Nimepita maeneo kwenye taasisi moja ya serikali nikakuta mashine ya kuzalisha barakoa inafungwa

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Hii ni hatua nzuri ya kufanywa na serikali maana sisi ni wadau wa kupaaza sauti juu ya mwenendo wa kusuasua wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa COVID 19. Kuna sehemu nimepita kama nilivyoeleza kwenye heading na kushuhudia mashine hiyo ikifungwa tayari kwa kuanza uzalishaji wa barakoa.

Lakini mimi nina swali moja kwa serikali.
Ikiwa Rais mwenyewe anapinga matumizi ya barakoa inakuwaje analeta mashine hiyo?

Jibu:
Watanzania tujiandae kuletewa sheria kali ya kuvaa hizi barakoa zitakazozalishwa na serikali. Serikali inachotafuta ni mapato na siyo nia ya dhati ya kuwakinga wananchi. Ingekuwa ni hivyo Rais angekuwa mstari wa mbele kuhimiza matumizi ya barakoa hapo kabla.

Hatimaye tunaenda kupata chanzo kingine cha mapato. Jamani acheni nipambane kugawa hivi vitambulisho vya machinga nisije kutumbuliwa buree..Ugali ni mtamu bandugu!
 
Raisi ameishasema vifaa vya kupambana na Corona LAZIMA vipitie Wizara ya Afya.
Kama unataka kutoa msaada utaenda kununua kwenye ghala la serikali ,ukifanya kuwa kiziwi ukaleta misaada kutoka nje,havitapita kirahisi.Magufuli hataki umashuhuri kwenye swala la Corona kwa kigezo cha msaada.
 
Umeleta mada nzuri ila nimehisi tu mtazamo wako wa jambo lolote lifanywalo na serikali lazima uwe(-) na imekuwa hivyo kweli.
 
Umeleta mada nzuri ila nimehisi tu mtazamo wako wa jambo lolote lifanywalo na serikali lazima uwe(-) na imekuwa hivyo kweli.
Amepinga wavaa barakoa kisha analeta mashine ataanza kulazimisha wanunue apate mapato. Kodi kwanzaaa
 
Duh, wewe jamaa hunaga jema kwa serikali.

Na kwa taarifa yako hilo unalowaza halitatokea.
 
Mashine unayozungumzia cherehani au kunamshine special

Kumbe Tanzania tunaweza kutengeneza vya kwetu....

Nimewaza huu ugonjwa ukiondoka duniani kumbe vile viwanda vya barakoa za vitambaa vinaweza kuwa viwanda vya kushona nguo kwa Bei rahisi....
 
Hii ni hatua nzuri ya kufanywa na serikali maana sisi ni wadau wa kupaaza sauti juu ya mwenendo wa kusuasua wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa COVID 19. Kuna sehemu nimepita kama nilivyoeleza kwenye heading na kushuhudia mashine hiyo ikifungwa tayari kwa kuanza uzalishaji wa barakoa.

Lakini mimi nina swali moja kwa serikali.
Ikiwa Rais mwenyewe anapinga matumizi ya barakoa inakuwaje analeta mashine hiyo?

Jibu:
Watanzania tujiandae kuletewa sheria kali ya kuvaa hizi barakoa zitakazozalishwa na serikali. Serikali inachotafuta ni mapato na siyo nia ya dhati ya kuwakinga wananchi. Ingekuwa ni hivyo Rais angekuwa mstari wa mbele kuhimiza matumizi ya barakoa hapo kabla.

Hatimaye tunaenda kupata chanzo kingine cha mapato. Jamani acheni nipambane kugawa hivi vitambulisho vya machinga nisije kutumbuliwa buree..Ugali ni mtamu bandugu!
Chapa kazi acha kubwabwaja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio siri hii nchi inaongozwa na WAJINGA wanaosababisha wananchi wote tuonekane wajinga na wapumbavu kama wao.

Unapingaje watu kuvaa barakoa kwa kipindi cha hatari kama hiki?

Sent using Jamii Forums mobile app

Halafu unasikia huyo huyo akishauri watu wajikinge na kufuata ushauri wa kitaalamu.

Ujinga katika taifa letu, ni mkubwa sana! Hata unapokuwa katika combo na fitna, uzandiki na figisu!! So sad!
 
Back
Top Bottom