Nimepotelewa jamani

Kakati

Senior Member
Apr 11, 2009
167
47
Habari za leo ndugu zangu. Nina huzuni nimeibiwa begi lenye laptop computer, vitambulisho vyangu vingi na hati zingine. Niliiweka chini ndani ya ukumbi wa Diamond tulipokuwa kwenye Graduation za wahitimu wa Aghakan. Nilitoka kumpiga picha mke wangu akiondoka ukumbinu alikuwa miongoni mwa wahitimu. Niliporudi watu walikuwa wametawanyika na begi sikulikuta! Natamani kama nikipata vitu vyangu vyote au baadhi. Nimetoa taarifa Slander Bridge police station. Mwenye njia yoyote nyingine anisaidie. Nimechanganyikiwa.
 
pole best, next time usijiamin sana hasa sehemu ya watu wengi bora ungelibeba tu!
Pole sana kwa Mara nyingine
 
Mkuu nibora ungeweka hata majina ya vitambulisho ulivyo poteza na hiyo itasaidia hata kwa yeyote anaweza akaviokota iwe rahisi kuvitambua aiseeee.... kwasababu kwa uzoefu wangu kwa hawa wezi ni kwamba, atachukua vile vya thamani na visivyo vya thamani atavitupa.
Pole sana mkuu

(alafu kuna member anatumia avatar yangu pasipo idhini )
 
Umehitimu, mkeo pia amehitimu.
nyinyi ni wasomi,
Licha ya ukumbi wa kifahari na ni mmiliki wa laptop computer..

LIPIA TANGAZO...

NA pole kwa kupotelewa mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom