Nimepewa zawadi ya Condom na rafiki yangu wa kike

Lawrichie

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
753
2,044
Poleni na majukumu wakuu.

Nipo kwenye mahusiano ya kirafiki na binti mmoja hivi kwa miaka mitatu sasa. Ni binti ambaye tunaelewana sana karibu kila kitu. Tunasaidiana, tunashauriana, tunapendana, tunaheshimiana sana kama marafiki, lakini zaidi tunaongea kuhusu kila kitu.

Kilichonifanya niandike uzi ni kwamba, jana jioni alinipigia simu, aliniomba nikitoka ofisini kwangu nipitie ofisini kwake kuna mzigo wangu kutoka kwake. Nikamwambia hakuna shida nitapitia...

Huyu binti ameolewa, mume wake ananifahamu vizuri tu na anajua kuwa mimi niko karibu na mke wake. And of course mume wake amekuta tayari sisi urafiki wetu umeanza kabla yake. Jamaa ni mtu poa sana and sometimes huwa tunaangalia football pamoja.

Sasa kawaida huyu jamaa kila jioni lazima amfuate huyu mke wake ofisini baada ya kufunga. Ikitokea hajamfuata basi binti huwa anatafuta usafiri mwingine wa kuwahi home.

Sasa Turudi kwenye lengo la uzi. Mimi baada ya kufunga ofisi ikabidi nipitie ofisini kwa bibie kama alivyoniomba. Ofisi zetu haziko mbalimbali sana. Kufika nikakuta ndio anafunga, kama kawaida tukataniana pale na kucheka kidogo. Akaniambia leo mume wake hayupo amesafiri kidogo so hatamfuata. Basi akafunga tukaanza kuelekea sehemu usafiri unapopatikana huku stori za hapa na pale zikiendelea kawaida.

Baada ya kufika pale akapata usafiri, kabla hajapanda akafungua begi lake akatoa pacel iyofungwa vizuri akanikabidhi. Nikapokea na asante juu, basi tukaagana na mimi nikaelekea kwangu. Baada ya kufika home nikafanya mishe zangu kama kawaida baada ya kurudi.

Baadae nikampigia simu kumuuliza kama amefika salama, akasema ndio basi tukaagana. Ndio nikakumbuka kuwa nilipewa mzigo halafu sijaangalia bado kuwa ni nini. Nikauchukua ili nifungue, la haula nakutana na BOX LA CONDOM ZA ROUGH RIDER, halafu kuna ka-note ameandika pembeni "KINDLY USE THEM RESPONSIBLY''.

Sasa wakuu nimetafakari mpaka sasa hivi sijapata jibu. Kwa nini iwe Condom na sio zawadi nyingine, amenionaje au anafikiria nini kuhusu mimi? Sijamuuliza kwa nini amenipa zile Condom tena na onyo juu. Nimekuja huku nisome mawazo yenu kuhusu hili..

Karibuni kwa ushauri...
 
Poleni na majukumu wakuu.

Nipo kwenye mahusiano ya kirafiki na binti mmoja hivi kwa miaka mitatu sasa. Ni binti ambaye tunaelewana sana karibu kila kitu. Tunasaidiana, tunashauriana, tunapendana, tunaheshimiana sana kama marafiki, lakini zaidi tunaongea kuhusu kila kitu.
Kuna demu unamtaka ila ameungua na yy anajua ila sasa ni rafiki yake pia kwaio kukueleza ukweli hawezi so amekupa kinga mapemaa usijeshika miwaya😎
 
Kilichonifanya niandike uzi ni kwamba, jana jioni alinipigia simu, aliniomba nikitoka ofisini kwangu nipitie ofisini kwake kuna mzigo wangu kutoka
Mke wa mtu unamuita binti. Yaani mke wau hutakiwi kuwa na ukaribu naye hata kwa bahati mbaya, huo ukaribu ulitakiwa uishe siku ya harusi
 
Una urafiki wa karibu hivyo na mke wa mtu?

Anyway amekupa utembee nazo, ili ukiingia 18 za mumewe na njemba zngne, wapate utelezi.

Acha ukaribu na mke wa mtu hivyo, tafuta mpenzi wako mgandane hivyo man.
Mume wake amesafiri.

Amekupa zawadi ya Condom.
Mke wa mtu unamuita binti. Yaani mke wau hutakiwi kuwa na ukaribu naye hata kwa bahati mbaya, huo ukaribu ulitakiwa uishe siku ya harusi
Acha shobo na wake za watu, hata kama mlikua marafiki wakubwa kiasi gani, Je wewe unaweza kuvumilia mke wako akiwa na urafiki wa karibu na mwanaume mwingine?

Ningekua mume wa huyo mwanamke ningeshakupa warning zaidi ya x3 na ningekua nishakuchapa makofi

yaani wanaume wote hawa wameumia kisa mwanaume mwenzao kudate na mke wa mtu?

naona mnavo ashum kwa wake zenu😄😄 poleni

mambo ya 50/50 hayo hakuna mwanamke asie na mchepuko😄😄😄

penzi la kwanza halifi linazimiaga😄
 
Kuna demu unamtaka ila ameungua na yy anajua ila sasa ni rafiki yake pia kwaio kukueleza ukweli hawezi so amekupa kinga mapemaa usijeshika miwaya😎
Hakuna demu namtaka ambaye yupo karibu nae..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom