Nimepoteza mama yangu kipenzi usiku wa leo

Pole sana mkuu, nakutakia uvumilivu atika kipindi hiki kigumu
 
Pole sana kiongozi: Mungu yuko pamoja na wewe na akuongezee ujasiri katika hiki kigumu cha kuondokewa na Mama.
 
mkuu Pdiddy

pole sana ... hii ni mapenzi ya mwenyezi mungu .... sote tutaifuata safari hii ya mama yetu mpendwa

mungu amuweke mahali pema
 
Pole sana. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
Pole sana mwanajamvi mwenzetu Pdidy! tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu elewa kwamba sote tuu njia moja na katika kipindi hiki kigumu kuliko jambo lolote hapa duniani tunakuweka kwenye maombi na mwenyezi mungu muweza wa yote ampunzishe mama yetu mahapa pema peponi amina...RIP mammy Pdidy...
 
Pole mkuu MUNGU amempenda zaidi naomba tueleweshe Msiba upo mji gani?
 
Mkubwa,
Mama ameondolewa duniani ili uyafanyie kazi aliyokufunza!..Hakikisha unasimamia alichokiamini!
Mungu ampumzishe mahala panapo pepo njema!
 
Pole sana mkuu.M.Mungu akutieni nguvu na muwe wenye subra katika kipindi hiki. Hakika sisi ni wa M.Mungu na kwake tutarejea
 
Pole sana Ndugu, inahuzunisha sana, nawapeni pole na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki cha Msiba.
 
Ni kipindi kigumu sana....ila kwa uwezo wake muumba mbingu, ardhi na sisi viumbe tuliomo na muipate nguvu na faraja kutoka kwake. Amrehemu mama na marhum wote waliotangulia mbele za haki

Pole sana kaka......na ndugu wengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom