Nimepita Powerbreakfast ya Radio Clouds mgogoro wa Dangote

Bibititi1

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
464
218
0951ef91e030d694f9c543526fe7470c.jpg
 
naona kama kuna ugomvi wa maslai kati ya machumu na bi ester! (naruhusiwa kukosolewa)
 
Nimesikiliza kwa makini sehemu ndogo tu ya mahojiano hasa huyo Esther, nadhani huyo dada hajui kwamba kitendo cha 'Prof. Bwana yule' kukubali kuhojiwa na Kipanya ndicho kilimvua uprofesa wake sasa naye kaja kuhojiwa na Kipanya bila kujua anaongea na akili kubwa ambayo ni zaidi ya hayo mamikrofoni, mameza na stafu wengine aliowakuta hapo.
Huyu dada ukimsikiliza kwa makini inaelekea anawakilisha kundi la 'expected loosers', anadaia ndiye coordinator lakini akiulizwa 'ametumwa' na Dangote au Serikali hataki kuwa wazi. Kilicho wazi ni kuwa kuna uwezekano awamu iliyotangulia ina maslahi ya ziada kwenye hii project na ni wazi calculations zao zilisha 'tabiri' ni nani angekuwa rais miaka kumi ambayo ingefuatia ambapo mambo hayakwenda sawa.
Tunapitia wakati mgumu kiuchumi lakini kama nilivyomsoma Ali Mufuruki tulikokuwa tunaelekea siko hivyo hatuna budi tupitia wakati huu ili kutengeneza mwelekeo sahihi. Suala la Dangote litafunua siri za uwekezaji wa Kitanzania ulivyo wa hovyo hovyo na ni suala la muda!
 
Wako hewani tuendelee kuwafuatilia

Sijui kuna nini tu katika sakata hili

Yaani ni kama sakata la Tegeta Escrow Account la za umma ama za watu binafsi....

Kizungumti hiki.....
 
Tatizo ni gas tu na si makaa ya mawe au nini, kama aliahidiwa kupatiwa gas ya Mtwara na hajapewa basi ndiyo mgogoro huo
 
asee hii issue ya Dangote ipo hot sana kilA mtu ana mrushia mwenzake mpira sikilza powerbreakfast nw uchuje kati ya serikali na Dangote yupi wa kulaumu
 
Huyu bi Esther anaonekana kuna kitu kazulumiwa maana anadai hasaminiki, na kua siku ya uzinduzi wa kiwanda hakupewa room, na pia anataka kujikweza sana anadai yeye ndo kamleta dangote, pia anadai kuna watu wa Kati wanamtibua dangote lkn amegoma kabsa kuwataja
 
Huyu bi Esther anaonekana kuna kitu kazulumiwa maana anadai hasaminiki, na kua siku ya uzinduzi wa kiwanda hakupewa room, na pia anataka kujikweza sana anadai yeye ndo kamleta dangote, pia anadai kuna watu wa Kati wanamtibua dangote lkn amegoma kabsa kuwataja
mimi kwa uwelewa wangu bi ester alikuwa dalali lakini mzigo ulivyokamilika hakupewa nafasi aliyokuwa anategemea
 
Kwani hawa clouds wanajua nini?hakuna wanachojua hawa wanaweza kuandaa matamasha ya fiesta tu ndicho wanachofahamu
 
Kwani hawa clouds wanajua nini?hakuna wanachojua hawa wanaweza kuandaa matamasha ya fiesta tu ndicho wanachofahamu

Defenetely, hakuna wanachojua

Lakini kosa lao ninaliona pamoja na kutokujua kwao ni kuleta watu wasio sahihi ktk kujadili ishu nyeti kama hii!!
 
Back
Top Bottom