Nimepigwa fine kwa kuvuka zebra cross, kwenda kulipia naambiwa karatasi haina ref number

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,400
2,000
Hii system ina mapungufu.

Ilipaswa fine itozwe kwa dereva kupitia leseni yake na siyo mmiliki wa gari, kwasababu naweza kumpa mtu gari langu akaandikiwa fine lakini akanyamaza bila kulipa wala kunitaarifu.

Sijui lkn wao wa track makosa kwa kutumia namba ya gari. Ingawa waliniambia kuwa nikamtafute aje alipe mimi sina kosa lkn lazima gari libaki hapo. Kwa kuchukulia kuwa kijana ni mtoto wa jirani nikaona ni bora nilipe yaishe.

Nafikiri wanatega mitego sehemu mbali mbali za jiji, wanatumia generator na kamera ambayo inawekwa mita kama 100 kutoka walipo halafu mtu wao ana-monitor kwenye laptop na kuwapa taarifa pindi gari inayodaiwa inapopita. Nilikaaanao sana ikipita gari ile system inasoma namba kama inadaiwa backgroud ya monitor yao inakuwa Nyekundu ama sivyo inakuwa white
 

Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,556
2,000
Naomba ushauri juzi Ijumaa nimepigwa fine kwa kuvuka zebra cross nikaandikiwa kulipia fine tshs. 30,000 tatizo nimeenda kulipia wakaniambia kwamba kile kikaratasi nilichopewa na traffic hakina reference no, nikaamua kunyamaza mpaka leo sijalipia,au nakosea wanajamvi kama hawana reference watanikamatia wapi
Ukimwona traffic yeyote unamwonyesha tu atakupatia ambayo ina reference number. Usipolipa baada ya siku saba inaanza kuhesbu faini ambayo inaongezeka kila siku. Lipa kabla ya siku saba kuisha.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,879
2,000
Inategemea mazingira mfano kwa tazara pale kuna zebra kabla ya mataa mandela road au pale buguruni sheli sasa utakuta mataa/traffic ameruhusu na baadhi ya wananchi wanajipendekeza kuvuka hapo unategemea nini na hadi kuitwa tena na traffic sio chini ya dk 20, wito wangu wananchi nao wawe makini na vivuko/zebra cross zilizo busy/sumbufu waweke vivuko vya daraja ie manzese
Kwangu mimi naona sehemu za zebra crossing zenye mgongano wa madeva vs waenda kwa miguu ni zile sehemu ambazo hazina taa za kuongozea magari bali zina alama ya zebra pekee. Haya maeneo ni hatari sana na madereva wengi Bongo hawajali bali huongeza mwendo na kupiga honi kali wanapoyafikia.
 

Step by step

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
1,096
2,000
jamaa wanakusanya mapato kwa ubunifu sana enzi za jk hizi mambo hazikuwepo yani tunaendesha gari kwa mashaka mashaka sana maisha ya kuviziana
 

kazikwanza1981

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
1,579
1,500
Very simple mtafute traffic police mwenye kile kimashine akupe ref number. Hiyo wamekuandikia toka kwenye driving licence.
 

kiliochangu

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
1,157
2,000
Naomba ushauri juzi Ijumaa nimepigwa fine kwa kuvuka zebra cross nikaandikiwa kulipia fine tshs. 30,000 tatizo nimeenda kulipia wakaniambia kwamba kile kikaratasi nilichopewa na traffic hakina reference no, nikaamua kunyamaza mpaka leo sijalipia,au nakosea wanajamvi kama hawana reference watanikamatia wapi

Mimi hawa polisi siwaelewi. Kuna siku traffic alinipiga fani ya 60,000 kwanza alinionea tu. akataka nilipe kwa kuwa wakati natoa leseni aliona pesa. kwa hasira nilimkatalia nikaona acha nikalipe Max-malipo. Kitu ambacho sijaelewa mpaka leo, nlipoenda kulipia wakaniambia mbona hiyo faini naonekana umeshalipia na udaiwi? Mpaka leo sijalipa maana nilijaribu kungiza leseni na namba ya gar inaonesha sidaiwi. Ushauri nadhani hawa watu wanatuchezea na hela tunazolipishwa huwa hazifiki iwapo utawalipa cash.
Ukikumbana nao bora wakuandikie ukalipe max malipo kulipo kuwapa wakajfanya wanakupa risiti, maana hii mpaka leo sijailewa
 

dalumi

Senior Member
Oct 19, 2013
138
250
wadau mimi nilipigwa fine imepita wiki mbili sasa. cha ajabu kabla wiki haijaisha nikawa naangalia kupata reference namba kwa kutumia ussd code yao ya *152*75# inaniambia leseni wala gari hazidaiwi. leo nimecheki pointi za leseni zinasoma 15 ambayo ni kua nimefungiwa leseni kwa miezi sita. asa hapa sielewi nifanye kipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom