Nimepoteza amani ya nafsi, nairejeshaje?

Ronee

Senior Member
Jun 1, 2018
156
155
Natumai mu wazima watoto wa mama Tanzania.

Leo nilikuwa nakatiza mitaa flani nikitokea kwenye matembezi mafupi, mitaa hiyo haijachangamka sana kwa maana ya wakazi wake wachache, ghafla nikasikia kelele na heka heka za hapa na pale, watu hawakuwa wengi. niliposogea eneo hilo nikakuta ni dogo flani wa miaka kama 16-17 amekatwa kwa kitendo cha kuiba kuku.

Basi vijana kama kawaida wamemgusagusa kweli hadi mdomo umekuwa kama wa kiboko mnyama, sikutaka kuwa nyuma! nikashika kiboko kutoa machungu ya matukio ya wizi niliowahi kutendewa, nilimchapa kweli tena fimbo za mgongoni na kichwani. Kisha nikaamua kuondoka baada ya kuwa nimewapigia police na wamewasili eneo la tukio.

Wakuu, nimefika nyumbani nikatafakari kitendo nilichomfanyia huyo dogo roho inaniuma sana. Najiuliza maswali mengi sipati majibu! Najiskia mkosaji sana japo ni kweli huyo dogo kaiba na kwa maelezo yake si mara moja, najiuliza kulikuwa na haja gani ya kushiriki ktk kutoa adhabu? Ni kwanini sikujihangaisha kufahamu shida inayopelekea huyo dogo aibe?

Bahati mbaya sana nimefika nyumbani namwelezea wife nae kanilaumu. Wakuu najiskia mkosaji sana! Sijui nifanyeje nipate amani.
 
Kuna typing errors kidogo, "amekamatwa" na si "kukatwa" sina utaalamu wa kusahihisha uzi ukishaenda hewani.
 
Isamehe nafsi yako! Kila mtu ni mkosaji, na wapo wanaokosea zaidi ya hapo. Uzuri ni kuwa umeona ulipokosea na umejutia, kitu ambacho chaonesha bado hujapoteza utu wako. Tubu kwa Muumba wako, halafu jipe msamaha mwenyewe! Na next time ukikutana na tukio kama hilo ufanye tofauti na ilivyokuwa awamu hii.
 
Nimekuelewa mkuu, thanks
 
Tubu kwa dhati na kwa kuugua mbele za Yesu Kristo mwombe akusamehe yeye ndiye anayeweza ku-solve kesi hizo kwani dogo akifa na wewe una share yake kwenye kifo na hakuna 50% share kwenye kifo, share zote kwenye kifo au kosa ni 100%.
 
Pole.
Unaweza kumfuatilia dogo pia kujua ana hali gani sahivi.Na ukampa kitu kitakachofanya aondoe kinyongo nawe.Maana ni wazi kama yupo hai atakuwa na kinyongo nawe japo hakufahamu.Mkipatana vizuri + kuomba toba kwa Mungu wako nadhani amani ya moyo wako na wa mkeo itarudi 100%.
Ila pia unatakiwa ukae mbali na hii michezo.Wameuawa watu wengi wasio na hatia!
 
Kuna siku kanisani kwetu mama mmoja alitoa ushuhuda kuwa mwanae ni mwizi sana na mdokozi ni mtoto mdogo wa miaka 12 lkn wao wana uwezo yani hakosi chakula wala daftari lkn mwizi tabia hyo kaitoa wap hakuna jibu kesha pigwa sana na majirani nusura kufa lkn mwizi tu sasa mchungaji alipomuombea yule mtoto ikaonekana kuwa ametupiwa majini awe mwizi nikajifunza kitu kumbe si wezi wote wanapenda kuiba ipo nguvu yamapepo yanayomfanya aibe japo pia wapo poa wezi kihalisia kuanzia hapo nikawa nikisikia.mwizi namuombea kama ni pepo limtoke kwa Jina la Yesu awe sawa.
 
Pole.
Unaweza kumfuatilia dogo pia kujua ana hali gani sahivi.Na ukampa kitu kitakachofanya aondoe kinyongo nawe.Maana ni wazi kama yupo hai atakuwa na kinyongo nawe japo hakufahamu.Mkipatana vizuri + kuomba toba kwa Mungu wako nadhani amani ya moyo wako na wa mkeo itarudi 100%.
Ila pia unatakiwa ukae mbali na hii michezo.Wameuawa watu wengi wasio na hatia!
Thanks mkuu, hiki ulichokisema ndio kilikuwa kichwani mwangu, nafikiria kufatilia hatma ya huyo dogo nione jinsi ya kumsaidia kama ni shida ndio zinamfanya aibe
 
Tubu kwa dhati na kwa kuugua mbele za Yesu Kristo mwombe akusamehe yeye ndiye anayeweza ku-solve kesi hizo kwani dogo akifa na wewe una share yake kwenye kifo na hakuna 50% share kwenye kifo, share zote kwenye kifo au kosa ni 100%.
Dah! Mungu anisamehe, nitaendelea kutubu bila kukoma hadi amani ya nafsi itaporejea.
 
we we umetenda Mabaya mangapi? Nani alikuadhibu?, Huyo dogo yawezekana ni family atmosphere, Au mazingira au vinasaba,toa boriti kwenye jicho lako kwanza.... Hakikisha unamsaidia huyo dogo fimbo haisaidii hapo
 
Kwa nini ulimchapa wakati huna hakika hata kama kweli aliiba? Hivi ujasiri huu mnapataga wapi?
Na heri kwako hakuuawa ingekuhaunt for life, ukome na uanze campaign against “mob justice”Mungu mara nyingi huwa ana namna zake za kusema na kuassign mtu mtu to raise awareness labda katumia mbinu hiyo kwako.
You might save lives!

Baada ya kukupa vipande vyako then pole!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom