Nimepoteza imani na benchi la ufundi la Yanga

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
905
1,406
Salama jamani?

Mimi mwenzenu ni mshabiki mkubwa wa Yanga na kama mashabiki wengine wa Yanga nafsi yangu huwa inaumia sana timu yangu ikifungwa.

Matokeo ya mechi dhidi ya Simba yameniumiza sana lakini kilichonikera zaidi ni kiwango kilichoonyeshwa na timu yangu. Timu kusema ukwel ilicheza katika namna ambayo ilinipa mashaka kama kwel ilikuwa na nia ya kuongeza goli na kutumia advantage ya Simba iliyokuwa pungufu na iliyopoteana.

Timu iliendelea kucheza bila haraka wala ubunifu wakati Simba ikiwa imepoteana, tena kilelemamalelemama hivi mpaka Simba iliyopungufu ilipojipanga na kupata nguvu. Hasa baada ya kuona hata wakija mbele kushambulia hakukuwa na tishio lolote kutoka Kwa Yanga na hatimaye wakashinda mchezo huo.

Kilichonisikitisha ni namna ambavyo Yanga huwa haibadili aina ya mchezo inaocheza hata kama hauna tija jambo ambalo kiufundi ni udhaifu. Pili mabadiliko yaliyofanywa ya kumuingiza Mahadhi ambaye kwa mtazamo wangu bado hajawa na ukomavu wa kumtumainia katika mchezo kama huu wa Simba na Yanga, nao ni dhaifu mwingine.

Tatu golikipa wetu pamoja na urefu alionao ana tatizo la kutokujua namna ya kujiposition na matokeo yake huwa anafungwa magori ya mbali ya juu au pembeni ambayo kwa kimo chake hutegemei afungwe. Hali inaonyesha hamna mtu anayemfunza katika hili ili abadirike na huwa anarudia makosa yaleyale ya kukosea kujiposition. Ni tofauti na Juma Kaseja ambaye alikuwa mfupi lakini alikuwa mahili Kwa sababu ya kujua namna ya kujiposition.

Hii ni timu ambayo mpaka sasa ina makocha wengi kuliko timu yoyote ambao wamepewa nyadhifa tofautitofauti wapo kina Pluijim, Mkwasa, Lwandamina mwenyewe na Mwambusi. Je, haya madhaifu kwann yanajitokeza bila utatuz? Hawashauriani na kocha aliyepo?

Mwisho nipongeze tu uhodari wa kocha wa Simba Omog katika suala hilihili la ufundi kwan amethibitisha kuwa mahili katika mbinu na saikolojia pia, upande wa fitness pia benchi la ufund la Simba limefanikiwa pia.

Karibuni wadau wenzangu wa Yanga tushee idea kuhusu timu yetu pendwa katika nyanja nilizozigusia, daima mbele.
7f11732e019913222e97d3858a70602c.jpg
 
Juzi tu hapa mlikuwa mnashangilia ushindi mnono wa kimataifa ulioletwa na uongozi huo huo na wengine kutaka kumzawadia Manji huo ushindi apoozee machungu, leo unakosa imani kisa mmefungwa na simba! Ina maana mafanikio kwenu ni kuifunga simba?
 
Pale kilichopo sasa ni mvurugano tu, kila mmoja anataka apange timu- hauwezi kuwaweka pluijim, mkwasa na lwandamina pamoja halafu timu ielewane, hapo tutawafunga hadi mseme po
 
Wachezaj ni wachovu na wanaonekana hawana hamu na mpira wanacheza tu kutmiza majukumu yao yawezekana kucheza muda mrefu bila mapumzko ama kutokua na hali ya ubngwa kutokana na kuuchukua misimu miwili mfululizo na hii uzikumba timu nying ktk lg kuu mbal mbal hapa dunian hasa wanapotoka kuchukua ubngwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom