Nimepigwa vibao na mke wa jirani yangu kwenye kituo cha basi.

Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo

Pole bujibuji ndo maisha hayo bana...
 
Buji nachelea kuamin kauakwel ka hii story!! Kama ni kwel bas pole!! Unajua mtu ambaye yuko funny kama wewe akiwa serious kuamin kazi! Anyways achana naye! Ni busara kwake mwenye hekima kusamehe makosa.
 
pole buji, wanakuonea kwa sababu wewe mpole, sijui ingekuwaje kama vibao hivyo angepigwa NN Nyani Ngabu.
 
Muhoji mumewe; yawezeka alaikwidwa kama wewew na kuona kwamba ajitete kuwa weye ndio chanzo ku save kipigo!
 
Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo

hahhahahaha haiwezekani usingiziwe itakua kweli.. ndo uache haya matabia sasa..pole kwa fedhea iliyokukuta natumai hautarudia tena
 
ndio aniingie kwa style ya udhalilishaji?
Pole Bujibuji ila huwezi jua alichoambiwa na mumewe unaweza kuta hajarudi nyumbani siku 3 na huyo mwanaume hakutegemea kuwa hizo habari zitakufikia sasa sijui atakuangalia je akikiuona..Duniani kuna mengi
 
Duh! inasikitisha sana, sasa ina maana umekubali tuhuma hizo? huoni ingekuwa ni busara kwenda kwa rafiki yako na kujadili juu ya fedheha hiyo uliyofanyiwa na mkewe?

Mimi hapa sielewi kabisa, yaani mke anaweza kuamini kabisa kuwa mumewe ambaye ni mtu mzima na akili zake timamu kwamba anaweza kushawishiwa na watu au mtu fulani kufanya jambo bila utashi wake! basi huyo hafai kuitwa mume kwani akili zake ni za kushikiwa na haiyumkini inaweza ikatokea akashawishiwa kuwa shoga na akakubali...........

It is normal for human beings to externalize our problems........... That is what she actually did.
Kama angekuwa mwanamke kweli, basi angempiga mumewe......
 
Badili muonekano wako,. Ukiona mtu amekufanyia jambo tayari ameshakupima na kuona anao uwezo wa kukufanyia hivyo. Ndio maana hakuna mtoto mdogo anayemrushia ngumi baba yake. Maintain your status.

Eeh, halafu nilitaka kusahau. Yawezekana huyo mama anakutaka ila wewe unajifanya mgumu. Unajua wanawake bana full visa ikiwa huwaelewi. Mimi secretary wetu alinipeleka polisi kwa pingu akidai nimemuibia lkn walipombana kwa maswali akasema mimi namuudhi sana kwa kuwa ninajisikia. Akaangua kilio kituoni mpk maafande wakatokwa na jasho kwa kushindwa kujua waandikeje statement
 
Na pia yawezekana hujui kuishi na majirani. Mwenzetu washawasha ni mjuzi wa mambo haya. Hata chupi za majirani zake wa kike zikianguka bafuni huzisuuza vizuuuri akazianika.

Braza washa wasap meeeeen! Long tym no hia you braza wea aa yu men?
 
Ama kweli ukishangaa ya Mussa........nimesikia ya wanawake kusutana. Hii ya kwako kaka mpya na kubwa. Pole sana bro mshukuru muumba kwa kutopandisha ghadhabu maana ungeweza fungua bucha bure.

Go report shambulio la kudhuru mwili......taratibu kwa msaada wa mjumbe umsongeshe kunakohusika atoe maelezo na ajue kuwa "law of the jungle" inapingwa. Taratibu zipo na zifuatwe
 
Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo

Buji nashindwa kukupa pole au kukucheka, manake sijui kama ni kweli au utani!! any way pole sana bana!!
 
Back
Top Bottom