Nimepigwa vibao na mke wa jirani yangu kwenye kituo cha basi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimepigwa vibao na mke wa jirani yangu kwenye kituo cha basi.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, Dec 7, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,165
  Trophy Points: 280
  Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
  Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
  Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
  Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
  Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
  Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  pole sana, huyo mwanamke stress zake anataka kukushushia wewe. kwani mumewe ni mtoto mdogo mpaka umpeleke? na wewe acha urafiki na wanaume waliooa, hususan majirani haswa wenye ndoa zenye migogoro
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,165
  Trophy Points: 280
  mumewe sio rafiki yangu, huwa tunasalimiana kimbalimbali tu. Na wala nilikuwa sijui kuwa huwa anakunywa brown water
   
 4. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aisee ningekuwa mimi ningemvurunda mbaya dah...uje tu na kuanza
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Duh! inasikitisha sana, sasa ina maana umekubali tuhuma hizo? huoni ingekuwa ni busara kwenda kwa rafiki yako na kujadili juu ya fedheha hiyo uliyofanyiwa na mkewe?

  Mimi hapa sielewi kabisa, yaani mke anaweza kuamini kabisa kuwa mumewe ambaye ni mtu mzima na akili zake timamu kwamba anaweza kushawishiwa na watu au mtu fulani kufanya jambo bila utashi wake! basi huyo hafai kuitwa mume kwani akili zake ni za kushikiwa na haiyumkini inaweza ikatokea akashawishiwa kuwa shoga na akakubali...........
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hapo unatafuta kesi, Wabeijin wanalindwa na sheria kama nini........!
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu yamekukuta makubwa,kuna ukweli ndani yake?
   
 8. M

  MyTz JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hahahahahahahahahahah........
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  pole sana mkuu

  ila hiyo kesi haitaishia hapo mpaka kieleweke,anakugambira stupid mbele ya watu,hapana rudi home katulie then chukua hatua,naimani huyo mama bado anahasira nawe,inakubidi ukae na mume wake myaweke sawa mkuu
   
 10. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Weak women are like that. Hapo ukute mume wake alijitetea kua alikua na wewe ila hajamwambia mume wake chochote, anakurukia wewe. Ndio kama ile thread imeanzishwa eti mtu anawakanya wanawake wa JF kuchat na mume wake.
  Hivi kwa nini wanaattack watu wengine na sio waume zake? after all he is the one who swore to love her forever, sio hao wanawake au jirani yake...
  Pole sana Bujibuji. Umefanya sawa kutomjibu. Cha msingi wewe unajua uko clean.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,165
  Trophy Points: 280
  ndio niko njiani naelekea kwake, ila kwanza nataka nimpitie mwenyekiti wa mtaa ili twende wote
   
 12. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hii bibi ya jirani yako haiko sawa kabisa. yaani umalaya wa mumewe ufacilitate wewe?. ingekuwa vema angempiga mumewe. kwa hali yoyote ile

  bujibuji waweza shikishwa adabu kwa kupigwa makofi kweli?.
  pole kwa kuaibishwa anyway!. peleka hii bibi ya jirani yako kortini
   
 13. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  inawezekana anakutaka kisirisiri ila we unampotezea
   
 14. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu nikilinganisha posts zako na tukio lilikutokea nahisi kama kuna ka ukweli ndani yake.
   
 15. M

  MyTz JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkuu una kila 7bu za kumshukuru Mungu...
  ungesingiziwa umemuibia simu (kesi ya wizi) hapo town ingekuwaje??? nadhani kifo kingekuhusu...
  pole sana kwa hiyo dhahama mkuu...
   
 16. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu huyo mama amekumaindi tu anatafuta upenyo wa kukuingia.
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  AMEAMBIWA UNAMKAMEROON MUMEWE, kashindwa kukwambia tu
   
 18. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he pole kaka....stress zinamsumbua hizo
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,165
  Trophy Points: 280
  nina finger prints shavuni, ila lazima nimlaze ndani leo
   
 20. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,165
  Trophy Points: 280
  ndio aniingie kwa style ya udhalilishaji?
   
Loading...