Nimepoteza nia ya kumuoa kwa sababu amechora tattoo

Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
9,646
34,284
Wakuu nilikua ninademu ambae ni wamuda mrefu sana nilipanga nae mipango mingi ikiwa ni pamoja na kumuowa, familia yake ilinijua na yangu ilimjua pia, mahusiano yetu yalidum zaidi ya miaka mitatu

Nilisafiri kikaz na kuwa nae mbali kwa muda kama wa mwaka mmoja huku tukiendelea na mawasiliano na mipango yetu ikiwa ni ileile ya kumuowa baada ya kurud na familia yangu na yake ilijua hivyo kuwa nikirud ni ndoa

Lakin baada ya kurud nimegundua kuwa amechora tattoo kwenye paja, kiukweli baada ya kugundua nimejikuta namchukia sana, moyo wangu unaamin kila mwanamke mwenye tatto ni malaya, nimesitisha mipango yote ya kumuowa.

Wazazi wake na wangu wanajuana na wameniweka kikao kuniuliza juu ya ndoa nimekataa sitomuowa huyo bint na nikiulizwa ni kwann nashindwa kuelezea sababu mwsho wa siku imekua mgogoro baina ya familia yangu na yake.
Najaribu kuuamimisha moyo wangu kuwa siyo kila mwanamke mwenye tattoo ni malaya lakin moyo umekataa kuamin.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa sipendi wanaume wanaochora tattoo nikidhani wote wahuni ila Lionel Messi akanifanya nibadili mtazamo wangu

Nilikuwa sipendi wanaume wanaosuka nywele nikidhani wote wahuni ila Jah Prayzah akanifanya nibadili mtazamo wangu

So na wewe mtoa mada siku utakapokutana na mwanamke ambaye amechora tattoo na siyo malaya utabadili mtazamo wako
 
Nilikuwa sipendi wanaume wanaochora tattoo nikidhani wote wahuni ila Lionel Messi akanifanya nibadili mtazamo wangu

Nilikuwa sipendi wanaume wanaosuka nywele nikidhani wote wahuni ila Jah Prayzah akanifanya nibadili mtazamo wangu

So na wewe mtoa mada siku utakapokutana na mwanamke ambaye amechora tattoo na siyo muhuni utabadili mtazamo wako
Wewe una tattoo? Achana kuangalia watu wa ulaya na kuwalinganisha na wa huku kwa mtogole
 
Back
Top Bottom