweza kubadili maisha yangu binafsi. Kwanza hakuna siasa inayosababisha mtu akae ndani asitoke kutafuta. Nisome vizuri utanielewa nimepoteza hari yamapambano. Hili nitatizo langu binafsi
 
mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,255
2,000
Pambana mkuu ndo ukubwa huo.. Mimi nipo kwenye changamoto kubwa sana zaidi ya hizo zako na sijawahi kukata tamaa wala kufikiria kujiua. Amini tu changamoto ndio maisha yenyewe haya. Bila changamoto maisha hayana maana.
Poa, ila nazani hujanisoma vizuri. Nimepoteza hari ya upambanaji. Kumbuka kama rasirimali Ninazo so naona ajabu kwanini nimekuwa hivi.
 
Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,473
2,000
Tatizo linaanzia hapo ulipoweka material kua source of your happiness. Pole mkuu jifunze kuishi maisha yote ya tabu na raha. Material haya si ya kuyategemea zaidi yanakuja na kupotea.. What's given can be taken.

Take a breath...Piga moyo maisha yana pande mbili, pande nyingine ndio hiyo sasa unapimwa uaminifu na imani yako.
Be strong mate 💪 Life is not a bed of roses. Keep fighting
You will shine with or without your friends
 
Shukran mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom