Ronee
Senior Member
- Jun 1, 2018
- 156
- 155
Natumai mu wazima watoto wa mama Tanzania.
Leo nilikuwa nakatiza mitaa flani nikitokea kwenye matembezi mafupi, mitaa hiyo haijachangamka sana kwa maana ya wakazi wake wachache, ghafla nikasikia kelele na heka heka za hapa na pale, watu hawakuwa wengi. niliposogea eneo hilo nikakuta ni dogo flani wa miaka kama 16-17 amekatwa kwa kitendo cha kuiba kuku.
Basi vijana kama kawaida wamemgusagusa kweli hadi mdomo umekuwa kama wa kiboko mnyama, sikutaka kuwa nyuma! nikashika kiboko kutoa machungu ya matukio ya wizi niliowahi kutendewa, nilimchapa kweli tena fimbo za mgongoni na kichwani. Kisha nikaamua kuondoka baada ya kuwa nimewapigia police na wamewasili eneo la tukio.
Wakuu, nimefika nyumbani nikatafakari kitendo nilichomfanyia huyo dogo roho inaniuma sana. Najiuliza maswali mengi sipati majibu! Najiskia mkosaji sana japo ni kweli huyo dogo kaiba na kwa maelezo yake si mara moja, najiuliza kulikuwa na haja gani ya kushiriki ktk kutoa adhabu? Ni kwanini sikujihangaisha kufahamu shida inayopelekea huyo dogo aibe?
Bahati mbaya sana nimefika nyumbani namwelezea wife nae kanilaumu. Wakuu najiskia mkosaji sana! Sijui nifanyeje nipate amani.