Leo asubuhi nikiwa nimepanda treni ya saa mbili tulipofika kamata tunashuka mara treni likaondoka. Watu kama 30 kwenye behewa letu tukawa hatujashuka. Hali hii ilizua zogo. Tukawa tumefikishwa stesheni bila kupenda. Nikauliza kwanini tumepitilizwa. Tukaambiwa eti uzembe wa mkata tiketi . Nikauliza mbona dereva asiambiwe kwamba watu hawajamaliza kushuka? Tukaambiwa radio call ipo behewa la kwanza na mwisho. Sasa jamani hela zote wanazopata wanashindwa nini kuweka radio call kila behewa. Halafu toka wameanza kuoperate hawajifunzi tu!